Kwa wale wasiopenda kujikuta wanafanikisha Infidelity...

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,778
59,133
Nachukia wazo la watu kutoka nje ya ndoa zao kama ambavyo nachukia wazo la watu kuingilia ndoa za wengine. Siku zote anaetoka nje ya ndoa yake anastahili lawama, ila sio wote wanaotoka nao wanastahili lawama kwasababu wengine hua hawafahamu kwamba wanaetoka nao ni waume/wake za watu.

Wapo watu ambao hawako interested kutembea na wake/waume za watu ila wanadondoka kwenye mitego ya "niko single, mume/mke wangu amefariki, nimekupenda nataka tuoane" n.k bila kujua.

Kwahiyo nimeona tushee vitu ambavyo mtu anaweza kutumia kugundua kama Mr/Miss Perfect wake mpya ni Mr/Mrs Cheater. Japo sio guarantee, inaweza ikasaidia kwa kiasi chake.

1. Hapokei simu usiku, hajibu msg au anazima kabisa huku akiwa na visingizio lukuki kwanini anafanya hivyo - huu ni muda ambao anakua na familia yake.
2. Mipango yenu sio ya muda mrefu -hivyo lazima kila anachopanga kiendane na ratiba ya nyumbani kwake hivyo anakua mwangalifu kutogonganisha ahadi zenu na mipango ya nyumbani.
3. Hawezi kutumia usiku mzima na wewe, akijitahidi sana anaweza akaiba siku mbili tatu kwa mke/mume wake kwa kudanganyia safari za kikazi ila haiwezi tokea kila mara.
4. Hawezi kutumia usiku mzima na wewe baada ya kumshtukiza kwamba unataka a'spend the night' - anapanga mwenyewe ili awe ameshaandaa mazingira kwa mke/mume wake.
5. Mara nyingi akikupigia simu yuko sehemu ambazo ni public - huko ndiko anapopata uhuru wa kuongea na wewe kwa uwazi.
6. Hakukaribishi kwake, anaweza akakwambia anaishi na mtu. . rafiki/ndugu anaemheshimu sana hivyo hawezi kukukaribisha anapoishi.
7. Anaweza akakutambulisha kwa marafiki zake (wanaomfichia siri) ila sio ndugu zake, especially wale watu wazima.
8. Yeye ndie anaepanga/suggest wapi mkutane ili kuepuka kukutana na watu asiotaka wawaone pamoja.
9. Ukitaka akusindikize sehemu/kwenye function anatafuta visingizio hata kama alishakwambia siku hiyo atakuwepo kwaajili yako na angependa mkutane kama kawaida.
10. Siku za sikukuu anakua 'unavailable' kwako.
11. Wakati mwingine simu yake ikiita anaiignore, akipokea anaomba utulie au anasogea pambeni.
12. Marufuku kufika ofisini kwake coz anajua ofisi inamtambua mkewe.
13. Hapendi ushike simu yake,na huwa mkali sana akikufuma hata kama unamuwekea kwenye charger
14. Wanachagua sana sehemu za kula,kufanya mazungumzo na kupumzika,mara nyingi huenda sehemu zenye watu wachache,nje ya mji au hupenda muonane sehemu zilizo na giza na watu wengi waasipopita au nyumbani kwa mwanamke,na husisitiza au hata kukung'ang'aniza upange mitaa fulani fulani....!!
15. Wengine hupenda mkikutana in public basi awe na rafiki yake wa kiume muwe watatu au zaidi,ili hata kama kuna wa kumuwekea doubts apate wakati mgumu kujua uko na nani hasa pale mtakapokuwa kwa public....halafu kuna wale wanapenda sehemu zinazojaa sana kama club ili iwe ngumu kuwa noticed....
16. Kwenye simu yake kakusave 'fundi ' au jina lako halisi( na si honey mpz darlin)
 
12. Marufuku kufika ofisini kwake coz anajua ofisi inamtambua mkewe.
13. Hapendi ushike simu yake,na huwa mkali sana akikufuma hata kama unamuwekea kwenye charger
 
12. Marufuku kufika ofisini kwake coz anajua ofisi inamtambua mkewe.
13. Hapendi ushike simu yake,na huwa mkali sana akikufuma hata kama unamuwekea kwenye charger

Ukiona mtu anawaka hata ukiiweka simu yake kwenye chaja ujue kuna kitu anaficha huyo
 
12. Marufuku kufika ofisini kwake coz anajua ofisi inamtambua mkewe.
13. Hapendi ushike simu yake,na huwa mkali sana akikufuma hata kama unamuwekea kwenye charger

Hahahaha. . . Namba 13 inachekesha.
Ntaziongeza pale juu kama hutojali. . . nasubiria ruhusa.
 
kumbe cheaters wana akili sana ya kukwepa viunzi eeh; very well-thought out strategy...
 
Ukiona mtu anawaka hata ukiiweka simu yake kwenye chaja ujue kuna kitu anaficha huyo

Tena kitu chenyewe si kidogo,ukisema ukifuatilie lazima utapata presha,BP,Oilcom,LakeOil,Bigbon..zooote..
 
wanachagua sana sehemu za kula,kufanya mazungumzo na kupumzika,mara nyingi huenda sehemu zenye watu wachache,nje ya mji au hupenda muonane sehemu zilizo na giza na watu wengi waasipopita au nyumbani kwa mwanamke,na husisitiza au hata kukung'ang'aniza upange mitaa fulani fulani....!!

Wengine hupenda mkikutana in public basi awe na rafiki yake wa kiume muwe watatu au zaidi,ili hata kama kuna wa kumuwekea doubts apate wakati mgumu kujua uko na nani hasa pale mtakapokuwa kwa public....halafu kuna wale wanapenda sehemu zinazojaa sana kama club ili iwe ngumu kuwa noticed....to be continued....bastards!!
 
Lizzy, kuna wale ambao wako mbali na familia zao, yaani mpaka kufunga ndoa wanafunga!! Yaani acha kabisa, mtu ambaye si mwaminifu kwa mwenza, ni mbaya mno!!

Yaani ni wabaya mno,ila hii dunia ina wanaume wakatili jamani...lol,halioni hata tabu kwenda kwa wazazi na ndugu wa mtu....na ukikuta kwao ndo mfalme mdogo basi hata hakuna nduguye wa kukuambia...kweli bila hekima na uwezo wa ki-Mungu wa kusamehe kuna watu wangechemshwa na kuliwa hai....!!
 
mhhhhh.....poleni sana.......

kwani si bora mtu useme tu nina mtu....ili ratiba iwe rahisi????

Si kila mtu anakubali kuwa OPTION, wanaume wanajua kabla ya kutongoza kuwa possibility ya kumpata mwanamke unayemuhitaji ambaye hafanyi biashara ni ndogo kama ukimpa ukweli huo...just curious...unawaambiaga kwamba umeoa?....lol:washing:
 
Yaani ni wabaya mno,ila hii dunia ina wanaume wakatili jamani...lol,halioni hata tabu kwenda kwa wazazi na ndugu wa mtu....na ukikuta kwao ndo mfalme mdogo basi hata hakuna nduguye wa kukuambia...kweli bila hekima na uwezo wa ki-Mungu wa kusamehe kuna watu wangechemshwa na kuliwa hai....!!

Yaani dear acha tu! Kuna binti alifunga ndoa, kumbe jamaa ana mke na watoto mkoa mwingine!
 
wanachagua sana sehemu za kula,kufanya mazungumzo na kupumzika,mara nyingi huenda sehemu zenye watu wachache,nje ya mji au hupenda muonane sehemu zilizo na giza na watu wengi waasipopita au nyumbani kwa mwanamke,na husisitiza au hata kukung'ang'aniza upange mitaa fulani fulani....!!

Wengine hupenda mkikutana in public basi awe na rafiki yake wa kiume muwe watatu au zaidi,ili hata kama kuna wa kumuwekea doubts apate wakati mgumu kujua uko na nani hasa pale mtakapokuwa kwa public....halafu kuna wale wanapenda sehemu zinazojaa sana kama club ili iwe ngumu kuwa noticed....to be continued....bastards!!

Hahahaa. . . Punguza munkari dearest.Ila kweli wanaboa sana. . . wote wake kwa waume. Hapo kwenye list hata sina cha kuongeza maana zimejitosheleza. . . ntachakachua kidogo niziweke ubaoni.
 
Kwanini tusijadili kuzuia ngono kabla ya ndoa?Kwani haiwezekani?
 
Lizzy, kuna wale ambao wako mbali na familia zao, yaani mpaka kufunga ndoa wanafunga!! Yaani acha kabisa, mtu ambaye si mwaminifu kwa mwenza, ni mbaya mno!!

KH hao ni wabaya zaidi maana wanakua hawana mipaka wala viashiria vya kwamba kuna mwingine. Hata kukaa kwake wiki anakukaribisha, ndoa unaahidiwa/unakubaliwa na kuamishwa unaaminishwa kwamba sio usanii. Kuna dada alienda kusoma nje akaolewa huko na nyumbani kaacha mume. Balaa tupu.
 
Back
Top Bottom