Kwa wanao hamia vyama vingine haswa wakitokea magamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanao hamia vyama vingine haswa wakitokea magamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Apr 16, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thread hii ni kutokana na habari ya mwenyekiti wa UVCCM Arusha Bw.Millya kutangaza kujiondoa magamba.

  Tatizo la hawa jamaa wanao hama kutoka magamba ni kwamba mbona wanafanya hivyo tu pale wanapo ona dalili za kushindwa katika chaguzi zao za ndani? pia pale wanapo hama wakienda CDM ama kwingineko wanataka moja kwa moja wawe wagombea wa nafasi husika? Hawajui kuwa tayari kuna watu wamo CDM miaka na wana uwezo mkubwa? Inatakiwa wakitoka watokako kwanza waende wakae wakijue chama na mwenendo wao mzima kimaisha uendane na wa chama husika na ukubalike ndipo wagombee. Mfano mzuri na fundisho kwa vyama vinavyo pokea wahamiaji/wakimbizi ni Mh.Shibuda, huyu jamaa amekuwa mwiba kwa CDM kiasi wanamsubiri amalize muda wake 2015 kisha arudi atokako kule magamba. Wao wanaweka maslahi mbele yanapo hujumiwa ndipo utasikia eti "nahamia" tena CDM. Kwa nini wasiende TLP,CUF na kwingineko? watu wahangaike kujenga chama wao waje na kula matunda tu haiwezekani.

  Mtu ambaye ni patriotic huhama pale tu anapo ona chama husika kimepoteza dira, uwajibikaji na sera zisizo mbadala kama ilivyo kwa magamba sasa. Hii biashara ya kuhama wakati wa uchaguzi hatuitaki. Kama mtu ana nia ya kuhama afanye sasa tena siyo kwa mizengwe ndani ya chama chake. Mwenye nia ya kuhama magamba afanye mapema siyo kusubiri mpaka 2015 watakapo anza kuenguana kwenye vyama vyao ndipo utasikia eti "nahamia CDM" Mjue huko mnako kwenda kuna watu tena waliobobea kwa sera, imani na mtizamo wa chama. Kwa hiyo Millya ukitaka kwenda CDM ama kwingineko karibia. Lakini uwe mwanachama wa kawaida kwanza kama wengine mpaka pale chama kitakapo kuona fikra na mtizamo wako ni wa kimapinduzi ya kweli na siyo njaa inayo kusumbua baada ya kuona maslahi yako yana hujumiwa.
   
 2. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu nao ni ujumbe wakuzingatiea na kunauwezekano alitaka kugombea Arumeru akatoswa ndo ikawa sababu so watu hawa tuwatizame kwa macho mawili kwanza
   
 3. Non stop

  Non stop Senior Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hili ni swala wana CDM inabidi kujiuliza na kua nalo makini sana, kwa nini wanapochafuka huko wanaona pa kukimbilia ni CDM?..au ndo kusema shetani akizeeka anakua malaika?
   
 4. paty

  paty JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,251
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  CDM makini naamini majembe yanacuja vizuri , toka kuteleza kwa bwana SHIBUDA sijasikia chochonyingine , Viva CDM
   
Loading...