kwa wale wapenzi na mashabiki wa yanga

astranaut

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,276
1,021
Wana yanga wenzangu wenye mapenzi mema na hii team mimi kwa upande wangu aina ya mpira anao ucheza yanga siulewi mimi kwa upande wangu nashindwa kuelewa kama ni mfumo mbovu au tatizo ni nini.

Kwa sababu hata kama ni mpira wa kaunta attack si kwa staili hiyo mpira hata hauna burudani ni kubutua tu,kuparamiana n.k utafikili ni soka la mchangani.

Je,tatizo ni wachezaji wenyewe wanashindwa kumuelewa kocha au tatizo ni kocha mwenyewe na aina ya ufundishaji? Hivi kweli kwa soka hilo naloliona huko club bingwa africa si asubuhi tu yanga atolewa.

Kimsingi mwinyi zahera kajitahidi kuleta nidhamu ya wachezaji lakini sasa kwa aina ya mpira anao ufundisha simuelewi
 
Kitu tayari hichoooo Yanga 1 - 1 Malindi.

Hii Yanga inatia huruma aiseee.Yule baunsa Molinga ndo hovyo kuliko wote,Wabrazil wetu wana nafuu sana.
 
Wana yanga wenzangu wenye mapenzi mema na hii team mimi kwa upande wangu aina ya mpira anao ucheza yanga siulewi mimi kwa upande wangu nashindwa kuelewa kama ni mfumo mbovu au tatizo ni nini.

Kwa sababu hata kama ni mpira wa kaunta attack si kwa staili hiyo mpira hata hauna burudani ni kubutua tu,kuparamiana n.k utafikili ni soka la mchangani.

Je,tatizo ni wachezaji wenyewe wanashindwa kumuelewa kocha au tatizo ni kocha mwenyewe na aina ya ufundishaji? Hivi kweli kwa soka hilo naloliona huko club bingwa africa si asubuhi tu yanga atolewa.

Kimsingi mwinyi zahera kajitahidi kuleta nidhamu ya wachezaji lakini sasa kwa aina ya mpira anao ufundisha simuelewi
Mechi na Kariobangi Shark FC walicheza vizuri ila mechi na Mlandege walicheza vizuri kipindi cha kwanza wale wachezaji waliopo kikosi cha kwanza. Walioingia kipindi cha pili walicheza hovyo sana. Ingawa inaonekana wakipata muunganiko itakuwa timu nzuri tu.
 
Ukitaka uone mpira wa Yanga mtamu usiangalie mpira wa Simba , ukiangalia soka ya Simba hata Yanga wajitahidi hivi hutawaelewa.Soka LA kitabuni ni tamaduni ya club au nchi, Yanga haijawahi kuwa na utamaduni wa soka LA kuvutia labda wakati wa Tambwe Leya na team ya wale vijana wadogo
 
Tatizo timu za Simba na Yanga zinasajili wachezaji wengi na kuacha wengi. Na msimu huu kulikuwa mashindano mengi kwa hiyo muda wa pre- season ulikuwa mdogo na ratiba za caf zimebadilika.
Simba nayo ina wachezaji wageni wengi muunganiko utachukua muda na vile vile kwa Yanga. Sijui tatizo la vilabu hizi nini hassa.
Yanga walihitaji kuwabakisha wachezaji kadhaa kama makambo, ajib na kuongeza kama wanne tu hassa kiungo, goal keeper na forward.
Simba walihitaji zaidi safu ya ulinzi kama watatu au wawili na winga mshambuliaji mmoja na kuwabakisha akina okwi na kotei.
Sasa kundi loote hili itachukua muda.
Mfano kiungo Simba wana Mzamiru yassin.Ndemla,Mkude,kahata,Shiboul, hassan dilunga,Ajib na Chama hebu tazama hapo ... na beki wamesajili mbrazil hajui mpira wa Afrika ni kubahatisha beki za kati Wawa dhaifu mipira ya juu hili tatizo. Sasa hapo viungo karibia 11.
Yanga Ngassa wa nini ? Goal keeper bora bado winga hamna.
Sioni wote kufika mbali japo kidogo baada ya muda Simba huenda ikafanya vyema tena labda kwenye ligi kuu.
 
Dah mara kibao tu bado timu moja hafu dk za sabini inalamba kadi nyekundu wanaanza kutafuta sare badala ya ushindi
 
Ukitaka uone mpira wa Yanga mtamu usiangalie mpira wa Simba , ukiangalia soka ya Simba hata Yanga wajitahidi hivi hutawaelewa.Soka LA kitabuni ni tamaduni ya club au nchi, Yanga haijawahi kuwa na utamaduni wa soka LA kuvutia labda wakati wa Tambwe Leya na team ya wale vijana wadogo
Sio kweli yanga ya maxmo ilikua na mpira wa pasi mzuri tu but baada ya hapo makocha wote wanaokuja wanataka pasi kidogo golini kama mpira wa man u,liverpool,spurs,n.k lakini cha kushangaza nao hawawezi
 
Wana yanga wenzangu wenye mapenzi mema na hii team mimi kwa upande wangu aina ya mpira anao ucheza yanga siulewi mimi kwa upande wangu nashindwa kuelewa kama ni mfumo mbovu au tatizo ni nini.

Kwa sababu hata kama ni mpira wa kaunta attack si kwa staili hiyo mpira hata hauna burudani ni kubutua tu,kuparamiana n.k utafikili ni soka la mchangani.

Je,tatizo ni wachezaji wenyewe wanashindwa kumuelewa kocha au tatizo ni kocha mwenyewe na aina ya ufundishaji? Hivi kweli kwa soka hilo naloliona huko club bingwa africa si asubuhi tu yanga atolewa.

Kimsingi mwinyi zahera kajitahidi kuleta nidhamu ya wachezaji lakini sasa kwa aina ya mpira anao ufundisha simuelewi
French football...haina madoido ndio maana France walichukua WC..angalia AFCON timu zilizocheza fainal ni koloni la France
 
Vuteni subira watan mtapata muunganiko tu
Yani kapindi chote cha maandalizi ya msimu team haijapata muunganiko unategemea ikapatie muunganiko kwenye club bingwa.Huo si utani msimu ujao viongozi wasitutanie na kama ikibainika tatizo ni kocha basi afukuzwe tu mambo ya kusajili kwamazoea huku hela zikiishia kwenye matumbo ya watu haikubaliki lazima tubadilike zama zimebadilika
 
Uko sahini.Na makocha wanaopata mafunzo kwa kifaransa pia wanakuwa wataalam e.g Aliyekuwa Uganda Desabre,Kenya (Migne),Zahera.Ndairagije,Herve Renard,Wenger,juzi kocha wa Madagascar Nicolas Dupuis......nk. nk
French football...haina madoido ndio maana France walichukua WC..angalia AFCON timu zilizocheza fainal ni koloni la France
 
Huwezi kuihukumu timu kwa ile sare ya jana. Ile mechi iliwanufaisha zaidi Malindi na siyo Yanga! Wachezaji karibia wote wa kikosi cha kwanza wa Yanga hawakucheza kwa kuhofia mechi ya kesho. Hata lile goli la kusawazisha walilofungwa dk za nyongeza, utaona kabisa ni goli halali la Yanga ya msimu uliopita wa akina Kabwili na kaka yake Kindoki na siyo hii ya akina Shikaro.

Sema tu kocha hawezi kukwepa lawama baada ya yeye mwenyewe kuchelewa kurudi kuiandaa timu huku akitambua kikosi chake ni kipya. Na pia kukataa kushiriki mashindano ya cecafa pia haikuisaidia timu bila shaka.
 
David Molinga kwa kweli anatia shaka sana, anyway tumpe muda tuone
 
Mpira magoli..wakuvutia kacheze play station..uliona Taifa stars walivyopata tabu kwa Senegal na Algeria..watu wanapress tu hakuna udambwi
Algeria hawana udambwi dambwi ama senegal... Ila unachezwa mpira unao eleweka
 
Back
Top Bottom