Kwa wale waliopitia UDSM pitia hapa toa mchango wa mawazo.

Apparent

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
220
110
Habari za muda huu wakuu.
Mimi nipo mwaka wa pili UDSM naomba kuuliza kama kuna aliewahi kufutwa kwenye mfumo baada ya kuchelewa kulipa ada.

Kusoma chuo bila mkopo ni mateso sana usajili unaisha leo halafu mwanaume huna kitu mfukoni na unatakiwa usome upate GPA nzuri.

Upande mwingine unaambiwa Serikali ya JPM ni ya wanyonge,usicheze na psychology ya maisha kuvurugika huwezi kutembea na kufanya la maana sababu una stress.

Kama una mkopo mshukuru Mungu toa shukrani kanisani na miskitini hujui wenzako wana hali gani inauma sana.
f4d3a6d0f40e7a826dff7743bc1c02c6.jpg
 
Duuu mkuu pole sana aiseee...chuo bila mkopo ni hatari sana hasa sis watoto wa jua kalii..ongea na uongozi wa chuo huwa ni waelewa sana
 
Mdogo wangu mbona hili limetolewa ufafanuzi na uongozi wa daruso....

Inaonekana hufatili mambo ya chuo kwako.....

Nenda ofisi za administration kwenye college yako hapo UDSM wakakupe maelekezo
 
udsm hakuna mtu huwa anafutwa kisa kuchelewa kulipa ada..kuna washkaji zangu wao walikua wanalipa ada wiki moja kabla ya final exams kuanza.
 
Mdogo wangu mbona hili limetolewa ufafanuzi na uongozi wa daruso....

Inaonekana hufatili mambo ya chuo kwako.....

Nenda ofisi za administration kwenye college yako hapo UDSM wakakupe maelekezo
tufahamishe ndugu.ufafanuzi gani
 
Back
Top Bottom