Kwa Wanahabari na Wadau wa Habari

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Naomba kuwajulisha kuwa tunakaribia kuzindua gazeti la CHIMBUKO LETU litakalosambazwa mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Katavi na Ruvuma hivi karibuni.

Kwa umuhimu wa pekee kama una taarifa au fununu za jambo linalovuta macho na masikio ya wengi unataka liandikwe kwenye gazeti letu la Nyanda za juu kusini, liwe zuri au baya tujulishe. Sisi tutaifuatilia kwenye mamlaka husika ili kupata habari kwa kina na kuichapisha.

Gazeti hili litaboresha uwajibikaji wa viongozi kwa jamii na kwa wananchi pia litamulika utendaji mbovu na matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wa umma. Tumejipanga kuwa watetezi wa wananchi wanyonge na kuwafikia wasiofikiwa kirahisi na vyombo vingine huko vijijini. Sisi ni Sauti ya wasio na Sauti.

Kwa Habari na Matukio wasiliana na

Ahadi Mtweve,
Mhariri Mkuu,
Gazeti la Chimbuko Letu,
S.L.P 6464 Mbeya.
Tel. 0252502842, Mob/Whatsapp 0764660220
Email: amtweveone@gmail.com au chimbukonews@gmail.com
 
Back
Top Bottom