Kwa wale wazoefu wa kununua simu mkononi msaada wenu unahitajika

Brown Mduma

Senior Member
Sep 29, 2020
180
283
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza naomba mnipe muongozo mzuri.

Natarajia kununua simu kwa mtu kwa shilingi 280000 ni nzuri ila wasiwasi wangu ni ku risk pesa afu mwisho wa siku ikaniletea uhalifu wa kuuambiwa nimeuziwa simu ya wizi.

Anaeuza kasema yupo tayar kuandikisha ata police coz simu ni yake ila sijui sehemu husika ya kuandikishana kwa issue kama hii ni wap ndio maana nimeona ngoja niombe ushauri kwa WanaJF
 
Nunua simu mkuu
Usiwe na wasiwasi kama ni yake na risiti ipo.

Cc: Mama Nla
 
Risiti zinaandikwa tu siku izi unaweza kwenda dukan ukafanya mpango ukapewa risiti
 
Kama yakwake kweli akupe na lisiti. Otherwise usinunue labda kama unamfaham na mnaaminiana sana
 
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza naomba mnipe muongozo mzuri.

Natarajia kununua simu kwa mtu kwa shilingi 280000 ni nzuri ila wasiwasi wangu ni ku risk pesa afu mwisho wa siku ikaniletea uhalifu wa kuuambiwa nimeuziwa simu ya wizi.

Anaeuza kasema yupo tayar kuandikisha ata police coz simu ni yake ila sijui sehemu husika ya kuandikishana kwa issue kama hii ni wap ndio maana nimeona ngoja niombe ushauri kwa WanaJF
No aina gani ya hiyo simu unayotaka kuinunua kwa 280k?
 
Ila kuna watu hata hawajali huwa wananunua tu, jana nimetangaza simu yangu fb fasta kuna dogo akanicheki anaitaka..hajaleta complication zozote mpka nikashangaa.
 
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza naomba mnipe muongozo mzuri.

Natarajia kununua simu kwa mtu kwa shilingi 280000 ni nzuri ila wasiwasi wangu ni ku risk pesa afu mwisho wa siku ikaniletea uhalifu wa kuuambiwa nimeuziwa simu ya wizi.

Anaeuza kasema yupo tayar kuandikisha ata police coz simu ni yake ila sijui sehemu husika ya kuandikishana kwa issue kama hii ni wap ndio maana nimeona ngoja niombe ushauri kwa WanaJF
Jihadhari na ujiepushe na kununua bidhaa kwenye black market
 
dah mie kununua simu kwa mtu haitatokea tena maisha,bora nika bila simu,nimelala polisi na kulipa hela kibao ili kesi iishe dada anakwambia kaibiwa kila kitu.hela nlitoa na ndani nililala
 
ukinunua kitu mkonon kama electroncs nenda kaandikishiane polisi au ofisi ya mtaa/kijiji inakuwa salama zaid ishu za risiti nying znaghushiwa za kutosha so usikimbilie sana risiti
 
Hiyo hela unapata simu nzuri tu dukani mpyaaa

Hata mkiandikishana kama ni ya wizi mwisho wa siku itakula kwako tu au utapata usumbufu mkubwa usio na ulazima
 
Back
Top Bottom