Kwa wana "TUNDURU" wote mahali mlipo, twende tukaikomboe Tunduru yetu kabla haijatwaliwa.

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
Ndugu wana JF, natoa wito kwa wanatunduru wote mahali mlipo twende tunduru tukaiokoe Tunduru na kuirudishia heshima yake؛‎ Tazama matukio haya yatokeapo wenzetu wanapopatwa na masahibu;

Wasukuma: wakati wa ngoma, hata Cheyo na Chenge lazima waende kujihudhurisha.

WAHAYA: Wakati wa msimu wa senene hujihimu kwenda bukoba ama kutuma pesa kwa ndugu zao ili waweze kukisanya senene wa kutosha hata waweze kuwatumia ndugu zao walioko Ulaya.

WACHAGA: wakati wa krismass n pasaka hujihimu kwenda kilimakyaro kwa ajiri ya kukutana na kufanya shughuli zote za kifamilia na ukoo.

WAKURYA, WARWENCHOKA NA WENGINE: Wakisikia bhoke ameuawa na wavamizi au ng'ombe wa kyaro wameibiwa , wote huomba kibari kutoka kwa mkuu wa kikosi na kwenda kulinda heshima ya ukoo.

Hata kwa MSWATI: wakati wa ANNUAL REED DANCE, waswazi wote hujumuika all aroud the globe.

Sasa ndugu zangu wa Tunduru, twendeni tukalinde heshima yetu huko Tunduru. Kwa wote mtakaoliona angazo hili mjulishe na mwenzio.
 
Back
Top Bottom