Kwa wale wataalam wa kiswahil naomben mawazo ya hili

stan b

Member
Sep 8, 2011
85
10
niambieni mzizi wa neno ' ALIYETAPISHA' Mi nimkal lkn hil limenishinda, haya karibun kwa majib
 
klf

Member
Jun 12, 2009
58
11
Kwenye kamusi mbalimbali, kutapisha mzizi wake ndio "tapika". Kama kamusi isemavyo kutapisha hutumiwa kueleza tendo la kufanya mtu atapike yaani kutoa kitu tumboni kwa kupitia mdomoni. Kuna maana nyingine pia - kurejea mafundisho wapewayo wari jandoni au unyagoni.
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,581
5,338
nadhani sio kiswahili kizuri na ndio maana tunashindwa kukielewa. ila moseley katoa mwangaza mzuri
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
659
289
niambieni mzizi wa neno ' ALIYETAPISHA' Mi nimkal lkn hil limenishinda, haya karibun kwa majib
Neno hilo lina makosa kisarufi lilipaswa liwe 'aliyetapikisha' kuna mazoea ya kufanya udondoshaji kwa makosa kwa kutoa 'k' hapo mzizi ni -tapik- ndio maana tunapata tapik-a, tapik-i-a, tapik-i-an-a halikadhalika tapik-ish-a. Hapo kwanza. Sarufi ni sayansi haina ukali.
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,704
3,235
Neno hilo lina makosa kisarufi lilipaswa liwe 'aliyetapikisha' kuna mazoea ya kufanya udondoshaji kwa makosa kwa kutoa 'k' hapo mzizi ni -tapik- ndio maana tunapata tapik-a, tapik-i-a, tapik-i-an-a halikadhalika tapik-ish-a. Hapo kwanza. Sarufi ni sayansi haina ukali.

KAMA mzizi ni -tapik-, vipi kuhusu neno matapishi, nako kuna udondoshaji?
 
gmcmp

New Member
Oct 11, 2011
1
0
tapikisha na neno matapishi n maneno mawili tofauti neno tapikisha n kitenzi na neno matapishi n nomino kwahiyo huo ndio utofauti wake ndugu
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
659
289
KAMA mzizi ni -tapik-, vipi kuhusu neno matapishi, nako kuna udondoshaji?

Naona tatizo hapo lipo kwenye udondoshaji na uchopekaji. Pia asili ya neno inaweza kuchangia kuongeza ukakasi. Ngoja tuendelee kulifanyia kazi.
 
kingtuma

Member
Jan 15, 2011
88
10
Kwa kawaida neno huweza kubadili mofolojia linapohama kategoria mf toka kauli ya kutenda kuwa kutendesha. Kwa neno "tapisha" mzizi ni -tapish- ikumbukwe vitenzi vingi vyenye asili ya kibantu huishia na irabu -a- ktk kitenzi halisi na
ukiondoa hiyo -a-unapata mzizi
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,581
5,338
Kwa kawaida neno huweza kubadili mofolojia linapohama kategoria mf toka kauli ya kutenda kuwa kutendesha. Kwa neno "tapisha" mzizi ni -tapish- ikumbukwe vitenzi vingi vyenye asili ya kibantu huishia na irabu -a- ktk kitenzi halisi na
ukiondoa hiyo -a-unapata mzizi
tafadhali toa mfano tukuelewe vizuri point yako...
 
Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
659
289
Kwa kawaida neno huweza kubadili mofolojia linapohama kategoria mf toka kauli ya kutenda kuwa kutendesha. Kwa neno "tapisha" mzizi ni -tapish- ikumbukwe vitenzi vingi vyenye asili ya kibantu huishia na irabu -a- ktk kitenzi halisi na
ukiondoa hiyo -a-unapata mzizi

Neno hata likihama kategoria nyingine mzizi huwa haubadiliki, vitakavyobadilika ni viambishi vilivyochopekwa. Hivyo kama nilivyosema awali ukilichunguza hilo neno utagundua kuwa mzizi ulipaswa uwe tapik- ila sasa watumiaji ufanya udodondoshaji. Udondoshaji wenyewe utokana na dhana ya akilini kuwa K- ni kauli ya kutenda na ish ni kutendesha hvyo anapotaka kuonesha usababishi au utendeshi hudondosha k-. Ikumbukwe kuwa k- ya hapo haiwakilishi kauli za matendo.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom