Kwa wale wajuzi wa ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,763
35,201
Habari za muda huu wakuu.

Naomba msaada wa kujua wanakupatikana Ng'ombe bora wa maziwa. Zaidi kwa mamahitaji ya ng'ombe mwenye mimba ambae hatachukua muda mrefu kuzaa.

Nitaomba kujua
1. Aina na gharama za Ng'ombe
2. Mazingira au hali ya hewa sahihi kwa Ng'ombe
3. Ushauri kuhusu ustahimilivu na matunzo ya Ng'ombe
4. Uzalishaji wa Ng'ombe au kiasi cha maziwa anachoweza kutoa na muda anaoweza kukamuliwa

Na ushauri mwingine wowote kuhusu huu uwekezaji.

Asanteni
 
Ila unaweza nunua ng'ombe alafu asitoe kiwango cha naziwa ulichoambiwa halafu ukiwaambia wanasema hujawahi kufuga ng'ombe umekosea mwenyewe hapo umeshapata hasara.

Anyway ngoja waje wakupe muongozo.
 
Habari Mkuu? Kuhusu ufugaji huu kwa ajili ya maziwa hasa kama ndio unaanza nakushauri kuwa makini sana kwenye ununuaji wa ngombe mkubwa hasa kama alishazaa. wafugaji wengi hawatoi historia kamili ya mnyama sometime unaweza kuta mnyama anashida ila wanakuficha.

Kesi yangu ilikuwa hivi nilinunua ngombe mkubwa na alishazaa kama mara 3 na alikuwa na mimba ya miezi mitatu wakati na mnunua na ngombe alikuwa na body score siyo mbaya ila baada ya kuzaa nimegundua ana shuda ya kiwele chuchu 2 hazitoi maziwa kabisa hivyo nikawa nimepeta hasara ya maziwa machache.

Hivyo kuwa makini sana ni bora ukanunua mtamba ngombe jike ambaye hajawi zaa akaanzia uzao wa kwanza kwako pia kuna taasisi za serekali wanauza mbegu japo ni kwa foleni na bei zimechangamka. Pia kuna ranchi ya mbogo walianziasha utaratibu wa kuagiza ngombe south afrika wenye kiwango kwahiyo kama mfuko upo poa wacheki upate kilicho bora.

Mbota.
 
Uwekezaji katika biashara ya Ufugaji wa ng'ombe ni uamuzi mzuri Ila unatakiwa nawe uwe committed siyo unawaachia wafanyakazi tu, Mara kwa kwa unatakiwa uwepo ndio utaweza kufikia malengo.

Ng'ombe Bora wa maziwa unaweza kupata kwa wafugaji wenyewe au katika taasisi maalum zinazojihusisha na uuzaji wa hao ng'ombe.nachofahamu ni kuwa ng'ombe wa maziwa wote ni wazuri Ila wanatofautiana kutokana na Aina yake,pia huwa Kila ng'ombe hafanani na mwenzake.

Kwa Dar, ng'ombe wa maziwa mwenye mimba anauzwa kuanzia sh. 2500000 iwe Aina ya Ayshire, fresian jersey n.k. Ng'ombe Hawa wanahitaji mazingira Safi na salama kwao, matibabu chakula Cha kutosha na maji, muda wa kupumzika pamoja na upendo na huruma.

Ng'ombe mzao wa Kwanza huanza kutoa maziwa kiwango Cha chini kulinganisha na kigezo Cha sifa ya utoaji wa maziwa kwa siku wa Aina ya ng'ombe husika.halafu kadri anavyozidi kuzaa ndio maziwa huongezeka mpaka kufikia kiwango chake halisi na huwa anakamuliwa mwisho miezi Saba. Wasiliana na 0715 141474 ni mfugaji Bora wa wilaya ya kinondoni
Habari za muda huu wakuu.

Naomba msaada wa kujua wanakupatikana ng'ombe bora wa maziwa. Zaidi kwa mamahitaji ya ng'ombe mwenye mimba ambae hatachukua muda mrefu kuzaa.

Nitaomba kujua
1. Aina na gharama za ng'ombe
2. Mazingira au hali ya hewa sahihi kwa ng'ombe
3.Ushauri kuhusu ustahimilivu na matunzo ya ng'ombe
4.Uzalishaji wa ng'ombe au kiasi cha maziwa anachoweza kutoa na muda anaoweza kukamuliwa
5.........
Na ushauri mwingine wowote kuhusu huu uwekezaji.


Asanteni
'
 
Hongera kwa wazo. Nitoe maelezo niliyoyapata kwenye maonesho za 8-8, 2020 mbeya. KANUNI 5 ZA UFUGAJI BORA. 1. Mbegu bora 2. Banda bora 3. Lishe bora 4. Udhibiti wa magonjwa (chanjo, matibabu), na usafi. 5. Utunzaji wa kumbukumbu. AINA ZA MBEGU. 1. Fisheries ( anatoa maziwa machache ila yana mafuta mengi. Anafaa zaid kwny barid e.g mbeya) 2. & 3. Asha & Diese (wanatoa maziwa meng bt mafuta machache, wanafaa zaid kwenye joto e.g morogoro) 4.

Brown swis ( nimesahau maelezo mana n mda mrefu). pia tangu ng'ombe kuzaa kamua miez 6-7 then acha 2-3 ajiandae kuleta ndama mpya. Tangu kuzaa subir at least 2 or 3+ months ndo apandwe tena. JINSI YA KUMPANDISHA. 1. tumia njia ya kawaida dume juuu ya jike au 2. Uhimilishaji (gharama ndogo za uendeshaji wa mradi). TAASISI ZA KUTEMBELEA. 1. Tarere (uyole mbeya chuoni) 2. Nationa artificial incermination centre ( arusha-usa river). Karibu
 
Back
Top Bottom