Kwa wana CHADEMA tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wana CHADEMA tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masanilo, Jan 2, 2011.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nina lazimika kuweka bayana nia yangu ya kukomboa jimbo uchaguzi mkuu ujao. Nina amini raisi bora atatoka chama cha upinzani. Ni muda mrefu CCM wamekuwa madarakani lakini maendeleo ya nchi yazidi kushuka. Ufisadi usio na kina unazidi kushamiri, rushwa na kupotea kwa utaifa vinazidi kushika kasi. Mikakati yangu ni kuimarisha CHADEMA kwa ngazi ya Kaya kwa kaya. Jimbo langu lina kata 17, Sekondari za Kata 4, seminary secondary school 1, shule 2 za serikali za sekondari. Hizi shule nitazitembelea na kuwapa misaada ya hali na mali ikiwa ni pamoja kujitolea kufundisha ili nifahamike zaidi kwa wanafunzi ambao ndiyo wapiga kura 2015 hasa elimu ya uraia.

  Nitaanzisha mashina ya chama kwenye kata zote 17, nitawezesha wapatikane watendaji kwenye kila kata na kufungua ofisi pamoja na kununulia baiskeli viongozi wote 17. Nitatoa ujira walau kila mwezi wa Shs 10,000 kwa kila kiongozi. Ni hela ndogo ila uwezo wangu si mkubwa na mimi si fisadi. Kila mwaka kutakuwa na mashindano ya kugombea Ng'ombe na jezi kwa vijana football na Netball. Mashindano ya mbio riadha na baiskeli. Ninaandaa manifeso ya uchaguzi ujao nikilenga matatizo ya wananchi wangu na sulihisho zake, sitoweka hapa JF maana najua itanakiliwa na CCM na kurudifiwa.

  Ninampango wa kuwasiliana na Makao Makuu ili kadi na viongozi wa juu wa chama waanze kampeni mapema kuandaa wananchi wangu kulinda kura zitoshe 2015.

  Pipozi powa! Peoples Power ! Tanzania is for Changes

  Rev Masa K
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bado unafikiria tu? Mbona mwenzio nilishaanza na tuko jimbo moja!!!!! Hutujui wapiga kura wako???
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hongera mkuu basi tutaunganisha nguvu suala kubwa na kukamata jimbo
   
 4. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,200
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Big up! Jiridhishe sana kuhusu utaratib wa kutumia wanafunzi ktk siasa, isije ikawa nongwa badae. Umakini ni muhm sana. Naona hili jambo litaigwa na wengine. Zingatia sana taratib na sheria wasije wakapata pa kushikia na kudondosha mpango huu mzuri.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Rev. tumegee ni jimbo gani hilo..., ? yawezekana hata wakwe zetu wapo huko wasijekosa hiyo n`gombe
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hahahahah Ngoja kidogo nipe muda kuna mambo naweka sawa!
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Rev.. thanks for a post that ..... with clean hands best explain how should CDM look forward to strengthen its political motives all around the country so that it can regain strongholds of CCM in 2015 election to liberate poor Tanzanian citizens and bring hope to our beloved natives

  god bless you
   
 8. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,343
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Rev if this is for real japokuwa mie sio mwana CDM nakuunga mkono mpango mkakati wako.

  Kwa baraka na maombi ya wanaJF utafanikiwa maana hali ya ufisadi iliyopo inatisha na hakuna dalili kama kuna ukombozi utatokea CCM. Njia pekee ni kusababisha confusion kwenye kambi yao.
  Ukisha anza keimpliment mkakati wako tushtue wadau sidhani kama utakosa wa kukuunga mkono ununuzi wa baskeli.

  Pia hakikisha kuna uwiano wa jinsi utakavyotumia resources kidogo ulizonazo maana itabidi ujue kwa makadirio kwamba vijana wangapi kutoka hizi skuli watakuwa bado wapo jimboni kwako maana kuna wataokuwa wamendelea (five + six).

  Kuhusu michezo itabidi umpate mwana michezo mwenye ujuzi na eneo hili ili akusaidie kuratibu. Kwa mfano ili kupata timu bingwa ya kata wakashindania jezi na mipira then ubingwa wa kata ukaweka zawadi zenye kueleweka ila ng'ombe awepo ili watu wajichane.
  Jina la mashindano liwe linaloibua utaifa zaidi badala ya kutukuza jina la mtu sio Makongoro Mahanga Cup.

  Juu ya viongozi wa kata wawe hawakuogopa umande, pick form fours na six leavers walioko huko. Tengeneza mtandao wa walimu wa shule za msingi na sekondari walioko huko maana hawa ndio huwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye vituo.

  Nitarudi badae na idea zaidi!!

  Safari ya 2015 ianze sasa!
   
