Kwa wale wanaopenda kuoomba ushauri wa kimapenzi kwenye mitandao ya kijamii

Democrat7

Member
Nov 26, 2013
32
11
Habari wa ndugu,

Kuna watu wengi , wake kwa wauume wana tabia ya kupeleka matatizo yao ya kimahusiano(mapenzi au ndoa) kwenye mitandao ya kijamii ili kuomba ushauri. Wanapoongea wanajaribu kutumia majina feki but story zinakuwa za kweli. Mfano utaona mtu anasema , mimi ni msichana wenye umri huu nina mpenzi wangu.....(anaendelea kuongea tatizo lake), au mimi ni mvulana nina umri huu, ninampenzi wangu .....(anaendelea kuelezea tatizo). Au utasikia jamani mimi ni mke wa mtu, lakini nimejikuta nimetoa nje ya ndoa naombeni ushauri, au utamkuta kaka anasema jamani mimi nimeoa, lakini kuna dada mmoja kazini huwa nafanya naye mapenzi, nahisi mke wangu anaanza kunifuatilia.

Watu hao wanapeleka siri zao kwenye mitandao ya kijamii ili wapewe ushauri. Sasa mimi swali langu ni kwamba wanajuaje kama hao wapenzi wao hawatasoma hizo stori zao kwenye mitandao hiyohiyo? Mtu akisoma story na kulinganisha matukio yaliyotokea katika uhusiano au maudhui ya ujumbe atagundua kuwa hiyo story inamhusu na atajua kuwa aliyeipeleka ni mwenza wake.

Sasa jamani kwa nini watu huwa wanafanya ujinga huu wa kuanika siri zao? Je ushauri wanaopewa unalingana na risk wanayoichukua just in case mhusika akasoma hiyo story kwenye mtandao?

TAFAKARI, CHUKUA HATUA
 
Unafikiri walitakiwa wapeleke wapi ambapo wangepata ufumbuzi bila kutoa siri.Kwa Mchungaji ?wachungaji wenyewe wakina Mzee wa upako au akae kimya ili atunze siri ya mtungi?

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
We all need smbdy to lean on...km humu jf kunasaidia sana w2 kupunguza stress,
kwn mpenzio akisoma ur problem atahakikisha vp ni wew?sio rahisi
 
^^
Kuna kisa cha kubuni kilikuwa kinasema kuwa "mke na mume walikutana kwenye mkutano wa wachawi,kila mmoja akabaki anamshangaa mwenzake Hee! Kumbe na wewe mchawi?.."
..
Ndivyo ilivyo na mitandao,ukiona umeguswa au mmekutana na mwenza wako humu,MEZEA chukua ushauri wa kukujenga.
Mwenye siri ni Mungu Binadamu ilimshinda kutunza
^^
 
Ni heri kuomba ushauri kuliko kugugumia mwenyewe ufe kwa presure ama ukonde kwa mawazo. Sioni tatizo hata lolote hapo
 
Sisi tunafarijika bhana na JF inatupunguzia stress kiukweli. kamwe mimi sitoki humu ndani
 
Ukipata matatizo kila mtu unayemuona unaamini anaweza kukusaidia hata usishangae

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom