Kwa wale wenyeji wa SHINYANGA nisaidieni

Mayongeyonge

Member
Jan 21, 2012
14
0
Wandugu mimi ni mwl nimepangwa kazi shinyanga mjini.Ninaomba nijulishwe mazingira ya huko eg hali ya hewa, huduma za jamii,na maisha kwa ujumla.
 
Karibu sana na mimi nafanya kazi huku naenjoy, kama kawaida ukibadilisha mazingira lazima uwe na uwezo wa kuadapt. Otherwise you are welcome mkuu.
 
Karibu home! Mazingira ni mazuri, ila ukame wa hali ya hewa. Maji ya kutumia ni 24 h kutoka ziwa victoria. Watu ni wakarimu sana. Utapata ladha halisi ya kabila la wasukuma. japokuwa kuna mchanganyiko wa makabila yote. Kwa kweli hutajuta....Umepangwa shule gani? Shinyanga ni mjini bwana...ni rahisi sana kwenda dar, kahama..ama mwanza, barabara ni nzuri sana...siku hizi tumeendelea.
 
Wandugu mimi ni mwl nimepangwa kazi shinyanga mjini.Ninaomba nijulishwe mazingira ya huko eg hali ya hewa, huduma za jamii,na maisha kwa ujumla.

Shinyanga kubwa....Kuna wilaya nyingi..ni wilaya gani umepangiwa..kama ni shinyanga mjini wala huhitaji kuwaza sana...ni kama miji mingine...zamani ilikuwa ndio kuwaza sana..lakini kwa sasa huhitaji.
 
Wandugu mimi ni mwl nimepangwa kazi shinyanga mjini.Ninaomba nijulishwe mazingira ya huko eg hali ya hewa, huduma za jamii,na maisha kwa ujumla.

Hali ya hewa ya Shy itasaidia nini mkuu!
Kule zipo challenge nyingi kama ilivyo sehemu yoyote ile hapa Tanzania. Usisahau kwenda Shy na jembe la kulimia!
 
Hali ya hewa ya Shy itasaidia nini mkuu!
Kule zipo challenge nyingi kama ilivyo sehemu yoyote ile hapa Tanzania. Usisahau kwenda Shy na jembe la kulimia!

kulima sio issue mkuu ni part ya kutafuta maendeleo.sasa unauliza hali ya hewa itasaidia nini wakati huo2 unaniambia ni sisahau jembe how comes
 
Wala usihofu Shinyanga ni mkoa mzuri sana kama wewe ni mchapakazi. Ushindani ni mkubwa, gharama ya usafiri ni kubwa ingawa barabara zimeboreshwa. Nunua baiskeli/pikipiki yako kupunguza gharama ya usafiri kwa safari fupi fupi. Ukipangwa Kahama tafuta mbuga za kulima Mpunga na mahindi. Tembelea Isaka, Kagongwa, Sungamile, Kahama mjini angalia watu wanavyojitahidi kuinua maisha yao kwa kulima au kufanya biashara mbalimbali. Kazi kwako
 
Wandugu mimi ni mwl nimepangwa kazi shinyanga mjini.Ninaomba nijulishwe mazingira ya huko eg hali ya hewa, huduma za jamii,na maisha kwa ujumla.

kwanza nakupa hongera kwa kupangiwa shinyanga kwani kama uko serious na maisha basi mambo yako yatakuwa mazuri sana. Shinyanga kuna opportunity nyingi tu ni juu yako kuangalia na kuchagua ipi ufanye kwa muda wako wa ziada.hali ya hewa shy ni jua kali linaloambatana na upepo mkavu.hapa ina maana no way ukaoga maji usipake mafuta, utapauka kupita kenge. Hata hivyo hii hali ni ya muda tu wakati wa kiangazi.kipindi cha mvua hali ya hewa ni tulivu sana yaani baridi kiasi.
Huduma za kijamii zipo sana kwani kuna kila kitu unachotaka pale. maisha kwa ujumla si ghali kama mikoa mingine kwani vyakula vinapatikana kwa bei nzuri tu, na siku hizi baada ya shy kuletewa maji toka ziwa victoria ile shida ya maji haipo tena kama enzi zile za utegemezi wa maji toka ning'wa derm.
 
Shinyanga kubwa....Kuna wilaya nyingi..ni wilaya gani umepangiwa..kama ni shinyanga mjini wala huhitaji kuwaza sana...ni kama miji mingine...zamani ilikuwa ndio kuwaza sana..lakini kwa sasa huhitaji.

Mkuu naomba kama wewe una ufahamu zaidi kuhusu upatikanaji wa huduma za jamii shinyanga vijijini. Huko ndiko nilikopangwa. I will thank you in deed
 
Mkuu naomba kama wewe una ufahamu zaidi kuhusu upatikanaji wa huduma za jamii shinyanga vijijini. Huko ndiko nilikopangwa. I will thank you in deed

mkuu jana nilikuwa shy vijijini nilienda kucheki mazingira kwanza kabla ha2ja pangwa asikwambie mtu kule ni pabaya ile mbaya hakuna maji wala umeme afu shule zipo ndani sana hakuna nyumba za waalimu ni kupanga tu na nyumba zilizopo ni za tembe.mkubwa mimwenye nimepangwa uko ila niliyojionea jana hadi raha ya kupata kazi imeniisha.ni pm kwa maelezo zaidi.
 
daah nyie waalim, sasa mnataka wanetu wasomeshwe na nani?
kama pangekua hapakaliki, basi msingepangwa maana kungekua hakuna watu wakuhitaji hiyo huduma ya elimu.
 
daah nyie waalim, sasa mnataka wanetu wasomeshwe na nani?
kama pangekua hapakaliki, basi msingepangwa maana kungekua hakuna watu wakuhitaji hiyo huduma ya elimu.
Watasoma st costantine, watafundishwa na wazungu..lol
 
Kapige kazi kaka usiogope ila usikubali ukazeekea huko manake wanaua sana vikongwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom