Kwa wanachama na wapenzi wa CCM tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanachama na wapenzi wa CCM tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Topical, Jan 29, 2011.

 1. T

  Topical JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sera ya CCM kwa ujumla wake ni nzuri wananchi wengi wanaikubali, isipokuwa swala linalokera ni utendaji,utekelezaji mbovu wa sera.

  Vyama vingine havijaonyesha sera mbadala ila wanachosema ni kwamba ccm kwanini hawatekelezi vema sera zao? e.g. kwanini shule za kata haziboreshwi?, walimu waongezwa n.k kwa hiyo hawana mbadala ila tukitekeleza vizuri sera zetu ..watakuwa hawana hoja!

  Ombi langu kwa Mh. Pinda (waziri mkuu) mtekelezaji mkuu wa asera na kazi za serikali .....

  Nafikiri mkuu watendaji wakuu wa sera waanze kuangaliwa hasa kwenye mashirika yanayotoa huduma muhimu kwa wananchi waliotuchagua.., mfano mimi naona wafuatao wameshindwa kutekeleza sera za chama waondolewa na chama kupitia serikali ya chama tawala...

  1. Wiiliam Ngeleja - wizara imemshinda umeme haupatikani ahadi zimekuwa nyingi utekelezaji zero, ameshindwa kuweka mkakati dhabiti kuendesha wizara..miaka 5 tunaongelea issue moja na ameshindwa kuja na solution..nafikiri ana problem upstairs...

  2. William Mhando - Tanesco imemshinda hatuoni nafuu wala mkakati wa kitaalum wa kuboresha shirika huyu mtu ni dhaifu unprofesion

  3. David Mattaka - Ameshindwa kutekeleza sera za chama kuhusu usafirishaji, hatuoni mkakati wa kitaalum wa kuboresha shirika hilo huyu mtu amezeeka amepewa kijana mdogo under 40 anaweza kusaidia kuleta mapinduzi

  4. Justin Mwandu - Ameshindwa kuboresha shirika la NIC, jamaa huyu ni mwoga na very slow learner, NIC inaweza vipi kushindwa na Heritage insurance?

  5. William Erio - Wa PPF, soon wastaafu watamlaani huyu mtu, kila maazimio ya kuongezwa pension hayapeleki serikalini wala hafanyi juhudi za kusaidia wazee wastaafu..

  Kuna haja ya wapenzi na wanachama CCM kuwakamia serikali yetu iwaondoe hawa..na wengine wabovu..kwakuwa ni utekelezaji tu unaolalamikiwa wla si sera sera ziko OK.
   
 2. dazenp

  dazenp Senior Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Crap..................................:A S thumbs_down::laugh:
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jitahidi next time unaweza ukapatia. Nani mwenye uwezo wa kuwateua au kutengua uteuzi wa hao watekelezaji?
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Shinikizo la wanachama wa ccm kwa serikali yao inaweza kusaidia
   
 5. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Jitahidi kupima mafanikio ya tamko la kukurupuka la UVCCM ndipo ujifunze tatizo ni la nani? Kama Rais wakati wa matatizo yeye ndio kwanza analala usingizi basi hata mkurupuke kushinikiza jua liwake mvua inyeshe hakuna mtu atakayewajibika> Afteall hakuna mtu anayetegemea maajabu toka kwa serikali hii.Tunasubiri 2015 ifike tuwaweke bench, hamna maan nyie
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Sijui kwanini ume-address(umepeleka hili ombi) hili kwa Pinda waziri mkuu asiyejua kuwa ana meno na nguvu,yeye kila ktu yuko neutral,ungeanza kwa kumueleza mapungufu ya utendaji wake,umshauri kama yuko hapo kufurahisha waliomweka bora aondoke aje mtu mwenye guts za kupingana hata na Kikwete aliyewateua yeye mwenyewe Pinda,Mhando,Mataka na wengine????

  Otherwise,nafikiri umefikisha ujumbe kuhusu hao waliojisahau na kubweteka kwa kuwa walio juu yao hawaoni wala hawataki sikia kuhusu ubaya wao,wamewekana wale nchi hii pamoja........
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  another islamophobia
   
 8. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwenye hiyo list ongeza..
  Kikwete
  Makamba
  wote hao nao wameshindwa kutekeleza majukumu yao..
   
 9. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Islam on Action
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kweli na Makamba ni kansa pia ya kutowajibika na uwezo mdogo ...lakini JK hana shida.

  Makamba ataondoka muda si mrefu...wala hilo halina mjadala..
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kikatiba ndio mtekelezaji mkuu wa sera za serikali iliyoko madaraka, anaweza kumshauri rais kuwaondoa "watekelezaji wabovu" kwa taasisi mbalimbali ili kutekeleza sera za chama tawala...kwa faida ya wanachi na taifa.
   
 12. s

  seniorita JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  you cannot put a new wine in old an old wine skin....ccm is irreparable.....
   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  hakuna asiyejua kuwa kikatiba ndio mtekelezaji mkuu wa sera za serikali iliyoko madarakani,the point is,is he doing his job???ni maamuzi mangapi Pinda kafanya kuonyesha yeye ana uwezo wa kuongoza serikali,taja....,amshauri nini Rais kama yeye mtendaji mkuu aliyeteuliwa na Rais ni poor performer,ana uwezo huo,ana guts hizo???? In short yule ni pambo,anajaza nafasi.......wewe Kikwete ndo aliyewateua kina Mhando na Mataka leo Pinda mteuliwa wa Kikwete pia akamshauri awawajibishe wateuliwa wenzie wasiofanya vizuri kama yeye???
   
 14. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Pinda amechemsha mrudisheni Lowassa mnayejaribu kumsafisha, fullstop
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo umegeneralize, PM kuna mambo mengi amefanya lakini anahitaji wanachama wa ccm kuwa wakali kwa serikali kufanya zaidi...hasa kuangalia mashirika yasiyo perfom
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wako wengi si lazima lowassa, kuna Magufuli, kuna membe, kuna kina nundu etc..list ya watekelezaji wazuri kwenye chama siyo issue..ila issue ni kwamba hakuna culture ya kuwafukuza wasiotekleza sera kama niliowataja

  Ndio maana nasema wanachama wa ccm wawe wakali kwa viongozi wao wawaondoe hawa..
   
 17. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ulio wataja ni particle ndogo sana, tatizo ni chama kuwa cha kifamilia. Kwenye katiba ya ccm hakuna mahali palipoandikwa kuwa kiöngozi lazima afikishe miaka10 yaani kama walivyofanya kwa sitta. Sasa jk ilikuwa inatakiwa aöndolewe na chama kuweka mtu kompetent. Kubaki na jk mwenye visa na wanaomchukulia vimada ccm haiwezi badilika. Kama ameshindwa hata kukemea/kumfukuza rostam na wizi wote huo hamna kitu hapo. Kikubwa tusisubiri 2015 tuanze sasa tumtoe madarakani kama tunisia, egpty, yemen, albania na kwingineko
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  You will be surprised, 2015 ndio mwaka tutapata kura nyingi kupita uchaguzi wowote Tanzania

  Back to the topic hawa viongozi wameshindwa kutekeleza ilani ya chama tawala waondolewe
   
 19. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa, labda utueleze kwanza kwa nini umewataja hao wachache wengine wote ukawaacha. Pengine ili orodha yako isituchoshe kusoma na isijaze server ya JF, taja wale unaodhani ni watendaji waaminifu, mahiri, na siyo wala rushwa. Hebu jaribu mkuu.
   
 20. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Unajua Topical,hatuongelei Pm kwenda kufungua mkutano,kujibu maswali bungeni,kwenda dodoma kukiwa na mgomo na kutuliza......ni DECISION gani kubwa yenye long term impact aliyofanya???ukimfikiria Pinda kwa mengi utajaza kurasa,point yetu ni kipi kikubwa alichofanya...mfano kwenye issue ya wanafunzi wa elimu ya juu,lets say mikopo....miaka na miaka bodi ya mikopo inalalamikiwa...angekuwa makini angewawajibisha wahusika,kuvunja bodi ya mikopo na kuanzisha chombo kingine makini ambacho kitawasaidia walengwa kwa umakini zaidi,yeye huenda na kutoa ahadi,oh serikali imeliona na inalifanyia kazi,oh sijui nini.......
  Issue ya DOWANS,yeye ni kati ya waliosema hatuwezi kukwepa kulipa DOWANS,juzi kamati ya wanasheria sijui wa CCM imeshauri vingine na kusema inawezekana kupunguza deni au kutolipa kabisa,wewe unaona tuna waziri mkuu???kwanini hakutafuta ushauri kwanza kabla ya kukurupuka??He is useless......,period!
   
Loading...