Kwa wale wapenzi wa hard core hip hop(rap) za USA za miaka ya 1989-2000's, karibuni

lbaraka

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
393
248
Habarini wadau,

Mimi ni mpenzi na mfuatiliaji sana wa ngoma za kitambo mziki ulipoitwa mziki. Muziki wenyewe nnauongelea hapa ni zile ngoma nyeusi, kubum kubam za mbele za miaka ya 1988 mpaka miaka ya mwanzoni mwa 2000 kabla ya commercial, trap na mainstream hawajakichafua.

Miaka hiyo artists walikuwa na umoja sana na walifanya kazi kwa crews zaid kuliko solo. Crews kama akina Public Enemy, Lord of Underground, The Roots, Black Star, Lost Boyz, Onyx bila kusahau West Coast Connection zilibamba sana.

Kwanza beats zao zamani zilikuwa zina rythm na kick nzito na quality ya juu ukifananisha na za sasa. Madjs na producers wa kipindi kile walikuwa wanafanya mastering ya kiwango kikubwa sana.

Hebu kwa wale malegendary wa miaka hiyo mje sasa mfuguke, haswa ni crews zipi ziliwabamba na ngoma zao pia karibuni
 
Back
Top Bottom