Kwa wanaioijua Tanzania vizuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanaioijua Tanzania vizuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kanyafu Nkanwa, Sep 24, 2010.

 1. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Marekani Yaimwagia Sifa Tanzania

  [​IMG]Rais wa Marekani,Barack Obama

  Na Mgaya Kingoba.

  MAREKANI imesema kwamba Tanzania ni moja ya nchi inazozipigia mfano miongoni mwa nchi zinazoendelea, kwa uongozi bora na unaodumisha utawala bora na utawala wa sheria.Kwa mujibu wa Rais Jakaya Kikwete, Rais Barack Obama wa Marekani aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, nchini humo.

  Rais Kikwete alisema wakati akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye
  Uwanja wa Barafu mjini Rujewa wilayani hapa katika Mkoa wa Mbeya, kuomba kura kwa wananchi wa wilaya hiyo. Alisema muda mfupi kabla ya kuhutubia maelfu ya wananchi uwanjani hapo, alizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Leonhadt, na kumuelezea jinsi Rais Obama alivyoimwagia sifa Tanzania katika hotuba yake UN.

  “Kabla ya kupanda hapa jukwaani kuzungumza nanyi, mliniona nazungumza na simu…alikuwa Balozi wa Marekani, ananiuliza kama nimesikia hotuba ya Rais Obama jana usiku kwenye Umoja wa Mataifa,” alisema Rais Kikwete.“Nikamwambia niko huku nahangaika, nitasikia saa ngapi? Wakati mwingine niko hoi bin taaban hata kusikiliza redio au televisheni huna muda.“Ameniambia kuwa Rais Obama ameeleza misingi ya Marekani kusaidia nchi zinazoendelea, na mfano wake akatoa Tanzania.

  Akasema nchi yetu inaongoza kwa
  kujali utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimu NGO,s, na tunatawala vizuri,” Rais Kikwete aliwaeleza wananchi.

  “Kama siyo mimi na akina Mwandosya, nani mwingine anayemsifu,” alisema Rais Kikwete akimtaja Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, ambaye alikuwapo kwenye mkutano huo akiwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Mbeya.

  Alisema kauli hizo za Marekani kuisifu Tanzania, hazitoi yeye, lakini kila anapofanya hivyo, baadhi ya watu huhoji kwani kila mara na Marekani.


  “Nikisema sifa hizi zinazotolewa na Marekani, watu wanasema, ‘huyu naye na
  Marekani kila siku.’ Wanasema wenyewe, siyo mimi,” alifafanua Rais Kikwete.
  Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania tangu Rais Kikwete aingie madarakani miaka mitano iliyopita, ikitoa ufadhili mkubwa katika miradi mbalimbali ya sekta za elimu, afya, miundombinu na nishati.

  Chini ya Shirika la Milllennium Challenge (MCC), Marekani itafadhili miradi ya
  umeme katika mikoa sita nchini; itajenga barabara kadhaa ikiwemo ya Tunduma-Laela- Sumbawanga na hivi karibuni ilitoa vitabu 800,000 kwa ajili ya shule za
  sekondari nchini hasa kwa masomo ya sayansi.
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Namshangaa sana huyu rais wetu anajua fika kuwa aliye rafiki wa marekani leo ndiyo adui namba moja wa kesho.Anatakiwa ajifunze kwa Mseveni aliepewa sifa hadi kufanyiwa dhifa ya kitaifa iliyohudhuriwa na masenator wote, Kagame, TAYROL na wengine.
  Huyu jamaa anaanza kutuandaa kuwa maadui wa kesho wa marekani.PIGA CHINI 31 OCT
   
 3. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunataka maendeleo sio misifa!
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kumbe hata na yeye mwenyewe anajijua, nilijua lazima atutumia hotuba hii kwenye kampeni zake
   
 5. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tujipange ili tuondokane na utegemezi.
   
 6. n

  nonotza New Member

  #6
  Mar 11, 2013
  Joined: Mar 11, 2013
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello everyone

  i do not understand swahili, could you please anyone out there translate the topic?
   
 7. NURDIN.HAMIS

  NURDIN.HAMIS Member

  #7
  Mar 11, 2013
  Joined: Mar 9, 2013
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  How do you know if the words si in swahil?

  Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   
Loading...