Kwa wale wapenda kihispaniola tubonge kidogo

Mimi ndio najifunza kwa kutumia app ya duolingo iko poa kwa kihispaniola

Mimi pia nilianzia hpo na duolingo,tafuta vitabu sasa usome kwa undani zaidi.
Usa unos libros para aprender mas.Duo lingo no es lo suficiente.
 
Nashangaa kidogo hii inahusu nini.
Kichwa kinasema "lugha ya Kihispaniola"- hakuna lugha ya Kihispaniola kwa sababu

1. Hispaniola ni kisiwa kikubwa katika Bahari Karibi ambako kuna lugha mbalimbali si lugha moja. Kisiwani kuna nchi huru mbili: Haiti upande wa magharibi na Jamhuri ya Dominika upande wa mashariki. Haiti wanatumia Kifaransa na Kikreoli, Jamhuri ya Dominika wanatumia Kihispania-

2. Kuna nchi ya Hispania (katika Ulaya) na lugha yake ni Kishispania. Lugha anayotumia "Hola mis amigos" inafanana kidogo na Kihispania lakini mwenzetu haonekani anajua lugha hii. Maana akitaka kusema "Habari rafiki zangu" hii ni "Hola amigos mios", si "mis amigos".

3. Tena "Como estas?" ni namna ya kusema "Hujambo", yaani kuuliza kuhusu mtu mmoja. Lakini alianza sentensi kwa kusalimu watu wengi. HApa anapaswa kutumia ama "estais" (kama ni marafiki wa karibu) au "estan" kama hawako karibu sana maana hapa ni afadhali kutumia umbo la kiungwana zaidi.

Sasa mwezetu ameleta hapa lugha ambyo si Kishispania kweli, na hakika si Kihispaniola . Lugha mpya?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom