Kwa wale wanaotaka kuwa Wahasibu bila kupitia advance (a-level)

chikuyu

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
277
179
NJIA RAHISI YA KUWA MHASIBU BILA KUZUNGUKIA ADVANCED LEVEL.

Nimeona watu wengi sana wanaulizia hii Kitu. Nikaona nidadavue kidogo ili wapate uelewa..
Endelea Kusoma hapa: KWA WATAKAOHITAJI kujua zaidi kuhusu ACCA, nitaandika tena siku nyingine...

Kwa wale ambao wamemaliza Kidato Cha nne au Cha sita na wanataka kusomea Uhasibu.. Kuna njia rahisi Kabisaa ya kuwawezesha kufika Chuo Kikuu na Kusoma Degree ya Uhasibu bila ya kuzunguka kupitia A-Level miaka miwili..

Yaani Ukimaliza tu Form Four unasoma ATEC I mitihani minne tu.. Then unafanya ATEC II mitihani minne pia.. Ukiwa vizuri kichwani ndani ya mwaka mmoja unamaliza hii mitihani.. unapata Cheti Chako cha Accounting Technician II..

Hicho Cheti kinakupa equivalent qualifications za kuingia Degree ya Uhasibu maana ndo Cheti kinaitwa Full Technician Certificate (FTC) huko TCU.. So unaingia chuoni Kabisaa bila mashaka ndani ya mwaka mmoja baada ya kumaliza kidato Cha nne...

Kwa Nini uhangaike kusoma vitu ambavyo Ni irrelevant advance Kwenye fani ya Uhasibu Wakati mpango wako Ni kuwa muhasibu!!?? Usihangaike... Fupisha njia tena gharama ni nafuu tu. Ukiwa serious hayo masomo ni ya kufaulu ndani ya Mwaka mmoja..
Utaratibu Uko Hivi….

Qualifications za Kuingia Accounting Technician (ATEC I)
Mtahiniwa mtarajiwa anayetaka kujisajili kwa ajili ya mitihani ya Accounting Technician Level 1 ni lazima aoneshe uthibitisho wa kuwa na moja wapo ya sifa zifuatazo:

1. Cheti cha mtihani wa elimu ya Sekondari (CSEE) chenye angalau ufaulu wa crediti tatu na kufaulu Hisabati na Lugha ya Kiingereza (Yaani apate C3 kwa masomo yoyote, Lakini Hesabu na Kiingereza awe amepata angalau alama D)

AU

2. Mitihani ya Taifa ya Biashara NABE Stage II na angalau ufaulu wa masomo manne (4) na cheti cha elimu ya Sekondari
AU
3. Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) yenye angalau ufaulu wa primary katika somo moja na subsidiary katika masomo yanayohusika, lakini ni lazima wafaulu (i.e wawe na D) angalau katika Kiingereza na Hisabati, O-Level Secondary Education,
AU
4. Cheti cha mwaka mmoja kutoka taasisi inayotambulika na ufaulu wa Kiingereza na hisabati “O” level kabla ya kupata cheti hicho.
5. Na vyeti vingine kama vitakavyotambuliwa na Bodi kila baada ya muda

MASOMO YA ATEC I NI HAYA HAPA

T.01 Bookkeeping and Accounts

T.02 Business Mathematics and Statistics

T.03 Intro. To Information & Comm. Tech

T.04 Business Communication Skills

Qualifications za Kuingia Accounting Technician (ATEC II)

Mtahiniwa mtarajiwa anayetaka kujisajili kwa ajili ya mitihani ya Accounting Techinician ni lazima aoneshe, uthibitisho wa kuwa na moja wapo ya sifa zifuatazo:-

1. Barua ya Taarifa ya kufaulu Accounting Techinician Level I
2. Advanced Level Secondary school Certificate kwa wanafunzi waliofanya masomo ya biashara. Lakini ni lazima wawe na ufaulu wa principal mbili. Yaani kama ni ECA angalau kwenye hayo masomo upate Masomo mawili alama D..
3. Cheti cha Accounting (NTA Level 4)
4. Diploma ya miaka miwili isiyo na somo kuu la Accounting – NTA Level 6
5. Wenye advance Level Secondary Education Certificate waliofanya masomo ya biashara O-Level na kupata ufaulu katika (Bookeeping na Commerce, yaani angalau D)

MASOMO YA ATEC II NI HAYA HAPA

T.05Principles of Accounting and Auditing
T.06 Principles of Cost Accounting and Procurement
T.07 Elements of commercial knowledge management practices and taxation
T.08 Accounting for public sector and Cooperatives

MUHIMU:

Mtahiniwa Mwenye Cheti Cha ATEC II Ni Sawa Na Mtahiniwa mwenye Diploma Ya Uhasibu ya Miaka Miwili. Hivyo Anaruhusiwa kuendelea na Degree YA Biashara/Uhasibu katika Chuo Kikuu chochote nchini. Kama Mtahiniwa Asipoamua kuendelea na Degree, basi anaendelea na Foundation Stage..

Qualifications za Kuingia Foundation Stage (Hii ni sawa na Degree ya Uhasibu)

Mtahiniwa mtarajiwa anayetaka kujisajili kwa ajili ya mitihani ya PROFESSIONAL ni lazima aoneshe uthibitisho wa kuwa na mojawapo ya sifa zifuatazo:
  1. NBAA Accounting Technician Certificate (ATEC II)
  2. Diploma ya miaka miwili katika Accounting au Accounting and Finance NTA Level 6
  3. Shahada kutoka chuo kikuu kinachotambulika au Taasisi ya Elimu ya juu (isiyokuwa ya Accounting).

  • Misamaha inaweza kufikiriwa somo kwa somo kutegemea masomo ya mtahiniwa.
MASOMO YA FOUNDATION STAGE NI HAYA HAPA

A1 Quantitative Techniques

A2 Business and Management

A3 Accounting

A4 Business Information

A5 Business Law

Ukifaulu mitihani hii ya Foundation unaendelea na Mitihani ya Intermediate then Final Stage.

NB: Mtahiniwa mwenye Degree ya Uhasibu (Accounting) anaanzia Intermediate Stage (Masomo 6), then Final Stage (Masomo 4).

MASOMO YA INTERMEDIATE HAYA HAPA

B1 Financial Management

B2 Financial Accounting

B3 Auditing Principles and Practice

B4 Public Finance and Taxation I

B5 Performance Management

B6 Management, Governance and Ethics

MASOMO YA FINAL HAYA HAPA
C1 Corporate Reporting

C2 Auditing and Assurance Services

C3 Business and Corporate Finance

C4 Public Finance and Taxation II

HAPO NDO UNAKUWA CPA (T)…

NADHANI SASA NIMEELEWEKA VIZURI

Rahisisha maisha yako ya shule / ya mwanao/ ya Nduguyo Kama mpango ni kusomea Uhasibu.. Usizunguke sana!!

KWA MAELEZO ZAIDI

Njoo Step Ahead Financial Consultant
tukupe suluhisho la Uhasibu!! Tuko ndani ya Jiji la Dodoma.. Tupigie kwa simu no. 0713388317/0757749641
COMBINED SAFCO PG 1 AND 2_page-0001.jpg
COMBINED SAFCO PG 1 AND 2_page-0002.jpg
 
Attachments

  • COMBINED SAFCO PG 1 AND 2.pdf
    1.9 MB · Views: 104

View attachment 1111650View attachment 1111651

kama nina degree moja nitaruhusiwa kuanza ATEC I?
 
Hakika nimefunguka kitu ambacho sikukijua kwa muda mrefu sana.
Shukran kwa mara nyingine tena
 
kama nina degree moja nitaruhusiwa kuanza ATEC I?
Kama una degree ya Accounting unaanzia Intermediate Level masomo 6 then final level masomo manne.

Kama una degree lakini siyo accounting unaanzia Foundation stage masomo matano then unaendelea na intermediate then final..
But hapo kwenye foundation you might get exemptions on subject by subject basis.. Kwa mfano wewe umesoma Degree ya Statistics unataka usome CPA, Utaanzia foundation but hutafanya masomo matano... hilo somo la A1 Quantitative Techniques kwenye foundation utakuwa Exempted maana tayari ushalisoma... etc..
 
Utaratibu wa kujiunga ukoje?

Taratibu za usajili
Usajili wa Watahiniwa

Watahiniwa wanaotarajia kujisajili kwa ajili ya mitihani ya Bodi wanatakiwa kujaza Candidacy Registration Form. Form hii ni lazima ijazwe kwa ukamilifu na kuwasilishwa Bodi pamoja na vyeti vinavyohusika vyeti vya masomo na vyeti vya kitaaluma, vikiambatanishwa na matokeo ya mitihani pamoja na picha tatu za pasipoti za rangi
Bodi imeweka masharti ya chini kabisa ya kujiunga yatakayo mwelekeza mtahiniwa kutambua alama zake za kujiunga na mitihani kutegemea sifa za awali zilizopatikana mwanzo.
Maombi ya msamaha/ Exemptions
Bodi hutoa msamaha kwa sehemu za mitihani yake. Msamaha huu unasimamiwa na Sera ya msamaha ya NBAA kuwa na sifa za kusamehewa, mtahiniwa ni lazima ajaze sehemu ya msamaha kwenye fomu ya usajili wa utahiniwa.
Maombi ya msamaha ni lazima yakamilishwe kabla ya kuanza kiwango ambacho msamaha unaombwa. Hata hivyo, mtahiniwa atafikiriwa upya kwa msamaha iwapo atawasilisha sifa ya ngazi ya juu, kwa sifa zilizopatikana nchi za nje ya Tanzania waombaji wanatakiwa kuwasilisha maelezo ya muhtasari wa masomo na matokeo kwa ajili ya mtihani anaotaka kufanya. Mtahiniwa hana budi kuwasilisha maombi ya msamaha angalau miezi miwili kabla ya tarehe ya mwisho ya maombi ya mtihani anakusudia kufanya.
Pia ni muhimu kuonesha uthibitisho kuwa Chuo Kikuu au Taasisi iliyotoa sifa hizo ni taasisi iliyotambuliwa rasmi. Uthibitisho huu ni lazima upatikane kutoka Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE) au taasisi nyingine muhimu za kitaaluma.
Tarehe ya mwisho kwa usajili wa mtahiniwa
Mtahiniwa mtarajiwa anaweza kusajiliwa wakati wowote wa mwaka, hata hivyo, kuna haja ya kuzingatia tarehe mtahiniwa anayotaka kufanya mtihani ili aweze kutumia maombi ndani ya tarehe zilizotajwa.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha fomu ya usajili wa mtahiniwa ni 15 Februari kwa mitihani ya Mei na tarehe 15 Agosti kwa mitihani ya Novemba.
Usajili wa kuchelewa
Maombi yaliyopokewa baada ya tarehe za kufungwa kwa maombi yanastahili ada ya kuchelewa.
Kuondoa usajili
Mtahiniwa anaweza kuondoa usajili kwa ridhaa yake au kama alivyoelezwa kwenye sharia ndogo za mafunzo na mtihani.
 
Mode of application ikoje? Ni online au vingonevyo?

baada ya ku download una submit kwa njia gani?
Postal au hand delivery kwenye ofsi za NBAA. Ukiingia wemye website yao utapata contact zao.
Ni vizuri ukifika ofsini kwao kwanza..
Hapo ni kujisajiri tu, then ukitaka kusoma unajisajiri kwenye CPA Review classes centre. Kama uko Dodoma karibu kwenye centre yangu, kama uko Dar utaniambie nikuelekeze review classes zilipo.
 
Kuna review center IRINGA?
 
Kuna review center IRINGA?
Iringa inaweza ikawepo though siko familiar nayo. Cha kufanya kama utakuwa interested kusoma review utanitumia namba yako then nitakuulizia kwenye Group letu la NBAA Trainers akijitokeza mwenye review huko nitakuunganisha naye. Nitumie kwenye number yangu hii hapa 0713388317.
 
Nimekutumia Meseji kwenye simu mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom