Kwa wale walioko kwenye ndoa/mahusiano ya muda mrefu(wanaoishi pamoja)

mmmh.
nadhani mod sasa ni wakati wa kuanza kufuatilia majibu ya Member Wengine kwa sie wanyonge.
Kwa hiyo Jibu langu limekumaliza kabisa, sasa na wewe unataka nifukue Makaburi saa hii, ujue watu wana wivu???
 
Sawa kabisa, lakini huoni miaka 10 ni kama tayari wako kwenye ndoa, sema hawana vyeti?
kwa hiyo hawa wakiachana ni kwasababu wamechokana na sio kwamba hawajuani kiaundani.
Mimi naongelea maswali yanayojitokeza pale tu unapoingia kwenye Mahusiano/Ndoa na sio kama umeshakaa kwenye Ndoa/Mahusiano miezi 6 huko ndio unaanza kujiuliza?
Fuatilia hata wale wanao kuwa kimapenzi bila kuishi pamoja na mwisho wao huwa kila mtu anatafuta mwingine ndiyo maana vyeti hutolewa mapema siku hiyo hiyo mkifunga ndoa ili mkaangaike navyo huko
 
Ukiwa kwenye ndoa ni sawa na kutakiwa kumeza jiwe yataka moyo sana, kikubwa uvumilivu, subra na kuutunza mdomo wako maana ndio utakao weza au kushindwa kulimeza jiwe
eti kumeza jiwe haaaa haaaa uione watu 10yrs kwenye ndoa kuna ndoa nyingine mwezi ndoa haipo hata masalia hakuna jamani
 
Jamani LadyAj ndio kusema Kama Nina kitu nataka kujua kuhusu mwenza wangu na labda familia yake nisiulize sababu nitaivunja ndoa?

Mfano: Baada ya mwezi ndani ya ndoa, nakuja ambiwa kuwa wale watoto wa shangazi,mjomba (wako) uliokuwa unasomesha ni jukumu langu sasa kuwasomesha....huoni Kama nilipaswa kuliulizia mapema Zaidi?
Huwezi kujua vyote mpaka uingie kwenye hiyo familia, kuna vitu huwezi ambiwa na mtu yeyote unazungukwa kama roundabout
 
Kitu ambacho wengi hawajuwi ni kuwa wengi wa watu me/ke wanakuwa na tabia za aina mbili. Ya kwanza ni ile ya kabla ya ndoa na pili ni baada ya ndoa. Kwa mfano tuchukulie mtu kama bbade kabla ya kuolewa anakuwa mwenye tabia njema kabisaa malavi davi upole a ucheshi wa kweli kweli na mara tu baada ya ndoa unampata bbade mwengine kabisaaaaa. sasa hapo ndio utajua kwa nini wahenga walisema ndoa ni uvumilivu.
Sasa utaikimbia ndoa? Na wanapofungisha huanza tabu ndiyo raha inafuata sijui waliwaza nini kuweka kiapo cha hivyo
 
Tutakushirikisha mangapi ndugu yangu!? Maana kuna mengi sana
Kuna ya unyumba
Ya ndugu wa mume
Ya marafiki wa mume
Ya michepuko
Minuno na misuso
Kuna maneno ya kashfa na dharau
Kuna mengi mnoo hata hayamaliziki
Kikubwa Subira tu na moyo wa imani
nikumeza jiwe tu
 
Huwezi kujua vyote mpaka uingie kwenye hiyo familia, kuna vitu huwezi ambiwa na mtu yeyote unazungukwa kama roundabout
Huoni ndio inachangia mahusiano yapwae...na michepuko iongezeke?
Ndio maana wanasema Marry your Best friend
 
Langu lililotikisa mahusiano yangu binafsi ni La mama mkwe,ngoja nipate Iftari kisha nitakuja tena kukuelezea vile namna alifanikiwa kunitikisa,mengine haya ya kawaida tu
Pole sana, mpe hi bimkubwa huyo!
 
Mfano mimi Binafsi nilishaingia kwenye mahusiano na mtu wa Taifa/Raia tofauti na mimi, baada ya kuzama kwenye mapenzi ndio tukaanza kujadili tutaishi wapi? Kila mmoja wetu akavutia upande wake, pamoja na kupendana kwetu tuliachana sababu hiyo, iwapo ningeuliza hili swali mapema pengine tusingeanzisha mahusiano yetu nikatafuta wa Taifa langu.
Kama ni hivyo mbona unaweza kufa bila kula papuchi....! Papuchi inaliwa kwanza alafu ndio mipango mingine inafuata
 
Kuna mambo yanahitaji kujadiliwa mapema ili kama hamuendani muachane mapema sana. Dini, watoto, wapi mtajenga na kuweka makazi ni muhimu sana.
Hilo nakubaliana na wewe mkuu but huwezi zuwia au kujua yote,kuna mambo hujitokeza wakati watu wameshaoana,ni kama mtu aliyeomba kazi utamfanyia interview na ataijibu kwa ufasaha but still hiyo haiku "garantee" kua huyo atakuja kua mfanyakazi bora au mwenye nidhamu ya kazi,

Hivi karibuni tumeshuhudia watu mbalimbali mpaka mawaziri wakitumbuliwa kutoka kwenye nyadhifa zao!! nadhani umenielewa.
 
Kama ulikuwa kichwani mwangu.....hayo ndio maswahibu ninayo zungumzia, ili tuelimishe wengine wanaoanza kufikiria kwenda kwenye maisha ya ndoa au hata mahusiano ya kawaida tu.
Hata hivyo mada yako imekuwa fikirishi sana Dear ndio maana umeona baadhi ya wadau wameenda tofauti na kile ulichokuwa unahitaji kufahamishwa.

Naomba nirudi kwenye mada, kuuliza maswali muhimu ni vizuri lakini kumbuka kuna maswali yenye majibu tena yakuridhisha kabisa masikioni pa muulizaji sasa basi maswali na majibu hayo hayawezi kufanya maisha ya ndoa yakawa rahisi.

Baadhi ya watu wakishafunga ndoa huwa utadhani wanaingiwa na mapepo basi mambo mengi hujitokeza ndani yake unabaki kujiuliza mbona tulilijadili hili kabla hata ya kufunga ndoa? Kwanini sasahivi mtu huyu amekuja kukiuka matakwa yetu?
Hapo ndipo utajua umuhimu wa busara, hekima na uvumilivu.
 
Hata hivyo mada yako imekuwa fikirishi sana Dear ndio maana umeona baadhi ya wadau wameenda tofauti na kile ulichokuwa unahitaji kufahamishwa.

Naomba nirudi kwenye mada, kuuliza maswali muhimu ni vizuri lakini kumbuka kuna maswali yenye majibu tena yakuridhisha kabisa masikioni pa muulizaji sasa basi maswali na majibu hayo hayawezi kufanya maisha ya ndoa yakawa rahisi.

Baadhi ya watu wakishafunga ndoa huwa utadhani wanaingiwa na mapepo basi mambo mengi hujitokeza ndani yake unabaki kujiuliza mbona tulilijadili hili kabla hata ya kufunga ndoa? Kwanini sasahivi mtu huyu amekuja kukiuka matakwa yetu?
Hapo ndipo utajua umuhimu wa busara, hekima na uvumilivu.
Na mimi nilihisi hivyo, nilihitajika kutoa mifano kidogo ili wengine wapate kuelewa, ila taratibu wachache wameweza kunielewa.

Safari bado ni ndefu....
 
Back
Top Bottom