Kwa waliosoma urusi miaka ya 83 hadi 89

paurlus

New Member
Nov 22, 2012
2
3
mambo vipi wana JF, kwema? Jina langu naitwa paulus baragi, natafuta marafiki ambao walisoma na mzee wangu aitwaye Nyakuwa Nyakitita Baragi nchini Urusi miaka ya 83 hadi 89 , alikua anasoma Mji wa Baku,azerbaijan ambayo kwa sasa imejitenga na urusi, nahitaj kukutana na rafiki yake ama mtu yeyote aliesoma nae mji moja huo wa Baku,azerbaijan kwa miaka iyo ya 83 hadi 89, alikua akisoma Azezbekova . Shukrani sana.
 
Du sema unatafuta baba zako wadogo/wakubwa na sio marafiki!! Samahani lkn kwani baba hayupo?
 
Kwanza karibu JF halafu pole,njia rahisi ni kujua baba yako alisomea fani gani katika hiyo miaka chuo gani , kiko mji gani ,mwaka gani ali graduate halafu muingize katika graduates .com utawapata tu baba zako wadogo na mashangazi pia mama wa kambo ! si 100%inategeme kama jamaa wamejiunga ama la but worth a try.
 
Du sijui kama wapo hao waliosoma urusi enzi hizo,sababu ni kuchanganyikiwa na maisha na wengi wao wakaishia kunywa nyagi,wake zao wa kidhungu(wengi wao walikuja nao)waliwakimbia baada ya kuona mambo si mambo,sijui kama kweli utawapata walio hai kwa sasa
 
Kuna thread inamzungumzia mzee huyo hapa.........ngoja nimwite Pasco
 
Last edited by a moderator:
Du sema unatafuta baba zako wadogo/wakubwa na sio marafiki!! Samahani lkn kwani baba hayupo?

Taratibu mkuu huyu mtu anawatafuta marafiki wa baba yake ambaye ana matatizo ya akili kwa sasa (Nyakuwa Nyakitita) ambaye alikuwa mhadhiri DIT na alishajadiliwa hapa muda si mrefu halafu wewe unamfanyia dharau? jaribu kuwa mstaarabu japo kidogo.
 
Pole sana jamani. Wenye wazazi waliosoma urusi miaka hiyo hebu waulizeni. pengine kuna jambo huyu kijana anataka afahamu kuhusu marahdi ya huyu baba yake. tuwe serious kwa issue serious kama hizi.
 
Pole sana. Unadhani hao marafiki wa zamani wanaweza kumsaidia kwa lolote? Kama kuferesh mind yake ama?
Nisikudisappoint, lakini narafiki hao wa zamani ukiwaona kwa sasa wanaweza wasipende kuwa involved. Usije ukavunjika moyo lakini, ila usiweke mategemeo juu saa.
 
mambo vipi wana JF, kwema? Jina langu naitwa paulus baragi, natafuta marafiki ambao walisoma na mzee wangu aitwaye Nyakuwa Nyakitita Baragi nchini Urusi miaka ya 83 hadi 89 , alikua anasoma Mji wa Baku,azerbaijan ambayo kwa sasa imejitenga na urusi, nahitaj kukutana na rafiki yake ama mtu yeyote aliesoma nae mji moja huo wa Baku,azerbaijan kwa miaka iyo ya 83 hadi 89, alikua akisoma Azezbekova . Shukrani sana.
Paurlus, pole sana!. nimeguswa!.
 
Yupo ,lakini ni mgonjwa {mental disorder}

Aiseee Ok nimekumbuka kuna thread ilikuwa inamzungumzia kumbe ni mzee wako huyo pole sana,kwani mama yupo urusi? Masha yupo wapi? Kwakua nyie ni ma half-cast mtatoka tu kimaisha,maana bongo mademu na wavulana halfcasts wanabahati ya kupendwa na wenye fedha zao!! Nenda DIT kama ulivyoelekezwa,pia mzee lzm atakuwa alichangia nssf/ppf lazima atakuwa na hela na pia kuna fao la matibabu nssf wanatoa ebu anzia hapo kwanza!
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom