Kwa wale wenye tatizo la kusikia tupeane ushauri mbinu za matibabu na changamoto tunazokabiliana nazo

Na tatizo hilonpia lilinikuta ukubwani...
Kuna aina mbili za usikivu kuna ile inayosababishwa na neva kwny ubongo kufa na ile ya pilihitilafu kwny mrija wa sikio nimesahu jina kitaalamu...

Ukiwa na tatizo la kufa neva sikio linakua linasikia kama kawaida sema ubongo unashindwa kutafsiri nini kinaongelewa mtu anaweza sema "Chi" we ukasikia "Kha" sasa ukiwa na shida hii hata uvae hearing aid za milioni kumi hazisaidii. Inabidi ujikubali tu kuwa wewe ni kiziwi.

Aina ya pili hyo hitilafu kwny mrija wa sikio ndio huwa ukivaa hearing aid unasikia but viziwi wengi niliokutana nao wanasema hearing aid hazisaidii so ni kujikubali kuwa husikii na kujifunza lugha ya alama..
 
Na tatizo hilonpia lilinikuta ukubwani...
Kuna aina mbili za usikivu kuna ile inayosababishwa na neva kwny ubongo kufa na ile ya pilihitilafu kwny mrija wa sikio nimesahu jina kitaalamu...
Ukiwa na tatizo la kufa neva sikio linakua linasikia kama kawaida sema ubongo unashindwa kutafsiri nini kinaongelewa mtu anaweza sema "Chi" we ukasikia "Kha" sasa ukiwa na shida hii hata uvae hearing aid za milioni kumi hazisaidii....
Inabd ujikubali tu kuwa wewe ni kiziwi..
Aina ya pili hyo hitilafu kwny mrija wa sikio ndio huwa ukivaa hearing aid unasikia but viziwi wengi niliokutana nao wanasema hearing aid hazisaidii so ni kujikubali kuwa husikii na kujifunza lugha ya alama..
pole sana pia mkuu una mda gani umepata ilo tatizo
Kukubaliana na hali ndicho kilichobaki ila naamini ipo siku
 
Tatizo kubwa ni unyanyapaa linauma sana
Mimi nimejisomea na kugundua vitamini b12 na b6 pamoja na calcium pamoja na vitamin k ukosefun tatizo so karibu vyote kwa pamoja nimetuma hivyo sikio langu LA kushoto now lina nafuu kubwa sana so kula mayai sana kila siku kunywa Maziwa mengi daily tumia blue band kwa fujo utaona changes tumia hata Maziwa ya ndio daily kwenye chai yako
 
Hii hali hata mimi pia ninayo na kwa mujibu wa makali mbalimbali nilizosoma wanasema huu ugonjwa either upone wenyewe au utumie dawa za kupunguza hali mbaya zaidi ya tinnitus....Ambazo ni sauti za kengeli,mivumo na kukwangua ndani ya sikio lakini pasipo kuwepo na sauti hizo katika mazingira ya kawaida nafikiri Vitamin B Complex ndo tumeshauriwa sana....pia kuna dawa hapo kwenye attachment wanasema huwa inaondoa tatizo hilo ila ni lazima ulipie gharama za usafirishaji maana hazi exist hapa nchini
Screenshot_20200222-225500.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupo wengi sana, cha muhimu ni kutokukata tamaa kuna njia ya operation inaitwa "cochlear implant". Hii inatatutua tatizo lote, ila gharama. Na matibabu yake hadi ulaya au marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hali imenifanya niwe kivutio zaidi mtaani yani unaonekana kituko zaidi unaweza kuitwa jina lako "xxx"wewe ukaitikia "asante nashukuru nimeshakula "/ watu wanacheka kweli kweli inabidi na wewe ucheke tu bila kujua tu cha msingi ni kujikubali tu hakuna dawa wala hearing aid zakusaidia tatizo hili la Usikivu ambalo ubongo kushindwa kutafsiri sauti kwenye sikio " tinnitus"

nimeangaika mahospital vyumba vya ent nimepima sana nimeambulia kuambiwa nina hatua ya tatu ya usikivu nitumie hearing aid mtaa mzima makelele yanaamia masikio kwangu nikatupa kule nikaenda buguruni malapa deaf school pale kujifunza lugha ya alama cha ajabu mtaani hakuna anaye fahamu lugha hiyo nikaona isiwe taabu nikaanzacheza na lips language aiseee na weza ongea na mtu na asijue kuwa I am deaf sometime mpaka nafurahia kuwa hivi.

nimeshafanya oral interview mara kibao naongea na ma hr vizuri kweli kweli mpaka wanashanga your deaf yes I am
kikubwa ni kujikubali tu
Life going on
All deaf go to heaven

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Never lose hope wakuu binadamu tunapitia shida nyingi sana kuna wengine wanamatatizo ya macho kutokuona, wengine wanahangaika kupata watoto, wengine wanashida ya uvimbe , wengine cancer, wengine kisukari wamekatwa na vidole ila sukari haipungui,

Si hivyo tu wengine ni ulemavu wa viungo uliotokana na ajali, wengine hawana wazazi wala ndugu hata mmoja, wengine wamelazwa mahospitalini nusu mwaka bila tatizo kuonekana, kuna waliokataliwa na wazazi.

ukipata muda wa kujua shida za wengine kwa undani utaona kabisa afadhari shida yako, Mungu ni mwema na hawezi kuruhusu jambo gumu litalokushinda kulibeba hata siku moja hiyo shida uliyonayo ndiyo mapito yako na mzigo wako unaoweza kuubeba...

ukifika muda sahihi yeye atajua akuponye kwa njia gani maana hakuna linalomshinda luka 1:37

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JIKUBALI

hili tatizo kumbe Ni kubwa hivi nilikuwa sijui. Marekan watu mil 50 .
Hizi Dawa za malaria nilivyokuwa primary nikizimeza maskio yalikuwa yanazibaga doz ikiisha yanazibuka.

Kuna mtoto wa Ndugu yangu nahisi anahili Tatizo mzazi wake Ni mbishi anasema atakaa poa tu na hataki kumpeleka hospital tatizo kabla halijawa kubwa.
 
Characteristics,

Mkuu nilidhani niko peke yangu! yani we tatizo lako ni copy ya la kwangu, wakati nasoma it was like unaniongelea mimi. let me share my story and testimony

nilizaliwa mzima kabisa kufika mwaka 2007 niko form one nimerudi likizo nikaanza kusikia sauti za ajabu ajabu kama maporomoko ya maji mara mashine kama engines na mwangwi fulani. Taratibu nikaanza kupoteza uwezo wa kusikia (almost miaka 13 sasa imepita)

tulihangaika KCMC, BUGANDO, Muhimbili etc etc nikapewa hearing aids hazikusaidia, tukaenda clinics mbalimbali hasa ile ya wahindi “hearwell clinic” pale upanga tilikua yunanunia devices kila mara na hazikuzaa chochote.

kuna kipindi nilienda ujerumani nikakutana na specialist aka recommend hearing aids ila hazikusaidia anything. Nilianza ku search nkajua tatizo linaitwa “tinnitus” na halina tiba specific....In the end nikamwambia baba ukweli tu kuwa tuache kupoteza fedha now ntaishi hivihivi, ilikua ngumu kuelewa ila in the end alielewa.