 9. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,186
  Likes Received: 2,747
  Trophy Points: 280
  Wa nyumbani tuko pamoja.......mda ukifika unikumbushe nikutumie mchango kidogo...ili kukuwezesha........we have to be the change we want...

  all the best,
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Be informed this is for real! Nakushukuru sana ushauri wako ni mzuri sana. Nadhani Maendeleo Cup itapendeza sana kuliko weka jina langu. Ushauri wako mzuri sana nimeuchukua kama ulivyo. Nimeambiwa niwe makini na nishiriki kwenye ku-update daftari la wapiga kura.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ngh'wana Makanza!

  Nakushukuru sana, Wasukuma wameamka sana kisiasa hawataki porojo! Ndo sababu nimeazimia kuboresha maeneo ya kule kwetu kwa kutumia malighafi watu na vitega uchumi vilivyo ndani ya uwezo. Tokea mwanzo sera zangu ni kuwapa mbinu waweze kuwa na maisha bora. Kofia na Tishirt baada ya miaka 5 hakuna tija. Nina utaalamu wa kufyatua na kuchoma tofari Thanks to National service 1991-2. Nitashirikisha wananchi tubadili nyumba zao kwa nguvu zao. Kama unawazo anuwai kuhusiana na maeneo ya kule kwetu basi wewe ni PM

  Masa K
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,052
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Ng'wana wa mayo!! Hii nayo ni takrima yani ufisadi.Kwanini uanzishe hayo kwa malengo ya kulinda zitoshe? kwi kwi kwi. Heri ya mwaka mpya.Mimi nitakuwa mpinzani wako sera yangu ni kugawa matobolwa bure, yani haki kwa wote.
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hahahahahaha haya bwana! Ila kumbuka wapinzani sisi si maadui tupo kuhakikisha serikali iliyo madarakani inawajibika kwa wananchi. Hahahaha watapokea matobolwa yako ila wakati wa kupiga kura watatumia busara zaidi.

  Eeeh bwana niko pouwa challenges za maisha zinazidi kuwa nyingi

  Heri ya mwaka mpya
   
 14. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,217
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  nami niko hivyo na Babu yangu alikuwa CCM miaka ya 1980 kama Mwenyekiti wa Wilaya lakini kwa kuwa hakuwaelewa aliama mwaka 1993 kwenda NNCR wakati huo sasa ameshakata roho, Mungu hamreemu maana ke mpaka sasa angekuwa CDM nami ninafuata nyayo zake kuakisha Nchi hii inakombolewa Upya kutoka mikononi mwa Genge la Vibaka wanaobaka vijisenti vya walapwiiiiiiiii
   
 15. DALA

  DALA JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 817
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 80
  Maneno na mawazo ya busara katika jitihada za ukombozi!

  Nafikiri umeweza kutambua changamoto ambazo zinatukabili kama wanachama wa CDM, nilishiriki kwenye uchaguzi mkuu katika nafasi mbali mbali ikiwemo kama mwanafunzi wa siasa.

  Kitu ambacho nilijifunza ni kwamba chama chetu kinahitaji mtaji mkubwa sana ya wananch "IMANI YA WANANCHI). Tunatakiwa kuhakikisha kwamba mfumo mzima wa uongozi katika ngazi za mikoa, wilaya, kata, mitaa na mashinani si jambo la kulifumbia macho kabisa!

  Viongozi walioko mashinani wengi wao hawajaelewa CDM inasimamia nini na mfumo wa ushirikiano kati ya makao makuu na ofisi za chini bado ni dhaifu sana! Katika kuimarisha chama ninapendekeza vijana tuklioko tayari kuifanya hii kazi tupewe jukumu hili na walioko vijijini waingizwe kwenye mkondo ili tufanikishe malengo yetu!

  Ninadhamira ya kweli kushiriki katika mageuzi haya!
   
 16. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,343
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Now you are talking Rev!
  Malengo yangu for 2015 nisaidie kupatikana wabunge wapya japo wawili be it from CDM, NCCR etc ila sio CCM.
  You have my backing, we dont have much resources at our disposal but we have the will and courage.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tuungane pamoja kila mtu kwa nafasi yake! Imani ya wananchi ni bora kuliko mamilioni ya CCM na wananchi kuwa maskini daima
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,394
  Likes Received: 1,550
  Trophy Points: 280
  una dhamira ya kweli kuwatumikia wananchi au unakwenda kuandaa mazingira ya kukiboresha kitambi?
   
 19. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,838
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  fanya hivo rev kuwapiga bao hawa mapimbi wa kijani mana wamegeuza siasa mtaji.
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwa kazi niliyonayo nadhani naweza boresha kitambi vile vile. Nafsi yangu inanituma nifanye ninalofikiria sasa. Habari za kusema Kilimo kwanza halafu wakati huo huo unahimiza kujenga machinga complex kila mkoa ina nisikitisha. Nisome kwa makini utanielewa
   
Loading...