Kwa waliooa tu

Youngstunna

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
258
294
Habarini wakuu?

Leo na swali dogo ningependa kila mtu ajibu kwa ubnafsi wake yeye kama yeye

Je, ni sahihi kuoga na mke wako bafu moja nyumba za kupanga? Yaani bafu Public kwa walio panga nyumba fulani?

Maana mara kadhaa nimempinga wife na kuzozana nae juu ya yeye kupenda hii tabia, Kwa upande wangu sizani kama hii ni adabu.
 
Tatizo halipo upande wa adabu ila tu kuvumilia macho ya watu na masengenyo yatakayoanza, ila kwa kuwa hatuishi kwa kufuata maneno ya watu...ni vema ukamridhisha wife maana kwa wanawake vitu vidogo kama hivyo kwao huwa ni vikubwa.
 
Sijakuelewa, umempiga mkeo sababu ya yeye kutaka/kupenda kuoga na wewe?
 
Tatizo halipo upande wa adabu ila tu kuvumilia macho ya watu na masengenyo yatakayoanza, ila kwa kuwa hatuishi kwa kufuata maneno ya watu...ni vema ukamridhisha wife maana kwa wanawake vitu vidogo kama hivyo kwao huwa ni vikubwa.

Inategemea zaidi na muda, huwezi kuingia na mkeo bafuni muda ambao watoto wanacheza na watu wamekaa hapo uani!

Nilikuwa naoga na wife asubuhi tuwahi kazini na kuokoa muda wa kujipanga! Kikubwa msilete mbwembwe mkachelewesha wengine, ogeni fasta tokeni. Majirani watawapenda na kuiga!

Usiku, muda ambao mnataka kwenda kulala ndiyo mzuri na watoto na wapambe washalala ndiyo mnakwenda kupiga mbizi.

Kuna neno hapo?
 
Sawa sawa mkuu nimekupata kwa ufasaha.
 
Mie mke wangu tunaoga tu.
Majirani watajuaje sasa kuwa tuna mahaba mazito?
 
Ni jambo la kawaida sana ila muhimu kuangalia mazingira msiwabugudhi wengine.
Kama mazingira mabovu jimwageni night kali
 
Mtachukua mda mrefu bafuni, sio vizuri ila nyumba yenu poa, kila sehemu ya mwili inasuguliwa kwa ufasaha
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom