Kwa wale wanaofanya Diet kujeni huku tuongee

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Habarini za kazi ,business na wale walioko shule

Leo napenda kuangalia hili swala zima la kina dada wanaofanya Diet ili angalau kuufanya mwili uwe mzuri na kuepusha magonjwa kama BP Nk Nk pia kwenda na fashion za urembo

Ni aina gani hasa yaa vyakula na matunda ,pia diet ipi itumike angalau iweze kumsaidia mtumiaji awe katika hali nzuri
,nimeshuhudia wengine wakifanya diet yes wanakonda/pungua lakini ukimwangalia vizuri usoni anaonekana kama amezeeka na ngozi haina afya au mvuto kama mwanzo ,wakati alipokuwa hajafanya Diet ngozi ilikuwa ya kupendeza nyororo na ya kuvutia usoni

,wengine hata kuulizwa mbona ngozi ya uso imejikunja?

Je ni vyakula gani , matunda na vinywaji gani vitumike ??

Nakaribisha michango yenu wadauzi mnaoenda na wakati
MziziMkavu
 
Fanya mazoezi hakikisha umetoa jasho na kweli mwili uchoke, kula kiasi matunda kwa wingi, protein na maji. Epuka kula wali hasa usiku, pendelea ugali,tambi( pasta), viazi na ndizi. Cha muhimu ni kula kiasi. Kwa miezi 6 nimepunguza kg 10 kutoka kg 82 na nimeacha kukoroma.
 
I will do it, now najitahidi mazoezi kiasi, hapo kwenye kula hasa wali ni sheeeeda
 
maji mengi tena ya uvuguvugu na matembezi ya jioni. kulala kwa wakati......lunch matunda mchanganyiko
kabla ya kulala ikumbishe akili ni nn kusudio na dhumuni lako. kwa uchache huo tu inanisaidia kuwa na muonekano safi wenye afya.
asubuhi dona na mboga za majani pilipili kiduchu dah nafurahia maisha yangu haya.
 
Fanya mazoezi hakikisha umetoa jasho na kweli mwili uchoke, kula kiasi matunda kwa wingi, protein na maji. Epuka kula wali hasa usiku, pendelea ugali,tambi( pasta), viazi na ndizi. Cha muhimu ni kula kiasi. Kwa miezi 6 nimepunguza kg 10 kutoka kg 82 na nimeacha kukoroma.

Hapo kwenye wali ndo kwenye kizaizai
 
Fanya mazoezi hakikisha umetoa jasho na kweli mwili uchoke, kula kiasi matunda kwa wingi, protein na maji. Epuka kula wali hasa usiku, pendelea ugali,tambi( pasta), viazi na ndizi. Cha m
B uhimu ni kula kiasi. Kwa miezi 6 nimepunguza kg 10 kutoka kg 82 na nimeacha kukoroma.
Mkuu unashauri mtu ale ugali usiku halafu aende kulala!? Mbona watalaamu wengi wa lishe wanashauri kula vyakula laini usiku hasa kutokana na mfumo wetu wa kusaga chakula kutokuwa na kasi ya kusaga. Inaaminika hata ndoto mbaya za kuota umekabwa na nyani shingoni au unafukuzwa na simba na ukijaribu kukimbia unashindwa hata kunyanyua miguu. Anyway ngoja waje wenyewe!
 
Fanya mazoezi hakikisha umetoa jasho na kweli mwili uchoke, kula kiasi matunda kwa wingi, protein na maji. Epuka kula wali hasa usiku, pendelea ugali,tambi( pasta), viazi na ndizi. Cha muhimu ni kula kiasi. Kwa miezi 6 nimepunguza kg 10 kutoka kg 82 na nimeacha kukoroma.

Swala la kula wali hapo naunga mkono.
Kwa utafiti wangu mimi mwenyewe niligundua wali una unachangia zito kuongezeka tofauti na ugali.
-Nilikula ugali mwezi mzima (lunch) na usiku matunda tu uzito ulipungua kutoka 70kg ->62
-Nilikula wali mwezi mzima (lunch) usiku matunda uzito uliongezeka 62->68
-pia nikila wali (lunch) huwa nakaa muda mrefu sihisi njaa ila nikila ugali saa 12 jioni nahisi njaa.

hitimisho: utumiaji wa ugali ni mzuri kwa mtu anafanya diet
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom