Kwa wale watu wa kikosi Maalum (Makomandoo) mliopo JamiiForums nitashukuru leo mkinijibu haya Maswali yangu yafuatayo

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
2,211
45
Umeandika mengi sana asilimia 90% ni uongo.Usifikiri komando lazima awe mwanajeshi.Kuna mtu anaweza kuwa komando lakini jeshi la magereza au polisi au pengine hata raia.Komandoo anaweza kuwa private lakini hana cheo chochote.Au akawa hata ofisa mkubwa.Ukomandoo ndani ya jeshi ni tawi moja wapo kama matawi mengine mfano ma dr na ma engineer.Ila labda kwa upande wa Jeshi komandoo katika medani zake wanafundishwa kutumia mikono zaidi kuliko silaha.
Kumbuka ukomandoo sio cheo ni fani kama fani zingine ndani ya jeshi .Magereza wapo makomandoo walio bobea.Unakumbuka wale waliotaka kupindua serikali mwaka 1982 mmoja wapo alikuwa anaitwa Tamim akauwawa pale kinondoni mkwajuni walipotupiana risasi na mtu flani jina namuhifadhi basi alikuwa ni raia wa kawaida tu japo alisomea ukomandoo alikuwa anaitwa Kamando Tamim hata kumpiga risasi walipata tabu sana.
 
KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,109
2,000

Maelezo mengi na marefu halafu yote ni Pumba tupu tu. Kwani ukibakia tu kuwa Msomaji na ukawaacha wanaojua Wachangie nawe Ujifunze utapungukiwa nini?
 
mkorea

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
3,431
2,000
Tulipokuwa Quba kwenye mafunzo nilipenda wanatuchukulia kama raia wa kawaida hata madem wa kule unapita nao....kurudi sasa yaani ni kero ukitaka kujichanganya na wana wa kijiweni kidogo simu isha ingia ni kero sana,ulinzi ulinz ulinzi hata ukitaka kuendesha bila leseni unatumia kitambulisho au gwanda,kuna siku nilikula bure kwenye mgahawa mmoja wa kishua jijini hapo...walivyoita mabaunsa nikatoa gamba wakanyong'onyea kama kuku wa mdondo.Ni kweli kuna siku niliamkiwa na dc halafu mimi ni janja tu sijagonga hata 30 nikaamkiwa na zee zima.
 
kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
16,336
2,000
Commando anakuzwa sana
Wakawaida sana Jana mmoja alikuja kuosha gari carwash anataka kuoshewa kwa buku 2 anasema gari sio lake la wananchi alikuwa katika jokes tu baadae akatununulia na ndizi tukala akasepa zake
 
kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
16,336
2,000
wapo makomandoo ila sio hawa wetu wa sasa iv,wamenenepeana....shoo zao wanavunja tofari lenye ratio ya mchanga mwingi sement kidogo pale taifa...wanapinda nondo ya milimita nne wanajiona wamepinda chuma..
Jana nimemuona kijana kwenye 34 ivi uniform mpya maroon ballet na bawa na sigara zake hana kitambi wala hajajazia kama harmonize
 
Rwehumbizadarlin

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
284
1,000
1. Je, ni kweli kuwa Majasusi wengi huwa ni Makomandoo?

2. Je, ni kweli kuwa katika Mafunzo yenu ya Ukomandoo huwa kuna Kipengele cha Kujifunza Uchawi?

3. Je, ni kweli kuwa kwa uwezo wenu mkubwa wa Kimedani nyie huwa hamna Kiwango Maalum cha Mishahara na kwamba Kiwango ukitakacho ukikiomba tu unapewa tena ukiwa unatetemekewa na kupigiwa Magoti?

4. Je, ni kweli kuwa Makomandoo wote wanatakiwa kujua Kuongea Lugha za Kimataifa kuanzia 7 mpaka 12 tena Kiufasaha kabisa?

5. Je, ni kweli kuwa Komandoo akiwa Likizo kuanzia OCD, RPC, DSO, RSO, RC, IGP pamoja na Mjumbe wa Nyumba Kumi wanatakiwa wajue na kila Siku wawe wanakupigia Simu kukuulizia hali yako na ikiwezekana hata Kukuamkia Shikamoo na Kukupigia Saluti huko huko waliko hata kama huwaoni?

6. Je, ni kweli kuwa Makomandoo mkiwa katika Mafunzo au Maisha yenu huko katika Kambi yenu msipopelekwa maeneo yenye ama Chatu wengi au Mito yenye Mamba wengi mkapambane nao huwa hamsikii raha mpaka kufikia Kitendo cha Kununa na hata Kususa Kula?

7. Je, ni kweli kuwa Makomandoo 5 mpaka 7 tu kwa Uwezo wao mkubwa wa Kimedani wakiamua Watu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam tulale Saa 6 Mchana na tuamke Saa 12 Jioni Kesho yake kwa kutupa Adhabu zenu inawezekana?

8. Je, ni kweli kuwa aina ya Karate wanayojifunza Makomandoo ni ile ya COMBAT ya Kuua kabisa Mtu au Adui na siyo hizi za Kawaida za Kumjeruhi tu Adui / Mtu mara moja kisha unamruhusu akale Ugali na Maharage Kwao?

9. Je, ni kweli kuwa Makomandoo wengi huwa hawana Watoto na kwamba hata uwezo wao wa Kuzalisha huondolewa au huondoka automatically tu kwa aina ya Mazoezi magumu na ya Hatari mnayofanya?

10. Je, ni kweli kuwa Makomandoo wengi huwa wakifikisha Umri wa kuanzia Miaka 55 hupewa Sumu na Kufa kwakuwa wanakuwa siyo Productive tena Kimedani na kwamba wanahofiwa wanaweza Kuvujisha au kutoa Siri za Jeshi na hata za nchi kwa Maadui?

11. Je, ni kweli kuwa ili Kozi ya Ukomandoo iwe imefana inatakiwa kama mlikuwa mmeingia 100 Mafunzoni basi 55 wawe Wamekufa na 25 wawe wamejeruhiwa kwa kuwa Vilema na wengine hata Makolomero yao na Ulimi kujitokeza Mdomoni na 20 tu ndiyo wawe Hai na Kukamilika?

Sasa ni wakati wa nyie Kunijibu tu nijue.
Yote ni kweli ,apa nilipo nina miaka 54 wamenambia mwakani ntakunywa sumu vikombe 30 ili nife japo hyo sumu ukimpa mtu mzima kijiko ki1 amelala yoooo
 
chef detat

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
16,391
2,000
Kitu pekee umekaribia kupatia kwa mbali,ni kweli macomando hureport kambi ya jeshi iliyo karibu lakini hawatafutwi kujuliwa halli na mtu ni wana report tu kwa sababu za ki usalama.
Police pia hu report kwa sababu sometimes husafiri na bunduki mfano smg kwenye gari
 
EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,416
2,000
Tulipokuwa Quba kwenye mafunzo nilipenda wanatuchukulia kama raia wa kawaida hata madem wa kule unapita nao....kurudi sasa yaani ni kero ukitaka kujichanganya na wana wa kijiweni kidogo simu isha ingia ni kero sana,ulinzi ulinz ulinzi hata ukitaka kuendesha bila leseni unatumia kitambulisho au gwanda,kuna siku nilikula bure kwenye mgahawa mmoja wa kishua jijini hapo...walivyoita mabaunsa nikatoa gamba wakanyong'onyea kama kuku wa mdondo.Ni kweli kuna siku niliamkiwa na dc halafu mimi ni janja tu sijagonga hata 30 nikaamkiwa na zee zima.
Shikamoo komandoo. Mi sijambo pamoja na mke wangu wote familia nzma tunakuamkia shikamoo baba mzazi.
 
Andres

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
380
1,000
Yaani ungejua hali kwa ground ilivyo.. anyway, somethings are better when are unknown to mass
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom