Kwa wanafunzi kuanzia form 1 - form 4 mnaweza kufanya online examination

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
4,975
2,000
Mfumo wetu una shida kubwa na tunajua hilo ni tatizo lakini hatupo tayari kusimama na kufanya maamuzi ya kuufanyia kazi sababu kazi ya gharama kubwa inayoambatana na mabadiliko!

Tunapoongelea kubadili au kuboresha elimu mara nyingi huwa tunamuangalia mwanafunzi peke yake... lakini kiukweli tuna wadau wengi wakiwamo wataalamu wa elimu, walimu, zana za kufundishia na kujifunzia, miundo mbinu sahihi na mengine.... ambavyo vyote gharama zake ni kubwa sana

Pia serikali inakua na kigugumizi kwenye mabadiliko sababu mengi ya hayo mabadiliko hayafai kufanywa kidogokidogo bali kwa mara moja
Ila sababu serikali yenyewe imewasomesha watanzania, na watanzania hao wanayaona mapungufu na wapo tayari kuyafanyia kazi kwa support ya serikali sasa ni muhumi sana sasa kuamua kuweka plan na kutenga mafungu walau kila budget kuwe na pesa ya kufanya maboresho ya elimu ili kiasi kitakapotimia watekeleze.

Tusisubiri wageni waje watuboreshee elimu sababu wao wakija wanakuja kufanya kazi wapate wanachokitaka; ila sisi ndio tunajua tunachokikosa na tunachokitaka. Wageni hawatafanya kwa maslahi yetu bali kwa maslahi yao kwanza

Mungu ibariki Tanzania
Pia kuna gharama za muda
Maana kuandaa wa taalamu wakuja kuwarecruit wanafunzi ni action ya more than 10 years ili mfumo ukae vizuri .

Sasa sisi utaratibu wetu tunafanya kitu kuanzia 2019 ili kufikia August 2020 wapigakura wawe wanakumbuka,hapa namaanisha kuwa tupunguze siasa kwenye Mambo muhimu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom