KWA WALIOOA TU (KITCHEN PARTY KWA WANAUME):Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KWA WALIOOA TU (KITCHEN PARTY KWA WANAUME):Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Baba Mtu, Oct 15, 2010.

 1. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Siku chache zilizopita tuliona ni jinsi gani mke anatakiwa fanye ili amfurahishe mumewe. Wadau wengi wakashauri pia itolewe kitchen party kwa ajili ya wanaume tu, alimaarufu kama SEBULE PARTY.

  Ifuatayo hapa chini ni sebule party, kazi kwako mdau mkuu, mzee mwanakijiji, urasa, invible, mpayukaji, mfukunyuzi, babalao na wengine wengi

  1. Mapokezi Mazuri
  Baada ya kurudi kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisheni:

  -Anza kwa maamkizi mazuri
  -Anza kwa Assalaamu 'Alaykum na tabasamu.
  -Salaam ni Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.
  -Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka baadae.

  2. Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha

  -Chagua maneno mema na jiepushe na maneno mabaya.
  -Shughulika nae unaposema au anaposema yeye
  -Sema kwa ufasaha na rejea maneno inapohitajika mpaka afahamu/aelewe.
  -Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda, mfano Mpenzi wangu, honey (asali, tamtam), (habibty), swaaliha (mwanamke mwema), n.k


  3. Urafiki na maliwazo

  -Tumia muda kuzungumza nae
  -Mfikishie habari njema
  -Kumbuka kumbukumbu zenu nzuri za kuwa pamoja.

  4. Michezo na burudani

  -Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya furaha
  -Chezeni na mshindane katika michezo na mambo mengine.
  -Mchukue kuangalia aina za burudani zilizo halali.
  -Jiepushe na mambo ya haram katika kuchagua aina ya burdani.

  5. Msaada katika kazi za nyumbani

  -Fanya kile ambayo wewe mwenyewe unaweza/ unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa anapokuwa mgonjwa au amechoka.
  -La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha wazi kuwa unathamini/unashukuru jitihada zake katika kazi.

  6. Kushauriana (Shuura)

  -Hususan katika masuala ya familia
  -Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu kwako.
  -Kuyazingatia maoni yake kwa makini
  -Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa maoni yake iwapo yatakuwa ni bora zaidi.
  -Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.

  7. Kutembelea wengine

  -Chagua watu wenye malezi mema wa kufanya mahusiano nao. Kuna malipo makubwa katika kuwatembelea jamaa na watu wacha Mungu. (Sio kuwatembelea kwa kupoteza wakati)
  -Kuwa muangalifu kuhakikisha tabia za Kiislamu wakati mnapowatembelea watu.
  -Usimlazimishe kuwatembelea wale ambao yeye hajisikii raha kuwa nao.

  8. Muongozo wakati wa kusafiri

  -Muage vizuri na kumpa ushauri mwema
  -Mtake akuombee dua
  -Watake jamaa wacha Mungu na marafiki kuiangalia familia wakati wa kutokuwepo kwako.
  -Mpe pesa za kutosha kwa mahitaji anayoweza kuhitajia
  -Jaribu kuwa na mawasiliano nae ama kwa simu, e-mail (barua pepe), barua, n.k.
  -Rejea haraka iwezekanavyo.
  -Mchukulie zawadi
  -Jiepushe na kurejea nyakati zisizotarajiwa au nyakati za usiku.
  -Mchukue (safarini) ikiwezekana.

  9. Msaada wa Kifedha

  -Unatakiwa kuwa mtumizi kwa mujibu wa uwezo wake wa kifedha.
  -Usiwe bahili na pesa zake (wala usiwe mfujaji).
  -Unapata malipo kwa matumizi yote unayotumia kwa ajili ya kumkirimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha mkate ambacho unamlisha kwa mkono wako (hadiyth).
  -Unahimizwa sana kumpa kabla yeye hajakuomba.

  10. Kunukia vizuri na Kujipamba mwili

  -Kufuata Sunnah ya kunyoa nywele za utupuni na kwapani.
  -Daima uwe msafi na nadhifu.
  -Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)

  11. Jimai (Tendo la ndoa)

  -Unawajibika kulifanya mara kwa mara iwapo huna dharura (ugonjwa,n.k)
  -Uanze kwa “Bismillah” na dua zilizo sahihi.
  -Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi tu (sio sehemu ya nyuma)
  -Uanze kwa vitangulizi (vya jimai) ikiwa ni pamoja na maneno ya mapenzi.
  -Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.
  -Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza
  -Epukana na jimai wakati wa damu ya mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni haram
  -Fanya chochote unachoweza kuepuka kuharibu kiwango chake cha haya alicho nacho (haya na staha) mfano kuvua nguo pamoja badili ya kumtaka avue yeye mwanzo huku ukiwa unamuangalia.
  -Epuka wakati wa jimai mkao ambao unaweza kumuumiza mfano kumgandamiza katika kifua inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe ni mzito.
  -Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.

  12. Kudhibiti Siri

  Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa siri za chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine ya kibinafsi.


  13. Kumuongoza katika Kumtii Allaah (سبحانه وتعالى)

  -Muamshe katika sehemu ya tatu ya mwisho ya usiku kusali “Qiyaam-ul-Layl” (sala za ziada za usiku zenye sujuud na ruku’u za muda mrefu).
  -Mfundishe kile unachokijua katika Qur’an na tafsiri zake.
  -Mfundishe “Dhikr” (njia za kumtaja Allaah kama alivyofundisha Mtume) za asubuhi na jioni.
  -Muhimize kutumia pesa kwa ajili ya Allah (S.W.T.) kama vile kutoa sadaka.
  -Mchukue katika safari ya Hijja na Umrah wakati unapokuwa na uwezo.

  14. Kuonyesha Heshima kwa familia yake na arafiki zake
  -Mchukue katika matembezi kwa familia na jamaa, hususan wazazi wake.
  -Waalike kumtembelea na wakaribishe.
  -Wapatie zawadi kunapokuwa na jambo maalum (kama sikukuu)
  -Wasaidie wanapokuwa na haja kwa msaada wa fedha, nguvu, n.k.
  -Endeleza uhusiano mzuri na familia yake baada ya kifo chake iwapo atakufa mwanzo. Pia kwa hali kama hii mume anahimizwa kufuata Sunnah na kutoa kile ambacho yeye (mke) alizoea kutoa wakati wa uhai wake kuwapa rafiki ya jamaa zake.

  14. Mafunzo ya Kiislam na Kumshauri kwa kumrekebisha

  Hii ni pamoja na:
  -Misingi ya Uislam
  -Haki na wajibu wake
  -Kusoma na kuandika
  -Kumhimiza kuhudhuria darsa na halaqah (darsa duara za msikitini na majumbani).
  -Hukumu za Kiislam zinazowahusu wanawake
  -Kumnunulia vitabu vya Kiislam na kaseti kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.

  16. Wivu unaokubalika

  - Hakikisha kuwa anavaa hijaab kamili anapotoka nyumbani.
  -Usimruhusu kuchanganyika ovyo na wanaume wasio- mahram.
  -Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano wake ni kama:

  1. Kulichambua kila neno na sentensi asemayo na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo hakuzikusudia.
  2. Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.
  3. Kumzuilia kujibu simu, n.k.

  17. Subira na Upole

  -Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.
  -Hasira lazima zionyeshwe pale anapochupa mipaka ya Allaah (S.W.T.), kwa kuchelewesha Sala, kusengenya, kuangalia yasiyofaa katika TV, n.k.
  -Kumsamehe makosa anayokukosea wewe (Angalia sehemu ya 18).
  -Ni namna gani unaweza kumrekebisha makosa yake?

  1- Kwanza, mpe ushauri kwa njia ya mzunguko na ya moja kwa moja mara kwa mara

  2- Kisha kwa kumpa mgongo katika kitanda kumuonyesha hisia zako). Tanabahi kuwa hii haihusishi kuhamia chumba kingine, kuhamia nyumba nyingine, au kutomsemesha

  3-Utatuzi wa mwisho ni kumpiga kidogo (kwa namna ilivyoruhusiwa) Katika hali hii, mume ni lazima aangalie yafuatayo
  - Ni lazima ujue kuwa Sunnah ni kuepukakumpiga kwani Mtume (S.A.W.) hakuwahikumpiga mwanamke wala mtumwa
  -Ni lazima ufanye hivyo katika hali ya juu kabisa ya kutotii, mfano mara kwa mara kukataa tendo la jimai bila ya sababu, mara kwa mara kutosali kwa wakati wake, kuondoka nyumbani kwa muda mrefu bila ya ruhusa na kukataa kusema pahala alipokuwepo, n.k
  -Usifanye hivyo mpaka awe umeshampa mgomo na kulijadili hilo suala pamoja nae kama ilivyoelezwa katika Qur’an
  -Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza au kumpiga usoni au katika sehemu zilizo nyepesi kuathirika katika mwili wake.
  -Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa kiatu, n.k.

  18. Kusamehe na makaripio yanayofaa

  - Mhukumu kwa makosa makubwa tu
  -Msamehe makosa aliyokukosea wewe bali mhukumu kwa makosa ya haki za Allaah, mfano kuchelewesha Sala, n.k
  -Kumbuka mazuri yote anayomfanyia kila wakati anapofanya makosa
  -Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na umuwazie dharura mfano huenda amechoka, ana huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake katika Uislam bado yamo katika kukua
  -Jiepushe na kumgombeza kwa mapishi mabaya kwani Mtume (S.A.W.) hakuwahi kumlaumu yeyote katika wake zake kwa jambo hili. Iwapo amekipenda chakula, hula na iwapo hakukupenda hukiwacha na hatoi maoni yoyote.
  -Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu wazi wazi
  -Epukana na kutumia jeuri au maneno yanayoumiza hisia zake
  -Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo subiri mpaka mnapokuwa faragha
  -Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii inasaidia kuweza kudhibiti maneno yako  Kwenu nyamayo, lady n, first lady, queenkami, caren, fixed point, lily,maria rosa, rose 1980, remmy na wengineo, mkiona wanaume hawawafanyii haya mjiulize mara mbili mbili, isije kuwa mmeo ana illegal small house.

  MUHIMU: KUDAI HAKI NI VIZURI KUKAENDA SAWA NA KUTIMIZA WAJIBU. HAIPENDEZI IWAPO UNADAI HAKI ZAKO WAKATI WEE WAJIBU WAKO HUTIMIZI.

  Soma zaidi kutoka hapa Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo | Alhidaaya.com
   
 2. babalao

  babalao Forum Spammer

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante kwa Bag Party yako baba naomba niongezee kidogo. Sehemu nyeti katika mahusiano ni namna ya kumtosheleza mwenzio (Angalizo Dont try this outside your wife utapata shida) Watu wengi sana wanashindwa kuwatosheleza wake zao huwaingilia wakati hawajawa tayali hawajalainika sehemu za siri. Kwa kuwaingilia bila kufanya maandalizi (foreplay). Ukifika nyumbani kila mara, jitahidi uwe na uso wenye furaha umwandae mwenzio kisaikolojia usimuudhi. Mkifika ndani, muulize kama tendo la ndoa linaweza kufanyika siku hiyo? Usilazimishe, mwandae mwenzio kwa kumsemesha lugha ya mahaba na kumshika shika sehemu ambazo zitamsisimua kama vie, matiti, chuchu, shingoni, kiunoni nk. Unaweza kumuuliza jee ni sehemu gani ukimshika anasisimka zaidi. Akiwa tayali unaweza kumwingilia usiingie kwa haraka ndani ingia polepole na uchezee jujuu, kwa kufanya hivyo utajikuta unachelewa kufika kileleni na mnaweza kufika kwenye kilele wote pamoja. Kwa kawaida mwanaume huwa anaweza kufika kileleni haraka zaidi kuliko mwanamke hasa akiingia ndani. Kama ukiwahi kufika kilele kabla ya mwenzio, jitahidi umsaidie naye amalize afike kileleni, usimwache kwenye mataa kitu hiki huwa kinawaudhi sana wanawake. Mambo haya na mengine zaidi unaweza kuyapata kwenye kitabu kinachoitawa Tendo la ndoa, mimi niliwahi kukinunua toka kwenye duka la Kase store huko Arusha.
   
 3. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kwa huku dar kitabu hicho naweza kukipata duka gani?? Uliza hapo uliponunua hicho chako kama wana wakala wao huku dar
   
 4. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huu ni upande mmoja vipi kwa wakristo
   
 5. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  mwanamke gani bongo ana muda wa kukusubiri wewe ufanye yote hayo?
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Huu mbona ni kama inabidi uwe mnafiki hivi? Utaweza kwa maisha yako yote?
   
 7. babalao

  babalao Forum Spammer

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna unafiki ndiyo mapenzi yenyewe.
   
 8. S

  Saiguran Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Angalizo Dont try this outside your wife utapata shida"???!
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Orait Orait
   
 10. babalao

  babalao Forum Spammer

  #10
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Baba mtu Jaribu kwenye maduka ya vitabu vya dini kina rangi ya kijani mtunzi nimesahau jina lake
   
 11. babalao

  babalao Forum Spammer

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Saiguran Umeipenda dont try this outside your wife? Ukitumia mbinu hizi kwa small house utapata shida atakuganda kama luba hii inatumika nyumbani tu ili kuimarisha ndoa
   
 12. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapo Dar mimi niliwahi kumnunulia kaka yangu kama zawadi kwenye arusi yake. Nilikinunua Kwenye round about ya shule ya uhuru mchanganyiko. Kuna kanisa moja la Assemblies of God wanauza vitabu kwa nje. Unaweza pia kwenda kwenye bookstores za vitabu vya kikristo na utakipata. Kimeandikwa na professor mmoja wa masuala hayo!!! Tendo la Ndoa ni kitabu kizuri sana... kinafundisha mambo mengi.:A S thumbs_up:
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  al madrasa
   
 14. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Asante magafu, siku nikipita maeneo ya kariakoo ntakifuta.
  Tehe tehe tehe tehe tehe tehe tehe, UNAFANANA KABISA NA MTOTO. Ntamuuliza mama mtu anieleze vizuri, isije alikuzaeni mapacha, na mwengine ndio wee (NI UTANI TU)
   
 15. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,002
  Trophy Points: 280
  :biggrin1::biggrin1: duh mkuu hicho kitabu nadhani kimepata promo ya kutosha hapa
   
 16. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Usiwe kama wabunge wa serikali ya CCM (JAPOKUWA NTAICHAGUA CCM OKTOBA 31), hoja ikitolewa/wazo likitolewa na kambi ya upinzani wataipinga eti kisa imetoka upande wa upinzani. Chukua kinachokufaa katika maisha yako na kisichokufaa kiache hapo.

  Hujawahi kuona gari imeandikwa CHIZI KATOA WAZO???!!!!
   
Loading...