Challenges
1. mwanzoni nilipata shida sana hada O level kimasomo nilishuka sana (sikua namsikia mwalimu)
2. watu walikua wananikejeli sana (it hurts aisee)
3. socialization ilipungua (nkawa najitenga na watu na sipendi maongezi na watu)
4. kuongea na simu kwa calls ni changamoto haswa

Good news ni kwamba after several years niliweza kukabiliana na tatizo langu (ingawa naona kuna improvements ukilinganisha na kipindi linaanza, now mtu kujua nna tatizo ni mpaka akae na mimi sana)

Achievements
1. Pamoja na kuwa na tatizo langu nilikua best student form 6 shuleni kwetu
2. chuo bachelor degree nikapata best student award in research
3. Masters nikapata best student award tena (nimemaliza mwaka jana december)
4. pamoja na tatizo langu nimeweza kufanikiwa kushirikishwa projects nyingi nimetembelea nchi kama germany, austria and hungary (2017) finland turkey and estonia (april 2019)

na sasa nina plan kuchukua PhD nishaanza applications.... my dream ni kuwa professor

nnachotaka ku advice wenzangu wenye tatizo hili, don’t let it demotivate you, unaeza fanya mambo makuu watu wakaishia kushangaa.. wala usiwe too emotional mtu akikukejeli cheka nae.. zamani nilikua naumia ila now tunacheka pamoja.

samahani meseji ndefu sana... ila am sure my testimony itakua na msaada kwa watu wachache.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Poleni sana àisee
Kuna uncle wangu sasa yapata miaka 20 masikio yameziba kbs
Nae alianza taratibu na amehangaika sana,sema ndg hawamtengi wala kumnyanyapaa na kazini hakufukuzwa wala kuachishwa,yan mimi nikikaa na watu wasiosikia wala sipati shida coz nishamzoea uncle hali yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah inwuma sana mie naona nipo hilo la neva yani ktu akiongea simuelewi anaongea nini naona ka lugha mpya vile..
Afu sasa ndugu wanakomaa kuvaa earing aid hzisaidii chochote mikelele tu
Na tatizo hilonpia lilinikuta ukubwani...
Kuna aina mbili za usikivu kuna ile inayosababishwa na neva kwny ubongo kufa na ile ya pilihitilafu kwny mrija wa sikio nimesahu jina kitaalamu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afadhali wewe mimi tangu darasa la pili ila now niko chuo. Cha kushangaza wanaosikia ndio wananiomba niwaeleweshe topic.
mtoa mada mimi tokea form 1 si sikii vizuri na sijawahi kuona ubaoni, nikawa mzee wa kuakaa nyuma class ,yaan ushahidi tuu nipo class ,but na kipaji cha hesabu yaani kile chenyewe siyo cha kawaida ,embu fikiria diploma nilikuwa na G.P.A YA 4.3 ,Degree na G.P.A YA 3.4 na sasa mwezi wa kumi nataka nianze masters ya actuarial science pale IFM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto zangu za shule zilipotelea mbali sababu ya changamoto hii pia kutokama na wazazi sio watu wa kucare sana kipindi cha mwanzoni nilionekana nina kibuli wala sio uziwi,wakati naanza secondary nilikua nikishika namba darasani nilipachikwa. Jina la dokta kwakua nilikua mkali wa masomo ya sayansi vibaya mno.

Wakuu tuna mengi mno yakusimulia ila tunapitia changamoto kutofautia na mazingira sana sana sisi tulio kuwa deaf ukubwani hatujui sign language hatuja soma uzi huu unanifuta machungu na kunipa faraja sana naomba nitoe pendekezo zaidi tusiishie kuelezea mapito pia tusaidiane zaidi kuji ng'amua katika swala zima la kiuchumi hasa katika kipindi hichi kigumu tunao angaika kutafuta kazi,tulio fukuzwa kazi ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami soon nitaleta story yangu yote mnayosimulia mnanikumbusha mbali sana mahangaiko yote ila Mungu ni mwema sana shida ya usikivu haijaisha ila maisha yanasonga nina tatizo hili Kwa zaidi ya miaka 25 sasa ila nashukuru Mungu naweza kusocialize na watu vizuri sifeel kunyanyasika tena kama zamani ingawaje usikivu bado ni changamoto ila Kwa msaada wa Hearing Aids maisha yanasonga nitaleta story za vitimbi nilivyopitia nikipata wasaa mzuri.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom