Kwa wale watu wa kikosi Maalum (Makomandoo) mliopo JamiiForums nitashukuru leo mkinijibu haya Maswali yangu yafuatayo

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,109
2,000
1. Je, ni kweli kuwa Majasusi wengi huwa ni Makomandoo?

2. Je, ni kweli kuwa katika Mafunzo yenu ya Ukomandoo huwa kuna Kipengele cha Kujifunza Uchawi?

3. Je, ni kweli kuwa kwa uwezo wenu mkubwa wa Kimedani nyie huwa hamna Kiwango Maalum cha Mishahara na kwamba Kiwango ukitakacho ukikiomba tu unapewa tena ukiwa unatetemekewa na kupigiwa Magoti?

4. Je, ni kweli kuwa Makomandoo wote wanatakiwa kujua Kuongea Lugha za Kimataifa kuanzia 7 mpaka 12 tena Kiufasaha kabisa?

5. Je, ni kweli kuwa Komandoo akiwa Likizo kuanzia OCD, RPC, DSO, RSO, RC, IGP pamoja na Mjumbe wa Nyumba Kumi wanatakiwa wajue na kila Siku wawe wanakupigia Simu kukuulizia hali yako na ikiwezekana hata Kukuamkia Shikamoo na Kukupigia Saluti huko huko waliko hata kama huwaoni?

6. Je, ni kweli kuwa Makomandoo mkiwa katika Mafunzo au Maisha yenu huko katika Kambi yenu msipopelekwa maeneo yenye ama Chatu wengi au Mito yenye Mamba wengi mkapambane nao huwa hamsikii raha mpaka kufikia Kitendo cha Kununa na hata Kususa Kula?

7. Je, ni kweli kuwa Makomandoo 5 mpaka 7 tu kwa Uwezo wao mkubwa wa Kimedani wakiamua Watu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam tulale Saa 6 Mchana na tuamke Saa 12 Jioni Kesho yake kwa kutupa Adhabu zenu inawezekana?

8. Je, ni kweli kuwa aina ya Karate wanayojifunza Makomandoo ni ile ya COMBAT ya Kuua kabisa Mtu au Adui na siyo hizi za Kawaida za Kumjeruhi tu Adui / Mtu mara moja kisha unamruhusu akale Ugali na Maharage Kwao?

9. Je, ni kweli kuwa Makomandoo wengi huwa hawana Watoto na kwamba hata uwezo wao wa Kuzalisha huondolewa au huondoka automatically tu kwa aina ya Mazoezi magumu na ya Hatari mnayofanya?

10. Je, ni kweli kuwa Makomandoo wengi huwa wakifikisha Umri wa kuanzia Miaka 55 hupewa Sumu na Kufa kwakuwa wanakuwa siyo Productive tena Kimedani na kwamba wanahofiwa wanaweza Kuvujisha au kutoa Siri za Jeshi na hata za nchi kwa Maadui?

11. Je, ni kweli kuwa ili kozi ya Ukomandoo iwe imefana inatakiwa kama mlikuwa mmeingia 100 Mafunzoni basi 55 wawe Wamekufa na 25 wawe wamejeruhiwa kwa kuwa Vilema na wengine hata Makolomero yao na Ulimi kujitokeza Mdomoni na 20 tu ndiyo wawe Hai na Kukamilika?

Sasa ni wakati wa nyie Kunijibu tu nijue.
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
3,027
2,000
Tulipokuwa Quba kwenye mafunzo nilipenda wanatuchukulia kama raia wa kawaida hata madem wa kule unapita nao....kurudi sasa yaani ni kero ukitaka kujichanganya na wana wa kijiweni kidogo simu isha ingia ni kero sana, ulinzi ulinz ulinzi hata ukitaka kuendesha bila leseni unatumia kitambulisho au gwanda, kuna siku nilikula bure kwenye mgahawa mmoja wa kishua jijini hapo. Walivyoita mabaunsa nikatoa gamba wakanyong'onyea kama kuku wa mdondo.Ni kweli kuna siku niliamkiwa na dc halafu mimi ni janja tu sijagonga hata 30 nikaamkiwa na zee zima.
 

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,109
2,000
Dar es salaam kuna watu million 6 na zaidi wote wanaweza kutulizwa na Makomandoo 5 mpaka 7 tuu 😅😅😅
Ninavyosikia kwa hawa Jamaa linawezekana Ndugu yangu. Ngoja waje wenyewe wakuthibitishie ni kwanini si tu linawezekana bali pia kwa aina ya Mafunzo yao ya hali ya juu kabisa ni rahisi pia.
 

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,109
2,000
Tulipokuwa Quba kwenye mafunzo nilipenda wanatuchukulia kama raia wa kawaida hata madem wa kule unapita nao....kurudi sasa yaani ni kero ukitaka kujichanganya na wana wa kijiweni kidogo simu isha ingia ni kero sana,ulinzi ulinz ulinzi hata ukitaka kuendesha bila leseni unatumia kitambulisho au gwanda,kuna siku nilikula bure kwenye mgahawa mmoja wa kishua jijini hapo...walivyoita mabaunsa nikatoa gamba wakanyong'onyea kama kuku wa mdondo.Ni kweli kuna siku niliamkiwa na dc halafu mimi ni janja tu sijagonga hata 30 nikaamkiwa na zee zima.
Shikamoo Komandoo!
 

mtamba PGO

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
527
1,000
Point 8
emoji736.png

Nyingine
emoji3582.png

Mmoja kati ya nilotoka nao tumbo moja Ni comando hakuna kilichobadirika kwake
Anawaheshimu wazee mtaani
Mambo ya kuripoti eti nani ajue yupo hakuna.
Amebadirisha mind set yangu kuwahusu Hawa watu
 

Zero zone

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
1,463
2,000
Tulipokuwa Quba kwenye mafunzo nilipenda wanatuchukulia kama raia wa kawaida hata madem wa kule unapita nao....kurudi sasa yaani ni kero ukitaka kujichanganya na wana wa kijiweni kidogo simu isha ingia ni kero sana,ulinzi ulinz ulinzi hata ukitaka kuendesha bila leseni unatumia kitambulisho au gwanda,kuna siku nilikula bure kwenye mgahawa mmoja wa kishua jijini hapo...walivyoita mabaunsa nikatoa gamba wakanyong'onyea kama kuku wa mdondo.Ni kweli kuna siku niliamkiwa na dc halafu mimi ni janja tu sijagonga hata 30 nikaamkiwa na zee zima.
Niambie Komandoo
 

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,109
2,000
Point 8
Nyingine
Mmoja kati ya nilotoka nao tumbo moja Ni comando hakuna kilichobadirika kwake
Anawaheshimu wazee mtaani
Mambo ya kuripoti eti nani ajue yupo hakuna.
Amebadirisha mind set yangu kuwahusu Hawa watu


Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Kafanyia Mafunzo yake Morogoro tu pekee au alienda mpaka Cuba na Israel kwa Makomandoo wa uhakika na waliokamilika Kimedani na ambao ndiyo nawaongelea sana hapa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom