Kwa waliofeli kabisa Darasa la Saba, Kidato cha 4 au 6, pitia hapa

chikuyu

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
277
179
JE, NI MTU MWENYE ELIMU GANI ANAWEZA KUSOMA ACCA?
ACCA ina ngazi kuu mbili:
1: Foundations in Accountancy (FIA)
2: ACCA Qualifications

HAPA NITAONGELEA TU FOUNDATIONS IN ACCOUNTANCY PEKE YAKE

Foundations in Accountancy (FIA)
Ngazi hii haina vigezo vyovyote vya Elimu ili mtu aanze kusoma. Hii ni kwa ajili ya mtu ambaye hana ujuzi wowote wa uhasibu au hana Elimu yoyote rasmi, ila anataka kuwa Muhasibu.. Hivyo, hapa ni sawa na mtu anayetaka kuanza Darasa la Kwanza la Uhasibu.

Unaanza na utangulizi kabisa wa Uhasibu.. Kujiunga ni MTU yeyote Yule ili mradi tu aweza Kujua Kiingereza akaelewa maana ya maneno yalioandikwa na Kufanya baadhi ya maswali ya Hesabu.

ACCA wana Online Platform ya bure kabisa kwa mtu anayehisi Kiingereza chake na Hesabu havipandi.. Anaweza kujifunza hapo kwa bidii huku akiendelea na shule yake ya FIA.

Hii ina maana gani?
Hii ina maana kwamba hata kama mtu kaishia Darasa la saba, ila akataka kujiendeleza Kielimu katika fani ya Uhasibu, anapata mahali pa kuanzia na kuendelea mpaka kufikia PhD akiamua.

Kwa hiyo kama wewe umeishia Darasa la saba, umefeli Kidato cha pili, umefeli Kidato cha nne, umefeli Kidato cha sita, etc. usikate tamaa ukahisi ndo mwisho wa elimu yako. Bado kuna njia ya kukufanya uendelee na shule yako na hatimaye ukawa Mhasibu anayetambulika Kimataifa (Ulimwenguni Kote).

Ili Kusajiriwa na Bodi hii kwa ngazi hii ya Awali ya Uhasibu (FIA), Mtahiniwa angalau anahitajika awe na Identity Card yoyote kama vile Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Taifa, Hati/Pasipoti ya Kusafiria, n.k

Kutegemeana na elimu yako hiyo, utapata mahali sahihi pa kuanzia kusoma Kozi hizi za Kimataifa na Kupata Vyeti tofauti tofauti na katika madaraja tofauti tofauti ambavyo vitakupelekea mpaka kupata ACCA Qualifications.

Pia kuna ushirikiano ambao Bodi ya ACCA wanao na Vyuo Vikuu vya Kimataifa vyenye sifa duniani kama vile Oxford Brookes University ambao wanatoa BSc (Hons) Degree in Applied Accounting kwa wanafunzi wanaosoma ACCA waliomaliza mitihani kadhaa na kufanya Research and Analysis Project kwa muda wa miezi sita.

Pia ACCA wana ushirikiano na Chuo Kikuu maarufu Duniani cha University of London ambacho ni kati ya Vyuo 10 bora nchini Uingereza. Chuo hiki kinatoa MSc in Professional Accountancy kwa wanafunzi wanaosoma au waliomaliza mitihani ya ACCA ambapo wanatakiwa kufanya idadi kadhaa ya Mitihani na Kufanya Research Project ya Chuo hicho na Kupata Masters Degree yako kutoka Chuo hiki cha Kimataifa.

JE, MITIHANI GANI UNAFANYA YA FOUNDATIONS IN ACCOUNTANCY?

Kwanza kabisa Level hii ya Mitihani wanafanya wale walioishia Darasa la Saba, Kidato cha Pili au Cha Nne au aliyetoroka shule bila kumaliza elimu yoyote lakini anahitaji kujiendeleza kwenye Uhasibu na ana uwezo wa Kuelewa Kiingereza na Kufanya hesabu. Makundi haya yanaanzia mitihani tofauti tofauti kutegemeana na Uwezo wao wa Kitaaluma.

NGAZI ZA FOUNDATION IN ACCOUNTANCY NA MASOMO HUSIKA
  1. Introductory Certificate
FA1 Recording Financial Transactions
MA1 Management Information

Certificate hii ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 2, yaani Regulated Qualifications Framework Level 2 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 5), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Technician Certificate.
  1. Intermediate Certificate
FA2 Maintaining Financial Records
MA2 Managing Costs and Finance
Certificate hii ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 3, yaani Regulated Qualifications Framework Level 3 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 6), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Ordinary Diploma. Kwa NBAA ni sawa na Accounting Technician Level I (ATEC I)

  1. ACCA Diploma in Accounting and Business (RQF Level 4)
FAB Accountant in Business
FMA Management Accounting
FFA Financial Accounting

Diploma hii ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 4, yaani Regulated Qualifications Framework Level 4 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 7), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Higher Diploma (Diploma ya Miaka miwili), Kwa NBAA ni sawa na Accounting Technician Level II (ATEC II)
NB: Mitihani yote ya Foundation in Accountancy (FIA) ni Computer Based Exams na inafanyika muda wowote ule unaohisi wewe uko fit kufanya mtihani. Hakuna limitation zozote. Mara tu umalizapo kufanya mtihani wako, majibu yako unapewa hapo hapo
  1. Certified Accounting Technician (CAT) Qualification
Mitihani miwili tu kati ya hii hapa:
FTX - Foundations in Taxation
FFM - Foundations in Financial Management
FAU - Foundations in Audit

Certificate hii siyo ya Lazima. Mtahiniwa anaweza kuamua kuendelea moja kwa moja kwenye ACCA Qualifications mara tu baada ya kumaliza mitihani yake ya ACCA Diploma in Accounting and Business (RQF Level 4). Anayefanya hii mitihani ni Yule mtu ambaye anatamani Kubobea katika taaluma Fulani. Hapa mtahiniwa anafanya mitihani miwili tu ya chaguo lake kutegemeana na taaluma ambayo huyo mtahiniwa anatamani kubobea.

Unaweza ukaamua kuwa mtaalam wa maswala ya Kodi, Mtaalam wa maswala ya Ukaguzi au Mtaalam wa maswala ya Utunzaji Fedha. Ni uamuzi wako sasa unachagua mitihani miwili kati ya hiyo. Mitihani hii ni Paper Based Exams, na unafanya kati ya MWEZI June na December either kwa pamoja au Mmoja moja.

CAT Qualificationsi ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 6, yaani Regulated Qualifications Framework Level 6 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 8), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Bachelor Degree. Kwa NBAA ni sawa na Foundation Stage.

KWA MAELEZO ZAIDI NAMNA YA KUISOMA NA GHARAMA ZAKE
TUWASILIANE
0713388317/0757749641
NIKO DODOMA MJINI

IJUE ACCA_page-0007.jpg
IJUE ACCA_page-0008.jpg
IJUE ACCA_page-0009.jpg
 
Shukran sana kwa maelezo yako. Hakika umetupatia taarifa muhimu kwa tulio wengi.

Ngoja watu wajikusanye, japo wengi hulia na gharama.
 
Shukran sana kwa maelezo yako. Hakika umetupatia taarifa muhimu kwa tulio wengi.
Ngoja watu wajikusanye, japo wengi hulia na gharama.
Ni kweli..
Lakini ukipiga mahesabu ni nafuu zaidi kuliko kozi nyingine zote hapa nchini..

Ukiwa na 3,000,000 unafikia hiyo level ya Diploma kabisaa... Sasa hapo unaweza kuendelea na chuo kikuu mahali popote...
Sasa hivi nchini ukianzia Certificate mwaka mmoja, ukasoma tena Diploma miaka miwili, ushatumia hela kibao sawa sawa na hiyo million tatu.. Na ukumbuke kwa course zetu hizi kama mtu umefeli la saba, au form two au four huwezi kuanzia certificate, lazima kwanza uresit upate credits/pass.. Ukijumlisha gharama za kuresit na kusoma Certificate na diploma utakuta ni kubwa sana kulinganisha na hii hapa 3 million. Ni just a matter of calculation....
 
Shukrani kwa mara nyingine, unazidi kunipa mwamko na kunifungua zaidi. Huenda siku moja nitakutafuta inbox au nitakuja maeneo yako unapopigia hizi kazi kwa maelezo zaidi.
 
Sasa mkuu kwamfano mtu aliyefeli kidato cha4 anaanzaje kufanya mitihani bila kusoma?
 
Sasa mkuu kwamfano mtu aliyefeli kidato cha4 anaanzaje kufanya mitihani bila kusoma?

Si kwamba anafanya mitihani bila kusoma.. Anaanzia kusoma level ya Introductory certificate, akifaulu hiyo anaanza tena Intermediate certificate, akifaulu hiyo ndo anamalizia na Dipploma in Accounting and Business.. Akifaulu diploma yake sasa anaweza akaamua aendelee na Degree chuo Kikuu au aendelee na ACCA Qualifcation baada ya kumaliza hiyo Foundations in Accountancy..
Kwa hiyo si kwamba anafanya mitihani bila kusoma. Ni lazima uingie darasani usome na ufanye mitihani ukifaulu ndo unapewa cheti.
Karibu sana.
 
Je inatbulika na serikali!!?
Je unaweza kusoma online bila kufika hata chuoni!!?
NB
ukiwa unajib weka na namba ya usajir kabisa tujihakikishie.
 
...
CAT Qualificationsi ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 6, yaani Regulated Qualifications Framework Level 6 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 8), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Bachelor Degree. Kwa NBAA ni sawa na Foundation Stage.
...

Tanzania panazungumzwa kuwepo kwa National Qualifications Framework (NQF). Sina hakika iwapo imeshahuishwa.
 
Aha Sawa mpaka kufikia kusoma hiyo diploma in accounting and business itachukua mda gan? Nakusoma anasomea wapi au chuo gani?
 
Tanzania panazungumzwa kuwepo kwa National Qualifications Framework (NQF). Sina hakika iwapo imeshahuishwa.
Sina uhakika na hii kitu ndugu. Najua Level ya Elimu iko kwenye National Technical Awards
 
Kwasasa hapa Tanzania ili usome chuo kikuu lazima uwe na credit tano za form four hii ime kaaje???
 
Hii elimu mbona kama vile imekaa kiujanja ujanja sana? Hmm!
Hapana Mkuu.. Sema tu watanzania hatuna taarifa sahihi juu ya mambo mazuri ndo maana tunaishia kuresit tu.. Hii ni bodi Kubwa sana ya uhasibu inayotambulika na kila nchi. Ukikutana na Mhasibu yeyote muulize juu ya ACCA kama anaijua uone atakwambia nini.. Hii ukiwa nayo wewe ni ni kama Lulu mbele ya wahasibu wenzako..

Ukipata muda pitia hapa kwenye website yao. https://www.accaglobal.com/gb/en.html
Labda tu niweke kitu kimoja sawa ambacho yawezekana wengi hawajakielewa kimfumo.
Mitihani hii haitungwi na Centre yangu ya Step Ahead na wala Cheti hakitoki kwenye training centre yangu ya Step Ahead.
Mitihani yote inatungwa na kusimamiwa na hizo Bodi za Uhasibu. Kama unasoma CPA, basi mitihani hiyo inasimamiwa na NBAA (National Board of Accountants and Auditors) na Kama unasoma hii mitihani ya Kimataifa mitihani inatungwa kutoka Uingereza na Bodi ya ACCA (Association of Chartered Certified Accountants).

Kwa hiyo sisi ni kwa ajili tu ya kuwaandaa wanafunzi wanaohitaji kusoma mitihani hii, tunafundisha hayo masomo yao kutokana na mitaala yao.
Kwa hiyo ndugu yangu usiwe na shaka kabisaa juu ya Elimu hii ya ACCA kwamba imekaa kiujanja ujanja.. Naamini una ndugu yako/rafiki yeyote ambaye pengine ni muhasibu au kasomea uhasibu. Wewe muulize unaijua CPA? Halafu muulize inautofauti gani na ACCA? Na ipi ni nzuri? Ila naamini kama umepitia kwenye hiyo website ya ACCA utakuwa umepata madini ya kutosha maana wao hawafichi chochote. Huwa wanatoa taarifa zote hewani kwa uwazi kabisa. Naamini umenielewa vizuri ndugu yangu. Uwe na amani na Elimu hii ya Kiuhasibu.

Pia walichokifanya wao ni kwamba Elimu ya Certificate ambayo wengi wanaanza kusoma ukiwa umemaliza na kupata PASS kwenye mitihani ya FORM FOUR, kwa ACCA ni kwamba wameivunja katika makundi mawili ya Introductory Certificate na Intermediate Certificate, kabla hujaanza level ya Diploma. Kwa hiyo hii inamsaidia hata yule aliyefeli kabisaa au aliyeishia hata darasa la saba kupata mahali pa kuanzia, yaani introductory certificate. Sample ya Certificate
diploma-certificate-acca-acca-certificate-sample.jpg
certificate-acca-member-1-638.jpg
 
Aha Sawa mpaka kufikia kusoma hiyo diploma in accounting and business itachukua mda gan? Nakusoma anasomea wapi au chuo gani?
OK Iko hivi..
Mtu kama hana background yoyote kabisaaa na uhasibu, anaanzia kwenye level ya Introductory Certificate, hapa anafanya mitihani miwili tu..
Akifaulu hiyo mitihani miwili anaanza Intermediate Certificate, hapa napo anafanya mitihani miwili pia.. Ila Syllabus Content imeshiba, ni masomo mawili ambayo yako detailed, Ukiyafaulu hayo unakuwa umeiva kweli kweli kuuanza uhasibu..
Ukishafaulu hayo mawili ndo unaanza sasa kuisoma hiyo Diploma in Accounting and Business ambayo hiyo ina mitihani mitatu...
Kwa hiyo jumla kuna mitihani saba tu ili upate hiyo Diploma. Baada ya hapo unaweza kuamua kuendelea na ACCA ambapo utaanzia Level ya Applied Skills, au ukahamia CPA ambapo utaanzia Level ya Foundation stage, au unaamua kwenda kukaa chuoni usome degree yako ya miaka mitatu..

