Kwa wale wapenzi wa Video Games

EGF

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
387
979
Habari wanajukwaa, Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu Kati ya FIFA na PES ni lipi gemu Bora kushinda lingine. Ningependa niulete mjadala huu kwenu wanajamii forum tujadiri hapa Kati ya FIFA na PES lipi ni Bora kushinda jengine...
images%20(22).jpeg
images%20(21).jpeg
 
fifa la mafundi ila pes la beginners so kila mwamba ngoma........
all in all Fifa is the best
movements......graphics..likeness....gameplay
na linazidi kunoga kila uchwao
 
Naipenda fifa sababu kila kitu ni realistic kabisa...
Commentators hawana mbwembwe hasa ufungaji gori
Pes ni ya watoto wa shule tuwaachie
 
Binafsi naipenda PES kwa sababu movement ya mchezaji inaendana kabisa na uhalisia wa mchezaji mwenyewe FIFA hiko kitu hakuna, Celebration ya wachezaji kwenye PES ni nzuri kuliko FIFA kingine kikubwa zaidi ni muonekano wa wachezaji kwenye PES kwa kumwangalia tu mchezaji unamtambua kirahisi kuliko mchezaji wa kwenye FIFA kumtambua wakati akiwa kwenye movement sio rahisi.
 
Mpaka unakuja kulinganisha FIFA NA PES,ni dhahiri ya kwamba haya magemu hujayacheza yote ukajifanyia mizania.
Ni sawa na kuja kuuliza SOMALIA NA UFARANSA wapi pameendelea....
 
Mpaka unakuja kulinganisha FIFA NA PES,ni dhahiri ya kwamba haya magemu hujayacheza yote ukajifanyia mizania.
Ni sawa na kuja kuuliza SOMALIA NA UFARANSA wapi pameendelea....
Nakili nilianza kucheza PES Ila nilishawishiwa nijaribu na FIFA kua ni zuri kuliko PES kwakweli sikutokea kulipenda ila nilichogundua watu wengi wanaocheza FIFA pia wanaweza kucheza PES Ila wanaocheza PES wengi hawawezi FIFA kwa tafsiri nyepesi ni kwamba PES ni Bora kuliko FIFA sema tu ni vile Fifa ina license za kutosha na linapewa promo kubwa Sana ...
 
Back
Top Bottom