Kwa wale wasiopenda kujikuta wanafanikisha Infidelity...

Nachukia wazo la watu kutoka nje ya ndoa zao kama ambavyo nachukia wazo la watu kuingilia ndoa za wengine. Siku zote anaetoka nje ya ndoa yake anastahili lawama, ila sio wote wanaotoka nao wanastahili lawama kwasababu wengine hua hawafahamu kwamba wanaetoka nao ni waume/wake za watu.

Wapo watu ambao hawako interested kutembea na wake/waume za watu ila wanadondoka kwenye mitego ya "niko single, mume/mke wangu amefariki, nimekupenda nataka tuoane" n.k bila kujua.

Kwahiyo nimeona tushee vitu ambavyo mtu anaweza kutumia kugundua kama Mr/Miss Perfect wake mpya ni Mr/Mrs Cheater. Japo sio guarantee, inaweza ikasaidia kwa kiasi chake.

1. Hapokei simu usiku, hajibu msg au anazima kabisa huku akiwa na visingizio lukuki kwanini anafanya hivyo - huu ni muda ambao anakua na familia yake.
2. Mipango yenu sio ya muda mrefu -hivyo lazima kila anachopanga kiendane na ratiba ya nyumbani kwake hivyo anakua mwangalifu kutogonganisha ahadi zenu na mipango ya nyumbani.
3. Hawezi kutumia usiku mzima na wewe, akijitahidi sana anaweza akaiba siku mbili tatu kwa mke/mume wake kwa kudanganyia safari za kikazi ila haiwezi tokea kila mara.
4. Hawezi kutumia usiku mzima na wewe baada ya kumshtukiza kwamba unataka a'spend the night' - anapanga mwenyewe ili awe ameshaandaa mazingira kwa mke/mume wake.
5. Mara nyingi akikupigia simu yuko sehemu ambazo ni public - huko ndiko anapopata uhuru wa kuongea na wewe kwa uwazi.
6. Hakukaribishi kwake, anaweza akakwambia anaishi na mtu. . rafiki/ndugu anaemheshimu sana hivyo hawezi kukukaribisha anapoishi.
7. Anaweza akakutambulisha kwa marafiki zake (wanaomfichia siri) ila sio ndugu zake, especially wale watu wazima.
8. Yeye ndie anaepanga/suggest wapi mkutane ili kuepuka kukutana na watu asiotaka wawaone pamoja.
9. Ukitaka akusindikize sehemu/kwenye function anatafuta visingizio hata kama alishakwambia siku hiyo atakuwepo kwaajili yako na angependa mkutane kama kawaida.
10. Siku za sikukuu anakua 'unavailable' kwako.
11. Wakati mwingine simu yake ikiita anaiignore, akipokea anaomba utulie au anasogea pambeni.
12. Marufuku kufika ofisini kwake coz anajua ofisi inamtambua mkewe.
13. Hapendi ushike simu yake,na huwa mkali sana akikufuma hata kama unamuwekea kwenye charger
14. Wanachagua sana sehemu za kula,kufanya mazungumzo na kupumzika,mara nyingi huenda sehemu zenye watu wachache,nje ya mji au hupenda muonane sehemu zilizo na giza na watu wengi waasipopita au nyumbani kwa mwanamke,na husisitiza au hata kukung'ang'aniza upange mitaa fulani fulani....!!
15. Wengine hupenda mkikutana in public basi awe na rafiki yake wa kiume muwe watatu au zaidi,ili hata kama kuna wa kumuwekea doubts apate wakati mgumu kujua uko na nani hasa pale mtakapokuwa kwa public....halafu kuna wale wanapenda sehemu zinazojaa sana kama club ili iwe ngumu kuwa noticed....
16. Kwenye simu yake kakusave 'fundi ' au jina lako halisi( na si honey mpz darlin)
kwa nini utembee na vitu used?wakati kuna vitu new model grand new?
 
Tatizo ni kwamba hawezi jua nani yupo tayari kuingia vitani na nani hayuko. Ila bado ni ustaarabu(japo kiduuunchu) kumweleza mtu ukweli akikubali ajue kabisa anachokubali.


Orait....thats the way, Lizzy si ndo tukisema(ga) hapa kila siku...lol
 
we smile wewe.....are u brand new? Lol
wanasemaje shem gari inayovutwa haiwezi kuovertake ile inayoivuta.mimi nipo kushoto saaaana na hvi vitu used scraper to me noooooooooo big noooooooooooooo
 
shosti hii sio kujrusha roho? Nimempoteza wang kwa mchezo hu wa kumkagua bata. Cna ham
 
Mtu ukiamua kutokuingia anga za wenye wake/waume ni uamuzi tu
Kama wewe ni mwanamke/msichana unapenda mwanaume mwenye "sifa nzito" - mwonekano bomba, outing za nguvu,mkwanja mzuri.... ujuwe most likely huyu ana mke.Wanaume wengi wenye sifa hizi walishapitia vipindi vya kujiweka sawa na wengi hu settle na mwanamke as a wife. Akisha settle, most probably mambo yake yanatengamaa. Akishajisikia ame settle, anaanza ku play around - WITH YOU.

Kwa kifupi, dalili mojawapo ya mwanaume aliyeoa - mtanashati, ana kauwezo hata kama si kivile,ana some disposable income which he can afford to spend on you.
 
mtu ukiamua kutokuingia anga za wenye wake/waume ni uamuzi tu
kama wewe ni mwanamke/msichana unapenda mwanaume mwenye "sifa nzito" - mwonekano bomba, outing za nguvu,mkwanja mzuri.... Ujuwe most likely huyu ana mke.wanaume wengi wenye sifa hizi walishapitia vipindi vya kujiweka sawa na wengi hu settle na mwanamke as a wife. Akisha settle, most probably mambo yake yanatengamaa. Akishajisikia ame settle, anaanza ku play around - with you.

Kwa kifupi, dalili mojawapo ya mwanaume aliyeoa - mtanashati, ana kauwezo hata kama si kivile,ana some disposable income which he can afford to spend on you.
si kweli? Wanaume wa watu wana hela ila ni hela ya stress mikopo kibao .ada za watoto na ndugu wa mke,mama mkwe mgonjwa weeeeeee
vijana wana hela bwana sema tu ni wabahili.wanaume wa watu wanaona aibu kumnyima mtu hela heri akaibe kwa wife akupe
 
Lizzy, kuna wale ambao wako mbali na familia zao, yaani mpaka kufunga ndoa wanafunga!! Yaani acha kabisa, mtu ambaye si mwaminifu kwa mwenza, ni mbaya mno!!
KH hii niliishuhudia mwezi novemba mwishoni. Mbaba kaacha mke wa ndoa na watoto upareni afu kaja kujifungisha ndoa na kabinti kengine bila ndugu yake hata mmoja kufahamu... Dunia haina siri, mwanamke kapata wa kumng'ata sikio, kajifungasha hajaamini alichokikuta. Fahamu zilimpotea kwa mda. Achana na wanaume walonyimwa uso wa haya jamani.
 
si kweli? Wanaume wa watu wana hela ila ni hela ya stress mikopo kibao .ada za watoto na ndugu wa mke,mama mkwe mgonjwa weeeeeee
vijana wana hela bwana sema tu ni wabahili.wanaume wa watu wanaona aibu kumnyima mtu hela heri akaibe kwa wife akupe
Unajua Smile,
Vijana siyo wabahili kama unavyosema.A single lad, has priorities and goals.
Spending money on a chick may not be his priority,
he would rather have you spend money on him lol.
Mume wa mtu, yeye anataka akupate kwa njia yoyote, abadili mboga lol kwa gharama.
Figure that out.
 
Unajua Smile,
Vijana siyo wabahili kama unavyosema.A single lad, has priorities and goals.
Spending money on a chick may not be his priority,
he would rather have you spend money on him lol.
Mume wa mtu, yeye anataka akupate kwa njia yoyote, abadili mboga lol kwa gharama.
Figure that out.

Kwa hiyo waume wa watu ni bora kiuwekezaji.
 
unajua smile,
vijana siyo wabahili kama unavyosema.a single lad, has priorities and goals.
spending money on a chick may not be his priority,
he would rather have you spend money on him lol.
Mume wa mtu, yeye anataka akupate kwa njia yoyote, abadili mboga lol kwa gharama.
Figure that out.
dah ni kweli.ila all in all mi vitu used situmii kabisa so sina expirience nao kiviiile kama lizy
 
dah ni kweli.ila all in all mi vitu used situmii kabisa so sina expirience nao kiviiile kama lizy


Huwezijua kama kitu ni used kama wewe unapenda mkwanja lol
Vitu used, vinajua kuhonga....Unapenda gifts weye?
 
Back
Top Bottom