Kwa wanafunzi wote waliowahi kufukuzwa au wamefukuzwa vyoni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanafunzi wote waliowahi kufukuzwa au wamefukuzwa vyoni.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ALPHONCE LUSAKO, Jan 29, 2012.

 1. A

  ALPHONCE LUSAKO Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TANGAZO
  KWA WANAFUNZI WOTE WALIOWAHI KUFUKUZWA VYUO VIKUU
  NCHINI TANZANIA.
  Awali ya yote, tunapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, ambaye amekuwa nasi katika harakati za kupambana na maisha ya kila siku, pia kutupa ujasiri wa kusimamia haki kwa maslahi ya Taifa hili.
  Fikra huru za wasomi zidumu katika jamhuri ya muungano wa TANZANIA, kwani ukombozi wa Taifa letu kifikra unategemea sana fikra huru za wasomi.
  Tunapenda kuwataarifu wanafunzi wenzetu wa vyuo vikuu nchini ambao wamewahi kufukuzwa au wamefukuzwa vyuoni kwa kuonewa au kwa mabavu ya watawala wa chuo husika kwamba, tumepanga kuja kufanya mkutano mkubwa jijini DAR ES SALAAM, ili kujadili matatizo yanayotukumba sisi kama wasomi wa nchi hii na madhara ya uonevu huo ambao ulishafanyika, unaofanyika na ambao unaendelea kufanyika katika vyuo vikuu nchini. Ifahamike kuwa mtu yeyote Yule embaye anasimama kutetea maslahi ya wanyonge katika Taifa hili anachukuliwa kama mtovu wa nidhamu/mhalifu kitu ambacho kinahatarisha amani ya nchi yetu.
  Kitendo cha watawala wetu kutumia nguvu nyingi haswa pale wanapotumia mabomu na maji ya kuwasha kuzima fikra huru za wasomi vyuoni, ni kulizika Taifa hili, na kama kweli kitendo cha kuzima fikra huru za wasomi kitafanikishwa kwa 100%, ni ukweli kwamba kutakuwa hakuna haja ya kuwa na wasomi nchini.
  Tunaomba mwanafunzi yeyote yule ambaye amewahi kukubwa na mkasa husika atume jina lake, namba ya simu, email yake na chuo chake kwenye email iliyopo hapo chini. Ifahamike kuwa tunajipanga kuandaa mkutano mkubwa jijini Dar es Salaam ili kupaza sauti zetu kwa maslahi ya Taifa letu baada ya kukamilisha zoezi la kupata wahusika.
  Hii ni nchi yetu sote na si nchi ya wachache, hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria kwani nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria . sisi kama vijana wenye fikra huru ni lazima tupaze sauti dhidi ya uonevu unaotokea na ambao unasadikika kuendelea kutokea vyuo vikuu nchini.
  Ili kufanikisha zoezi hili, tunaomba ujumbe huu ufike kwa watu wote nchini kwa maslahi ya kukomboa fikra huru za wasomi.
  Contact: w.together@yahoo.com
  EMEKHA, IKHE.
  To be forwarded..
   
Loading...