Kwa walio Dar es Salaam tu: Hili ndilo suluhisho la uhakika kukabiliana na gharama zilizopanda za internet

Solution ni kuifuta tu hii wizara na waziri wake asomewe albadri kama afande sele tuanze upya
Hili ndiyo suluhisho la kudumu.

Hatuwezi kuwa na mtu mpuuzi halafu anashikilia ofisi nyeti kama hii ya mawasiliano.
 
Hii serikali inachekesha sana, yani njia nzuri ya kujipatia kodi kirahisi ni ku invest katika mambo ambayo watu wanayapenda, mfano sigara na bia ndio huwa zinaongoza kwa kodi miaka mingi tu! Hivyo vitu viwili ni kama chanzo cha burudani na hutasikia watu wakilalamikia huko sababu kodi zake zimeekwa in a manner hazileti sintofahamu!

Wangeweza kulifanyia hili kazi wangesambaza internet kwa watu na kuwauzia kama ilivyo maji au umeme hakika wangepata hela sana ila wao wamekazana kuvuruga vifurushi kwenye mitandao, yani wangeweza ku regulate soko bila kuumiza watu hata hawa wenye mitandao wasingekuwa na nguvu kama ilivyo sasa
Sasa mkuu kuongezs gharama Kwa mtumiaji ndio kuongeza makusanyo ?walevi wamepungua Sana sababu ya Bei na Sasa watumiaji wa mtandao watapungua Sana ,imekuwa kama anasa sasa
 
Tujichange watu tunaoishi sehemu moja tununue starlink tuwe tunashare tu malipo ya mwezi
mkuu ile kit ya starlink ina cost bei gan kwan! na vip kuhusu anga la bongo lipo support na starlink satellites?
naona huku kwetu mambo taiti.
 
Dunia inaondoka kwenye mifumo ya analog kwenda wireless! Wewe unakuja na idea ya kuunganisha miwaya kama TTCL!
With all due Respect You don't know shit about Network/Internet. Next time uliza au kaakimya kwenye upande wa Internet itaendelea kuwa wired mpaka yesu atakapo rudi.
 
Sasa mkuu kuongezs gharama Kwa mtumiaji ndio kuongeza makusanyo ?walevi wamepungua Sana sababu ya Bei na Sasa watumiaji wa mtandao watapungua Sana ,imekuwa kama anasa sasa
Walevi wamepungua sababu hela ya kunywa tu hawana. Ukitaka kujua wanywaji wapo tangaza offer tu utawaona😁😁😁
 
Kama upo Dar maeneo ya Kariakoo, Mjini posta, Msasani, Peninsular, Upanga, Kinondoni ya Morocco, Mikocheni, Masaki, O'bey, n.k Kuna fiber za kutosha kama zuku, Raha, Gofiber, n.k

Fibre ni internet ya waya, unavutiwa waya hadi sehemu ulipo nyumbani kwako, ni internet ya waya lakini kuna kifaa utapewa kinaitwa wireless router, hiki kifaa kitakuwezesha utumie internet kwa wifi ya simu au laptop ama vifaa vingine vyenye wifi.

Kwa mfano internet ya fibre ya zuku inapatikana kino, kariakoo, msasani, peninsular, upanga,n.k utalipia elf 70 kwa mwezi (kifurushi cha chini) au zaidi (kuna vifurushi vina speed kali sana hivi ni kama watumiaji ni wengi na vina speed kali sana) pia hapo hapo utakuwa umelipia na channel za zuku utazocheki kwa kingamuzi.


A.10 Mbps = 69,000,
B.20 Mbps = 99,000
C.40 Mbps = 129,000
D.100 Mbps = 249,000.

Tukumbuke Mbps (Megabits per second) sio na zile megabytes ambazo huwa tunadownload, zile huwa na herufi kubwa ya "MB", ukitaka kujua unaweza kudownload MB ngapi kwa sekunde, hapa kilinganishi ni kwamba 1 Mbps ni sawa na MB 0.125 kwa hio mfano kifurushi A cha 10 Mbps ukifanya hesabu unapata uwezo wa kudownliad MB 1.25 kwa sekunde moja, ukija kifurushi B ni MB 2.5 kwa sekunde, n.k japo speed hushuka pale mnapokuwa watumiaji wengi mnaanza kugawana speed.

Utaweza kutumia internet bila kikomo, speed ni nzuri hata kwa kifurushi cha chini cha elf 70 ambacho unaweza kudownload mb 1 (nasikia sikuhizi ni 2) kwa sekunde, ni speed nzuri hata videos utaangalia bila kukwama na hata kwenye kudownliad utaweza kudownload muvi hata ya GB 1 kwa takribani dakika 18 tu, kitu kizuri zaidi ni hakuna kikomo, hakuna mambo ya ukifikisha gb kadhaa speed inashuka. Makampuni mengi gharama za vifaa na kuletewa waya wa internet hadi kwako ni bure ikiwa utalipia bando la mwezi au miezi kadhaa.

Changamoto ni kwamba haipo kila sehemu Dar na pia inabidi uwe mazingira ya nyumbani au ofisini ili kutumia wifi ya kifaa chao.

Kwa waliopo nje ya maeneo hayo au mikoani TTCL nao wana fibre sema nasikia ni gharama.
Huku Buza hakuna mkonga mkuu
 
Sijawahi kufurahia kifo ila kuanzia leo nimeamini Magufuli alichelewa kufa.
Alichukia uhuru wa habari mpaka akaanzisha Wizara ya kunyonga uhuru wa maoni. Mungu muweke alipopastahili.
Amekufa Vifurushi vimepanda bei
 
Amekufa Vifurushi vimepanda bei
Hili swala lilikuwa linafanyiwa mchakato kabla hajafa na huyo waziri mjinga akasema hadi kufika April watakuwa wameboresha vifurushi kuwa vya gharama nafuu.. ishu ambayo watu walikuwa wakiilalamikia ni kuexpire kwa vifurshi.

Watu walitaka vifurushi visiwe vya kuexpire, huyu waziri mjinga ndio kaja nasolution yake ya kijinga baada ya kukaa na wajinga wengine wa Wa pale TCRA
 
Sijawahi kufurahia kifo ila kuanzia leo nimeamini Magufuli alichelewa kufa.
Alichukia uhuru wa habari mpaka akaanzisha Wizara ya kunyonga uhuru wa maoni. Mungu muweke alipopastahili.

Kueleweka 0%
 
1.Kama una familia kitasaidia kuoungiza gharama za kila mtu kujinunulia data

2.unapata channels za kingamuzi cha zuku

3.utatumia bila kikomo, hata ukitumia gb 20 kwa siku ni wewe tu, nenda hata halotel uulizie hio gb 20 kwa siku sh ngap .
Ukitoka nyumbani ndiyo basi tena si ndiyo?
 
Back
Top Bottom