Characteristics
Member
- Aug 21, 2019
- 17
- 17
Ndugu zangu natanguliza salamu kwenu ni matumaini yangu mko salama na mnaendelea na majukumu yenu. Kwa wale wenye changamoto za kiafya Mungu awapiganie mrudi katika hali zenu za hawali sijajua bado kama mada hii iko jukwaa husika au la.
Kama mada inavyosema huu uzi ni kwa ajili ya watu walio na tatizo la kusikia pamoja na wote wenye ndugu marafiki na majirani wenye tatizo hili tukutane hapa tupeane matibabu kwa wale waliopona hili tatizo, changamoto tunazokumbana nazo pamoja na mbinu au njia mbalimbali za kuweza kukalibiana nazo.
Nianzie kwangu, mimi ni kijana niliyebahatika kuzaliwa bila changamoto yoyote ya kiafya. Tangu mdogo nilikuwa nasikia vizuri kabisa mpaka namaliza kidato cha nne nilikuwa nasikia vizuri tu. Kipindi cha kusubiri matokeo ndio hali ilianza kubadilika na mimi sikutambua nilikuwa najua naskia vizuri tu lakini kuna rafiki yangu ndio aliyegundua na kuniuliza characteristics umekuwaje masikio siku hizi?
Kwanza nilikuwa najisikia vizuri tu baada ya siku kupita ndipo hali ilianza kubadilika kabisa; kelele masikioni zilianza. Nilikosa amani kabisa, nilikosa raha mara moja nikaanza matibabu. Nilienda Hindu Mandal hospital na Aghakhan lakini sikupata nafuu. Niliishia kupewa dozi nyingi ambazo ukimaliza unafata tena mpaka dawa zikaanza kujirudia tena yani ile ulizopewa miezi miwili iliyopita ndizo unazopewa tena mwezi huu.
Mzazi akasema twende Muhimbili lakini kabla hatujaenda Muhimbili mzazi wangu akahamishwa kituo cha kazi na kupelekwa Mwanza hivyo tukahamia Mwanza huku tukiacha makazi yetu Dar. Matibabu yakaanza Bugando nikapimwa uwezo wa kusikia (nitaweka hapa matokeo yake), dozi nimekunywa zisizo na idadi inafika kipindi mpaka mzani unakuonea huruma.
Nikaambiwa ninunue mashine yaani hearing aid tukanunua mashine hizo laki saba kinachosikitisha ni kwamba haikusaidia chochote bali zinazidisha kelele. Kuna mtu alitwambia huwa zinatofautiana ubora tununue zingine bora zaidi. Katika harakati kabla hatujanunua zingine tukapata taarifa shirika moja linagawa hizo mashine bure. Nikaenda tarehe tajwa pale Nyanza primary nikapewa hizo mashine, nazo hazikufanya chochote. Tukumbuke hapo nilisitisha kwenda form five kwa mwaka huo ili nifuatilie matibabu muda ulizidi kwenda bila matokeo yoyote kuonekana. Mwaka jana ilibidi niende tu kusoma.
Changamoto ni kubwa sana ndugu zangu lakini nashukuru Mungu nimeingia form six bila tabu yoyote na nimeanza kuzoea hali hii japo changamoto zake ni nyingi. Namisi sana kupiga story, kucheka na kujichanganya lakini Mungu ni mwema naamini ipo siku atasema neno moja tu juu yetu nasi tutapata kupona. Nilisikitika sana niliposoma uzi wa Mpauko katika harakati za kugoogle ndipo nilipoona uzi wake na kuamua kujiunga JamiiForums.
Katika harakati za kutafuta matibabu niliingia pia mtandaoni nikagundua hii hali kitaaram inaitwa tinnitus na ni watu wengi sana wanasumbuliwa na hii hali kuna mahali nilisoma wanasema wa Americans million hamsini wanasumbuliwa na hii hali.
maajabu ni kwamba watu wanapona kwa njia tofauti tofauti wengine wanapona baada ya kuanza kulala na kupata usingizi kwa masaa manane wengine baada ya kufanya mazoezi ya yoga na wengine wamepona baada ya kunya maji mengi kwa siku na kuna forum kabisa inaitwa ya watu wenye tatizo hili Web result with site links.
Tinnitus Talk
Watu wametoa shuhuda mbalimbali.
Karibuni sana.

Talk about tinnitus, pulsatile tinnitus, hyperacusis, and ear pain with us. Compassionate support with the latest research news and treatment options.
www.tinnitustalk.com
Karibuni sana.