Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,270
Mnapokwenda kutafuta maisha na kuwekeza nyumbani, mlishafikiria maisha ya uzeeni na gharama za matibabu? Nchi za Scandinavia na baadhi ya nchi za Ulaya matibabu ni bure hasa ukiwa umelipa tax katika maisha yako ya kazi.
Unapoamuamua kustaafu nyumbani, umejenga ghorofa zuri tu, lakini maradhi ya uzee nayo yanakusogelea. Hospitali zetu zinahitaji Bima ya Afya wakati nchi uliyofanyia kazi ujanani unaweza kupata tiba bure.
Wa Jamaica hawana matatizo, wakiingia Ulaya wanaona ni mother country, wananunua nyumba na wala hawawazi tena backa yard (nyumbani). Matatizo yako kwa Waafrika, wanapenda kuendeleza nyumbani.
Waghana na Wanigeria wengi walioingia Ulaya miaka ya 60, walijenga kwao. Sasa wakiwa na miaka 80, 70 gharama za matibabu hawazimudu tena, wenye watoto wanarudi Ulaya kupata matibabu ya bure. Wasio na watoto na hawakuacha nyumba Ulaya kurudi inakua ni vigumu.
Afrika tunahitaji kuboresha mfumo wa afya. Wazee wenye pesa wanajipangia check up South Africa mara mbili kwa mwaka kama $5,000.