Kwa wale wenye maduka ya reja reja ni kitu gani ukiweka kinavutia zaidi wateja?

H
IMG_20210116_210334_632.jpg
 
Duka ni vitu vya chini !

Nikisema vitu vya chini namaanisha;
_Mafuta ya kula na ya taa.
_Unga.
_Mchele.
_Maharage.(Weka ya aina tofauti tofauti)
_Sukari.
_Ngano (ya unga ukiweza weka na nzima)

Na ;
_Kama una friji weka maziwa flesh na mtindi aya ya Tangaflesh ,Darflesh ,Asas nk.
_Pia kama uko uswahilini weka yale maji ya kandolo uza 100 (hapa utarudi kunishukuru)

Cha mwisho na chamuhimu zaidi;
_Kuwa na kauli nzuri kwa kila mteja anayefika ofisini kwako.

All the best.
 
Sijachelewa sana
Hata wewe pia hujachelewa.

Chunguza kwa makin sana ni nini watu wanaokuzunguka wamekosa au wanakipata umbali mrefu kiweke wewe
Mfano makaron, brush na nafagio ya ndan dawa na manukato ya maliwaton, vioshea vioo nk
2
Jenga uaminifu na wateja wako akiulizia kitu Kama hakipo muahid kuw utaleta
3 tafuta sehemu ya kuaminika na ya Bei Chee kwa ajili ya kuchukulia vitu
Nk epuka kununua vitu kidogo kidogo hutaona faida yake
Nidhamu+heshima+ucheshi +uaminifu = wateja wa kudumu
Tumia mfumo wa FIFO (first in, first out) kuepuka vitu kuexpire vukiwa dukan

Muelezee mteja furaha yako kwa yy kufika dukan kwako
4 kuwa wa kwanza kufungua na uwe wa mwisho kufunga



All the Best mpambanaji
 
Unajua watu wengi hapo ndipo tunapofeli kwenye biashara. Biashara haiendi ivooo.. Huwezi kuweka dukani mali unazotaka ww.
Kwasababu wateja wanatofautiana baina ya eneo moja hadi jingine. kitu kinachouzika sinza haina maana kinaweza pia kinaweza kuuzika manzese. Ni maeneo mawili tofauti na mahitaji yao ni tofauti na hivyo biashara zitakua Zinatofautiana.

Huezi screenshot duka lako ukamwambia na ww weka hiv. Unless muwe eneo moja (location) otherwise unaeza mwingiza mwenzio chaka akaleta mali dukani kwake zisizotoka na baadaye zikaexpire na kuleta hasara kubwa.

Ukitaka ndugu yangu usifeli WEKA DUKANI MALI WATEJA WANAZOTAKA SIO WW UNAZOJISIKIA TUU KULETA.
Uwe na daftari na peni nzuri. Alafu andika zile mali wateja wanakuuliza. Aĺafu ukiona Mali hiyo wanaiuliza uliza haraka sana waletee wateja wako ili wasiikose na ww upate maheraaaaa.

Mwisho wa siku utajikuta una duka lenye mali zinazotoka na kukupa faida kwa wepesi.
Ni yangu tuu ayooo!!!
 
Vocha na bidhaa zingine ndogondogo lakini kwa ujumla biashara ya duka ni pasua kichwa sana sikushangai ww kuomba ushauri
 
Najiuliza niongeze nini dukani kwangu. Bidhaa gani ni nzuri dukani na zina faida nzuri kidogo. Hili duka si la hali ya chini sana ni duka la kati.

Karibuni tujadili nini na nini kisikosekane dukani kwanza kina faida halafu kinavutia wateja.
Mara chache chache toa zawadi ya pipi kwa wateja hasa watoto wanaotumwa hapo dukani. Hao watakuwa wateja waaminifu. Akitumwa dukani hataenda duka lingine bali atakuja dukani kwako
 
Back
Top Bottom