Je itakuchukua muda gani kuimaliza hii Diploma?
Ukiwa vizuri kichwani wa kuelewa vitu vizuri, unaweza kuimaliza ndani ya miaka miwili.. Ila ni mpaka ufaulu yote, ukifeli unarudia tena hilo somo ambalo umefeli..
Mitihani hii ni Computer Based Exams (CBE), yaani ukishajiona umeiva unaomba mtihani kuna registered CBE Centres za ACCA ndo unafanyia paper hapo. The moment unavyoclick tu Submit answers, tayari unarudishiwa na Majibu yako maana yako automated tayari kwenye mifumo yao ya computer. Na baada ya masaa 72 unapewa Cheti chako online kwenye account na hard copy wanakutumia kwenye Postal address yako uliyojisajili nayo.

Je unasomea wapi mitihani hii?
Kuna Centre ambazo ziko registered kwa ajili ya kufundisha mitihani hii... Kwa mfano ukiwa Dar es Salaam, unaweza fika pae Osman Tower karibu na Jengo la Quartary Airways kama halijabadilishwa... Pale utakuta kuna centre inaitwa Financial and Business Training Centre (FBTC), au unaenda EMERSON EDUCATION CENTRE Kule Upanga utapata Centre ya Kusoma..

Mimi Centre yangu inaitwa Step Ahead, iko hapa Dodoma mjini ndo nafundisha mitihani hiyo kwa wale wanaojiandaa..
Kwa hiyo hizo bei nilizoziweka hapo za kusoma ni kwenye Centre yangu.. Dar ziko juu kidogo..

Kwangu pia nimeweka Huduma ya Hostel kwa ambao watakuwa wanahitaji kusoma kwangu lakini wako nje ya Dodoma..
Naamini nimekujibu maswali yako.
Karibuni sana

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Je inatbulika na serikali!!?
Je unaweza kusoma online bila kufika hata chuoni!!?
NB
ukiwa unajib weka na namba ya usajir kabisa tujihakikishie.

Hello ndugu,
Naomba nielezee kitu kimoja hapa ili watu wote wakielewe..
Kuna utofauti mkubwa kati ya Academic Qualifications na Professional Qualifications.
Ukitaka kufundisha Academic Qualifications ni lazima usajiliwe na NACTE/TCU wakutambue..
Ukitataka kufundisha Professional Qualifications ni lazima usajiliwe na Board hiyo husika inayoisimamia profession hiyo husika ili ikutambue. Kwa hiyo sisi tunafundisha Professional Qualifications na tuko Registered na Bodi ya Uhasibu ya Ndani (NBAA)-National Board of Accountants and Auditors na Bodi ya Nje ya Kimataifa (ACCA)-Association of Chartered Certified Accountants. Na tuna vibali vyote vya kufanya Biashara Tanzania (Business Lisence na TIN), pia tumesajiliwa Brela na kupewa Certificate of Incorporation..
Je unaweza kusoma online bila kufika hata chuoni!!?

Hii mitihani ni Professional Syllabus Content Siyo Academic Syllabus Content. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya Academic Content na Professional Content. Tofauti kubwa kabisa hii hapa.... Academic Syllabus Contents are Very Long and Thin while Professional Syllabus Contents are Very Short and Fat...
Kama unaanza kusoma unashauriwa uingie darasani ufundishwe kila kitu na kufanyishwa mazoezi mengi ya mitihani ndo uingie kwenye paper ukiwa umeiva. Ukiingia bila kuwa na Detailed understanding, unafeli kiulaini.
Lakini pia lazima utambue kuwa Professional Syllabus is much of more Practical than Theoretical. Inakuelekeza kabisa nini unaenda kufanya makazini.
Ukisoma kwa kukariri kama vyuoni kwenye academic syllabus contents, utapata shida sana kufaulu mitihani hii..
Na kumbuka mtihani unatungwa na hiyo bodi ya uhasibu siyo chuo tunaokufundisha.. Naamini umenielewa vizuri..
Karibu sana..
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom