kwa waliosoma Darajani (Gilman Rutihinda) Shule ya msingi pale Kigogo

Lucas

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,457
1,108
Jamani, leo nimeamua kuikumbuka shule yangu ya Msingi niliyoipenda sana... Gilman Rutihinda ama kwa waliosoma miaka ya nyuma kidogo iliiitwa Darajani... naomba tukumbushane enzi hizo,. kipindi hicho hakuna international school... tulikuwa tunakimbiza!!! walimu kina KImangano(huyu nasikia alikuja hamia kumbukumbu) Sadalla, na wengine wengi tu. kama upo hapa jamvini karibu.

nakaribisha pia na wale waliopenda ushindani na shule yetu kama Msimbazi mseto, Chang'ombe na hata Kumbukumbu wenyewe karibuni sana
 
Mlikuwa mnakimbiza kipindi hicho, sasa hivi unakimbiza au kimbizwa? Ndo cha maana kwa sasa.

tulikimiza sana, hata sasa bado vijana wetu wamo... japo sina data kamili.... nakumbuka kuna miaka ya hivi karibuni darasa la saba kwa mkoa DSM ilikuwa shule pekee ya st kayumba iliyoingia top ten ikiwa ya sita.... so bado wamo... though enzi hizo tungekuwa wa kwanza au wa pili
 
Akina mwalimu Sipendi, Kinunda, Assey, Kallanje, Mwamanga, James wa darasa la kwanza, Mwl Gadi mtaalam wa kupiga na rula, Kimangano alihamia Kumbukumbu ila aliendelea kuwa friend wa shule yetu, Sadala nasikia alikuja kuwa mwl mkuu pale... dah. Nilisoma pale mkuu
 
Viboko vya Sadalla vilinifanya niwe na akili aisee! Nakumbuka kila Jumamosi tulikuwa tunaenda kushindanishwa na shule nyingine kwa mitihani, sasa ole wenu mtu wa kwanza asitoke Rutihinda, halafu maksi zako zikipungua kulinganisha na mtihani uliopita unachapwa viboko idadi ya alama zilizopungua! Sasa tuliokuwa tunapata 40 kwenda juu tulikuwa hatuna amani wakati wote,
 
Dah, umenikumbesha mbali... hao wa la kwanza... sikuwakumbuka kwa sana nilihamia madarasa ya juu kidogo, bakora za sadallah ulitumia?
 
Viboko vya Sadalla vilinifanya niwe na akili aisee! Nakumbuka kila Jumamosi tulikuwa tunaenda kushindanishwa na shule nyingine kwa mitihani, sasa ole wenu mtu wa kwanza asitoke Rutihinda, halafu maksi zako zikipungua kulinganisha na mtihani uliopita unachapwa viboko idadi ya alama zilizopungua! Sasa tuliokuwa tunapata 40 kwenda juu tulikuwa hatuna amani wakati wote,

ah ha ha ha uwe hujafikisha marks 120 katika masomo matatu???!! bakora utaenjoy!! i remember kutumwa fimbo za kuwachapia wenyewe.....
 
Mi wakishua bana, nilisomaga aghakhan.

kwa taarifa yako, enzi zetu Rutihinda ndio ilikuwa ya kishua... kwanza ada yake ilikuwa tofauti na wengine,
wengine wakilipa ada shs 20 au 220, sie tulilipa shs 3000, halafu watoto wa vigogo walikuwa wengi sana hapo, kuna baadhi walitoka mbezi, oysterbay, kinondoni, Mbagala, chang'ombe.... i mean kona karibu zote za jiiji... nakumbuka kuna mtu alikuwa anatoka kipunguni anakuja Rutihinda akitafuta elimu bors
 
Gilmana mlikuwa wakwanza kimkoa miaka fulani hadi sie wa lasaba huku mikoani tulikuwa tukijua uwepo wenu!
 
Ni kweli mkuu, nakumbuka kuna kipindi mwanafunzi mwenzetu aligongwa na gari maeneo ya Kurasini akiwa anakuja shuleni asubuhi, kwa bahati mbaya akafariki. Sasa nilipokuja kuifahamu Kurasini nikabaki kujiuliza ni kwa nini watu walikuwa wanatoka mbali kiasi kile kuifuata shule Kigogo ilhali maeneo yao shule zilikuwepo? Asilimia kubwa ya wanafunzi pale walikuwa siyo wakazi wa Kigogo na funny enough ni kwamba watoto wengi wa Kigogo walikuwa wanasoma aidha Msimbazi Mseto ama Mzimuni, nilikuja kuambiwa kuwa kupata admission Gilman Rutihinda ilikuwa ishu kubwa..

Gilman mlikuwa wakwanza kimkoa miaka fulani hadi sie wa lasaba huku mikoani tulikuwa tukijua uwepo wenu!

Ile shule kwa jinsi bakora zilikuwa zinatembezwa ni lazima ufaulu tu mkuu, mbaya zaidi wazazi walikuwa wanaunga mkono zile fimbo eti ili watoto wao wafaulu, hivyo kimbilio pekee ilikuwa ni kupata alama za juu ili usilambwe mboko, lol..!
 
Gilmana mlikuwa wakwanza kimkoa miaka fulani hadi sie wa lasaba huku mikoani tulikuwa tukijua uwepo wenu!

Nakumbuka, sisi mwaka wetu pamoja na kupiga mtihani wa mock Dsm lakini tulienda pia kupiga na mock ya morogoro pia...
 
Ni kweli mkuu, nakumbuka kuna kipindi mwanafunzi mwenzetu aligongwa na gari maeneo ya Kurasini akiwa anakuja shuleni asubuhi, kwa bahati mbaya akafariki. Sasa nilipokuja kuifahamu Kurasini nikabaki kujiuliza ni kwa nini watu walikuwa wanatoka mbali kiasi kile kuifuata shule Kigogo ilhali maeneo yao shule zilikuwepo? Asilimia kubwa ya wanafunzi pale walikuwa siyo wakazi wa Kigogo na funny enough ni kwamba watoto wengi wa Kigogo walikuwa wanasoma aidha Msimbazi Mseto ama Mzimuni, nilikuja kuambiwa kuwa kupata admission Gilman Rutihinda ilikuwa ishu kubwa..

Ile shule kwa jinsi bakora zilikuwa zinatembezwa ni lazima ufaulu tu mkuu, mbaya zaidi wazazi walikuwa wanaunga mkono zile fimbo eti ili watoto wao wafaulu, hivyo kimbilio pekee ilikuwa ni kupata alama za juu ili usilambwe mboko, lol..!

mie nawafahamu watu ambao waliingia darasa la saba wakiwa vilza wa hesabu lakini kwa adhabu za pale uwanja wa damu.... weee walikuja kuwa safi sana!!
 
Dah,aisee umenikumbusha mbali kweli,mi nlikuwa nasoma Kawawa p/r 2likuja kufanya mtihan wakt 2ko la 6,kpnd kile 2likuwa 2naona watoto wa pale mnaringa,na 2likuwa 2nawaogopa vbaya.
 
kati ya vut nilipienda tukiwa Rutihinda ni kujengewa confidence ya kuwa UNAWEZA.... kila aliyepita rutihnda anajua hilo
 
poleni wana rutihnda kwa mliofikwa na mafuriko
 
Viboko vya Sadalla vilinifanya niwe na akili aisee! Nakumbuka kila Jumamosi tulikuwa tunaenda kushindanishwa na shule nyingine kwa mitihani, sasa ole wenu mtu wa kwanza asitoke Rutihinda, halafu maksi zako zikipungua kulinganisha na mtihani uliopita unachapwa viboko idadi ya alama zilizopungua! Sasa tuliokuwa tunapata 40 kwenda juu tulikuwa hatuna amani wakati wote,

dah! Jombaa umesoma pale? Poleni kwa viboko aisee.
 
ni kweli.., mm nlisoma mseto na mitihani ya jmosi ya ujirani mwema mlikua mnatupelekesha kwa kweli..,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom