Myangu
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 7,172
- 9,700
Ukistafu huduma bure mzee hajakufahamisha vzr.Bahati yake
Ukistafu huduma bure mzee hajakufahamisha vzr.Bahati yake
Ukiwa na miaka 80, 90… Tanzania ni rahisi kupata huduma ambazo ni personalised care. Unapata watu wa kukuhudumia masaa 24 na unaweza kuwalipa laki 5-6 kwa mwezi wote wawili.Kweli kabisa kwenye suala la huduma ya afya.
Ila mzee wangu aliishi UK kama miaka 23. Nashangaa hakutaka kutumia fursa hiyo wala nini. Hata ile kwenda kutembea hakutaka kabisa. Madai yake upweke wawauwa wazee huko kuliko magonjwa. Akadai home is where your heart is. Na kuzidi kudai bongo raha pamoja na shida zake.
Twakubaliana nawe kuishi ni kupanga na kupanga ni kuchaguwa.
Kuna huduma za kulipia nssf km sijakosea badala ya hiyo NhifKwahiyo diaspora wakale waliko peleka mboga 😂
Mnapokwenda kutafuta maisha na kuwekeza nyumbani, mlishafikiria maisha ya uzeeni na gharama za matibabu? Nchi za Scandinavia na baadhi ya nchi za Ulaya matibabu ni bure hasa ukiwa umelipa tax katika maisha yako ya kazi.
Unapoamuamua kustaafu nyumbani, umejenga ghorofa zuri tu, lakini maradhi ya uzee nayo yanakusogelea. Hospitali zetu zinahitaji Bima ya Afya wakati nchi uliyofanyia kazi ujanani unaweza kupata tiba bure.
Wa Jamaica hawana matatizo, wakiingia Ulaya wanaona ni mother country, wananunua nyumba na wala hawawazi tena backa yard (nyumbani). Matatizo yako kwa Waafrika, wanapenda kuendeleza nyumbani.
Waghana na Wanigeria wengi walioingia Ulaya miaka ya 60, walijenga kwao. Sasa wakiwa na miaka 80, 70 gharama za matibabu hawazimudu tena, wenye watoto wanarudi Ulaya kupata matibabu ya bure. Wasio na watoto na hawakuacha nyumba Ulaya kurudi inakua ni vigumu.
Afrika tunahitaji kuboresha mfumo wa afya. Wazee wenye pesa wanajipangia check up South Africa mara mbili kwa mwaka kama $5,000.
Hii pension ukiipokelea bongo, Mwigulu wa wakati huo anachomoa tozo la miamala.Utaratibu ni kwamba ukishafikia umri wa kustaafu unayo haki ya kuishi popote na unalipwa mafao yako ambayo yanategemea ulifanya kazi kwa mshahara kiasi gani.
Ni hela inayokuja kila mwezi, kama ni mtu aliyejipanga vizuri mapema. Inatosha kulipia bima nzuri tu Afrika na kuishi vizuri. Pia anakuwa na uwezo wa kusafiri muda wowote kurudi ulaya kwenda kupata matibabu.
Pia akipenda, njia nzuri ni kukata bima toka Ulaya. Ni bora kuliko za kiafrika.
Hii pension ukiipokelea bongo, Mwigulu wa wakati huo anachomoa tozo la miamala.
Asante sana hii ya pension ni nzuri kama huna wategemezi wengi na kama ulivyosema kujipanga.
Sio cha bahati ukweli ndio huo. Mtumishi wa umma akistaafu anapewa bima ya mstaafuBahati yake
Kabisaaa kitu cha kumfaidisha mwananchiSiku hizi BIMA packages zipo nyingi hata huko NHIF. Kama kweli mtu aliishi ulaya au marekani hadi uzeeni hawezi kushindwa 2,000,000 premium membership ya nhif kwa mwaka.
Huwa nasema serikali iangalie swala la universal health care, kama tuna tozo kibao ambazo a normal mwananchi doesn't really benefit, why can't we have tozo for health care. Then baada ya hapo kila mtu awe na kadi yake kwa ajili ya matibabu bure! Kama tunakatwa TSH 100kwa kila lita ya mafuta, I'm pretty sure mwigulu can come up with a tangible system that'll be helpful to a normal mwananchi.
Wewe umeshasikia sifa za Mloganzila, ukimpeleka mgonjwa mpe buriani kabisa.Kila kitu kinategemea mtu anavyojipanga. Ulaya apartment ya vyumba viwili, sebuleni, jiko na bafu mtu unanunua kwa almost 300,000€ ambayo unalipa kwa mkopo. Hiyo hela kama unaweza kuiwekeza bongo vizuri, uwezekano wa kuishi vizuri ni mkubwa kuliko ukiwa Ulaya.
Kuna gharama kubwa sana za kumiliki nyumba ikiwepo mtaji kwanza, na uendeshaji wa nyumba ni ghali mno. Bora mtu ajipange awekeze huko kuliko kuwekeza ile hela ulaya.
Gharama za miamala siyo mbaya ukizingatia unaweza kutumia kadi yako ya benki ya Ulaya popote na ukakwepa japokuwa inaweza kuwa ghali kutumia kadi nje ya Ulaya but still it is an option.
Ukinunua nyumba Ulaya, jasho lako lote inabaki Ulaya kwa mfumo wa mkopo.
😭 Ferdinand Masau.Yule Dr alifungua clinic ya moyo Dar na aliambiwa ameiba vitanda vya Muhimbili, mwisho baba wa watu alikufa kwa stress.
Wewe umeshasikia sifa za Mloganzila, ukimpeleka mgonjwa mpe buriani kabisa.
Kama pension yako itatosha kwenda Nairobi hospital na unaishi Tanzania hapo utakua umeyapanga maisha.
Kwakweli kama hujanunua nyumba na kumaliza mortgage, au kujenga Africa. Kuitegemea pension kwa malazi, chakula na matibabu utaishi kimasikini sana.Mimi kwa kweli nawashauri marafiki waishio Ulaya wajipange mapema.
Kila kitu kinawezekana ila inategemea umeanza mapema kiasi gani.
Kwakweli kama hujanunua nyumba na kumaliza mortgage, au kujenga Africa. Kuitegemea pension kwa malazi, chakula na matibabu utaishi kimasikini sana.
Kadi hapa gharama itakuwa labda ATM tu lakini ukilipia hotels na sehemu zinazokubali Mastercard au Visa, hamna muamala wowote. Unachanja kama kawaida.Kila kitu kinategemea mtu anavyojipanga. Ulaya apartment ya vyumba viwili, sebuleni, jiko na bafu mtu unanunua kwa almost 300,000€ ambayo unalipa kwa mkopo. Hiyo hela kama unaweza kuiwekeza bongo vizuri, uwezekano wa kuishi vizuri ni mkubwa kuliko ukiwa Ulaya.
Kuna gharama kubwa sana za kumiliki nyumba ikiwepo mtaji kwanza, na uendeshaji wa nyumba ni ghali mno. Bora mtu ajipange awekeze huko kuliko kuwekeza ile hela ulaya.
Gharama za miamala siyo mbaya ukizingatia unaweza kutumia kadi yako ya benki ya Ulaya popote na ukakwepa japokuwa inaweza kuwa ghali kutumia kadi nje ya Ulaya but still it is an option.
Ukinunua nyumba Ulaya, jasho lako lote inabaki Ulaya kwa mfumo wa mkopo.
Usitupangie maisha, kama ukihitaji kuishi kibepari we ishi tu kivyako...Inategemea ntu na ntu.
Mwisho wa siku sote ni wapitaji katika dunia hii, hata utibiwe vipi mwisho wa siku utaondoka tu, hivyo nivyema ukafanya kile kinachokupa amani.
Watanzania kwa ujumla kilichotuharibu ni kuzaliwa kwenye ujamaa, yani mtu hata uwe wapi bado utakumbuka nyumbani, utamkumbuka mjomba, shangazi, etc, wenzetu kwao familia ni baba mama mtoto, kaka na dada wanapambana kivyao. Obama akiwa senetor tu, angeweza amisha ndugu zake wa karibu USA, ila amekulia kwenye ubepari.