Kwa wale wapenzi wa matangazo ya TV na Radio, tangazo lipi unalipenda?

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,267
2,000
Kwenye TVs na radio hakuna muda napenda kama ule wa matangazo kama ni mpira au taarifa huwa nasubiria ipite nisikie/nione matangazo hasa yale yenye ubunifu.

Mpenzi wa matangazo weka lililowahi kufurahisha tuenjoy hapa.

Nitaanza na yangu penye masahihisho tusahihishane maana kukariri tangazo lote sio kitoto.

CRDB
Mzee: eeeh kijana ebu tuambie umejiandaandaaje kumchukua binti yetu.

mzee: una Nyumba kijana?
Kijana: ndiyo mzee
Mzee: Unagari?
Kijana: ndiyo E-Gx 100
mzee: una tembo mastercard?
Kijana: mmh hiyo mzeee
Mzee: hmmm kijana unataka kumchukua binti yetu kwenye dunia hii hauna tembo mastercard???
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,267
2,000
Kuna lile la dawa tatu kombe la dunia 2006 kuna watu lilikuwa linawakera ila mimi nililipenda hatari.

Je una maumivu ya flu?, je una maumivu ya mgongo? je una maumivu ya kichwa?

Mimi natumia dawa tatu wewe je?Tumia dawa tatu. Kale kadada kanajigeuzageuza tu.
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
17,531
2,000
Kama kawaida ya Kasie kupenda kucheka mizaha na masihara. Mie nililipenda tangazo la ivory cocoa alilotangaza mzee majuto hasa pale bukta inapokuwa inadondoka hahahahahahaa.

Matangazo ya vichekesho kwangu nayapenda.

Kasie Dadiiiiii.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,267
2,000
Kama kawaida ya Kasie kupenda kucheka mizaha na masihara. Mie nililipenda tangazo la ivory cocoa alilotangaza mzee majuto hasa pale bukta inapokuwa inadondoka hahahahahahaa.

Matangazo ya vichekesho kwangu nayapenda.

Kasie Dadiiiiii.
hili tangazo ni nooma.. kuna lile pia kalifanya la LAPF kastaafu Kala mafao kajenga nyumba katulia na mke wake kaja rafiki yake ambaye alikuwa kwenye mfuko tofauti eti anatafuta kazi.

Alimwekea vyomboo vingiii kisha akamwambia unashangaa nini mimi nipo na my wife ndani tunapeana marahaa hahah.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,267
2,000
Daby leo umekunywa kinywaji gan? maana nimeishia kucheka tu dah
Mbiti napenda jokes na mizaha saana.

Sasa kuna mtu anajua napenda matangazo kanitumia Tangazo moja la malaria.

mtoto anamuuliza babake.

mtoto: baba nataka kuwa dereva wa ndege.
Baba: unamaana unataka kuwa Rubani?
Mtoto: ndiyo ndege inapaaje angani

Baba: he he he he mwanangu hayo ni mambo ya kitaalamu saana.

Mzee kilaza saana kashangaaa saan. Eti he he he hahaha
 

MBITIYAZA

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
15,046
2,000
Mbiti napenda jokes na mizaha saana.

Sasa kuna mtu anajua napenda matangazo kanitumia Tangazo moja la malaria.

mtoto anamuuliza babake.

mtoto: baba ndege inapaaje angani
Baba: he he he he mwanangu hayo ni mambo ya kitaalamu saana.

Mzee kilaza saana kashangaaa saan. Eti he he he


ahhhhhhhhh leo nakiri rasmi NIMEZEEKA! yaan najitahd kukuelewa SIKUELEWI kipi kinakuvutia kupitia matangazo !lol
 

Wahli

Senior Member
May 30, 2017
111
225
Aseeh kuna lile tangazo la kiwi miaka ya tisin napenda pale jamaa anaposema
Hebu jitokeze simama mbele za watu alafu alfajir kwenye kipindi cha kombora radio Tanzania
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,267
2,000
The Namba one Tangazo for me ni Vodacom Pindua Pindua
Sijaliskia nirushie basi.

Kuna lile pia nadhani ni la airtel pia. Nikikaa na klaree muda wote anakuambia ninyoe staili fulani hivi kama mshikaji nipige paaap paap..

Kama walivyokuwa wanafanya wale jamaa kwenye tangazom
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,267
2,000
Kuna matangazo ya eazypesa yalikuwa yanarushwa eastafrica radio ya mmasai anaitwa lomayan na jamaa yake oswald yalikuwa yananichekesha hatari...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom