Kwa wale wenye matatizo sugu ya tumbo kama mimi tukutane hapa!!!!

ufumawicha

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
504
209
Wale wote ambao mmepona matatizo ya matumbo au bado manaumwa kama mimi tukutane hapa ili tuweze kushauriana nini cha kufanya kwani naamini humu Jf ndiyo kila kitu!Mimi nimeugua Tumbo sasa ni mwaka wa 21.Linaunguruma,linauma sana na kujaa mithili ya puto.Nimezunguka sana hadi kufikia sasa natibiwa hapa rufaa mbeya ila hakuna unafuu.Wanashuku vidonda vya tumbo lakini nimeshapima Ultra sound,Barium meal,barium enema,Widal test na H.pyrol test vyote havijaonyesha ugonjwa.Sasa kila chakula nikila ni tatizo tumboni.Nilijaribu pia kuwaona watu wa tiba mbadala lakini sifichi baada ya mwezi mmoja wa kutumia dawa zao nilizidiwa na ajabu nilipowasiliana na wale watu wa tiba mbadala kuwa nimezidiwa hata simu hawakupokea!!!!
Kwa mliowahi kupona tupeni ushauri ili nasi tujaribu kufanya kama nyie.
 
jitahidi kula kwa wakati, vyakula viwe laini na sio vikavu, usitumie pilipili au chakula chenye chumvi nyingi, pendelea maji ya kunywa ya vuguvugu na si baridi, usinywe uji wa ulezi, usinywe kimiminika kilicho na gesi, achana na nyama za kukaanga kama kitimoto, fanya hivyo bila kukosa kwa wiki moja mpaka mbili hata ukisikia maumivu jikaze ufanye hivyo kwa muda huo baada ya hapo utatupa feedback jamvini
 
Nakushukuru sana kwa ushauri,ndugu.
Ninaanza kuufanyia kazi sasa hivi.Hata hivyo naomba unieleweshe hili.Nimekuelewa kuwa natakiwa niache vyakula vya kukaanga kwenye mafuta lakini namna gani vyakula ulivyosema kama nitakuwa nachemsha tu kwenye maji nalo hilo ni baya?Pia kula kwa wakati unamaanisha nini?
 
Wale wote ambao mmepona matatizo ya matumbo au bado manaumwa kama mimi tukutane hapa ili tuweze kushauriana nini cha kufanya kwani naamini humu Jf ndiyo kila kitu!Mimi nimeugua Tumbo sasa ni mwaka wa 21.Linaunguruma,linauma sana na kujaa mithili ya puto.Nimezunguka sana hadi kufikia sasa natibiwa hapa rufaa mbeya ila hakuna unafuu.Wanashuku vidonda vya tumbo lakini nimeshapima Ultra sound,Barium meal,barium enema,Widal test na H.pyrol test vyote havijaonyesha ugonjwa.Sasa kila chakula nikila ni tatizo tumboni.Nilijaribu pia kuwaona watu wa tiba mbadala lakini sifichi baada ya mwezi mmoja wa kutumia dawa zao nilizidiwa na ajabu nilipowasiliana na wale watu wa tiba mbadala kuwa nimezidiwa hata simu hawakupokea!!!!
Kwa mliowahi kupona tupeni ushauri ili nasi tujaribu kufanya kama nyie.
mkuu mm huu ni mwaka wa pili tumbo hqliumi sema linajaa gesi halafu linakuwa gumu sana kias nlikua siwez kula zaid ya kunywa chai au uji nmeangaikq sana hospital kubwakubwa bila mafanikio ila nmetumiq ubuyu nliambiwa tu na babu mmoja ukwel nna nafuu kubwa sana kwan naweza kula jqpo ni baadhi ya vyakula lqkin nashukuru kwan nlikuwa hali mbaya lilikuwa limevba kias hata kujisaidia nlikua nasimama mana nkichuchumaq siwez jarbu ubuyu mumuja na tafuna ile mbegu utaona matokeo au tafuta mafuta yake kabisa mkuu yan sitak hata kukumbuka mana nlikuwa nmekata tamaa kabisa.
 
Mimi lilinisumbua wiki iliyopita nikatumia dawa za kuua minyoo sasa hivi naliona liko poa kabisa
 
mkuu mm huu ni mwaka wa pili tumbo hqliumi sema linajaa gesi halafu linakuwa gumu sana kias nlikua siwez kula zaid ya kunywa chai au uji nmeangaikq sana hospital kubwakubwa bila mafanikio ila nmetumiq ubuyu nliambiwa tu na babu mmoja ukwel nna nafuu kubwa sana kwan naweza kula jqpo ni baadhi ya vyakula lqkin nashukuru kwan nlikuwa hali mbaya lilikuwa limevba kias hata kujisaidia nlikua nasimama mana nkichuchumaq siwez jarbu ubuyu mumuja na tafuna ile mbegu utaona matokeo au tafuta mafuta yake kabisa mkuu yan sitak hata kukumbuka mana nlikuwa nmekata tamaa kabisa.
Ndugu nikolaus,ni ubuyu wa aina gani maana nimetembea Mwanjelwa mbeya kila ninaoupata tayari umewekewa rangi au hata huo unafaa?
 
mkuu mm huu ni mwaka wa pili tumbo hqliumi sema linajaa gesi halafu linakuwa gumu sana kias nlikua siwez kula zaid ya kunywa chai au uji nmeangaikq sana hospital kubwakubwa bila mafanikio ila nmetumiq ubuyu nliambiwa tu na babu mmoja ukwel nna nafuu kubwa sana kwan naweza kula jqpo ni baadhi ya vyakula lqkin nashukuru kwan nlikuwa hali mbaya lilikuwa limevba kias hata kujisaidia nlikua nasimama mana nkichuchumaq siwez jarbu ubuyu mumuja na tafuna ile mbegu utaona matokeo au tafuta mafuta yake kabisa mkuu yan sitak hata kukumbuka mana nlikuwa nmekata tamaa kabisa.
Kutibu gasi, kunywa maziwa chnganya na vitunguu thaumu, kunywa wakati wa kulala kila siku mpaka utakapo ona uko fit, jee hutoki damu unapo pata haja kubwa?
 
Mimi lilisha nitesa sana,nikaja kugundua kuwa tatizo langu ni pale ninapokula nyama nyekundu ndio huwa napata shida,huwezi amini mkuu tokea nilipoachana nazo mpaka leo ni takribani miaka 8,tumbo langu liko shwari kabisa.Jaribu hiyo kama utaiweza ingawa ni ngumu kidogo mwanzoni.Pia kuna vitu kama maziwa fresh situmii,maharage na jamii zake situmii kabisa.Kiurahisi uwe na diary ambayo utakuwa unarekodi aina ya vyakula ambavyo ukila tumbo lako linakuletea shida,ukishavijua epukana navyo.
 
Nakushukuru sana kwa ushauri,ndugu.
Ninaanza kuufanyia kazi sasa hivi.Hata hivyo naomba unieleweshe hili.Nimekuelewa kuwa natakiwa niache vyakula vya kukaanga kwenye mafuta lakini namna gani vyakula ulivyosema kama nitakuwa nachemsha tu kwenye maji nalo hilo ni baya?Pia kula kwa wakati unamaanisha nini?
kama unachemsha nyama yani supu sio mbaya lakini sio ukaange au kuchoma yani usile kavu kavu kama ni ya kuchoma basi iwe laini sana sana, kula kwa wakati namaanisha usiruhusu tumbo kuwa wazi yani asijipe muda mrefu bila kula hadi ukahisi njaa, jitahidi kula mara kwa mara hata kama ni chakula kidogo sio mbaya kuliko kusubiri njaa ikuume.
 
Jamani poleni sana kwa wanaosumbukiwa na mago jwa ya tumbo.Naomba kushare nanyi experience,kuna duka moja mjini moshi linaitwa mombasa store lipo double road opposite office za tigo,hawa jamaa ni wataalamu wa dawa mbali mbali hasa za tumbo.Kwa yeyote anayeweza kuwatembelea ajaribu.Dawa za hasa za magonjwa ya tumbo ni nzuri sana.Wanatoa pia ushauri kuhusu magonjwa mengine.
 
Kutibu gasi, kunywa maziwa chnganya na vitunguu thaumu, kunywa wakati wa kulala kila siku mpaka utakapo ona uko fit, jee hutoki damu unapo pata haja kubwa?
Damu sitoki,isipokuwa wakati fulani choo huwa ngumu
 
Kutibu gasi, kunywa maziwa chnganya na vitunguu thaumu, kunywa wakati wa kulala kila siku mpaka utakapo ona uko fit, jee hutoki damu unapo pata haja kubwa?
Hapo kwenye vitunguu saumu nitaomba tushauriane,ni aina gani inafaa?Maana sasa hivi ziko aina nyingi sana!
 
Wale wote ambao mmepona matatizo ya matumbo au bado manaumwa kama mimi tukutane hapa ili tuweze kushauriana nini cha kufanya kwani naamini humu Jf ndiyo kila kitu!Mimi nimeugua Tumbo sasa ni mwaka wa 21.Linaunguruma,linauma sana na kujaa mithili ya puto.Nimezunguka sana hadi kufikia sasa natibiwa hapa rufaa mbeya ila hakuna unafuu.Wanashuku vidonda vya tumbo lakini nimeshapima Ultra sound,Barium meal,barium enema,Widal test na H.pyrol test vyote havijaonyesha ugonjwa.Sasa kila chakula nikila ni tatizo tumboni.Nilijaribu pia kuwaona watu wa tiba mbadala lakini sifichi baada ya mwezi mmoja wa kutumia dawa zao nilizidiwa na ajabu nilipowasiliana na wale watu wa tiba mbadala kuwa nimezidiwa hata simu hawakupokea!!!!
Kwa mliowahi kupona tupeni ushauri ili nasi tujaribu kufanya kama nyie.
-->>FANYA FRUIT FASTING/
YAANI ISHI KWA KULA MATUNDA MBALIMBALI MPAKA USHIBE KWA MWEZI MMOJA/ NI GHALI NA KITU KIGENI SANA AFRICA / BUT 100% TIBA.KAMILI.
 
Back
Top Bottom