Kwa Wale Wajuzi Wa Cement Bora

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Naamini mafundi wazoefu watakuwa wanajua. Naomba kujua,

Cement ya Bamburi ya kule Kenya inaweza kulinganishwa na cement gani ya hapa Tanzania kwa viwango vya ubora?
 
Sent from my cupboard using mug
Cement zote ziko sawa hamna cement inayo izidi nyenzake hapa duniani.

Mfano hiyo cement ya kenya ya 42.5N ni sawa na cement ya simba, dangote, twiga ya 42.5N! HAKUNA TOFAUTI.

Vivyo hivyo kitaalamu cement ya kenya ya 32.5R ni sawa na cement ya dangote ya 32.5R! HAKUNA TOFAUTI.

Acha kuwa na mawazo potofu ya kusema cement hii ni bora kuliko ingine. Si kweli.
 
Cement zote ziko sawa hamna cement inayo izidi nyenzake hapa duniani.

Mfano hiyo cement ya kenya ya 42.5N ni sawa na cement ya simba, dangote, twiga ya 42.5N! HAKUNA TOFAUTI.

Vivyo hivyo kitaalamu cement ya kenya ya 32.5R ni sawa na cement ya dangote ya 32.5N! HAKUNA TOFAUTI.

Rekebisha hapo isomeke 32.5R Bumburi=32.5R Dangote umeandika N
 
Cement zote ziko sawa hamna cement inayo izidi nyenzake hapa duniani.

Mfano hiyo cement ya kenya ya 42.5N ni sawa na cement ya simba, dangote, twiga ya 42.5N! HAKUNA TOFAUTI.

Vivyo hivyo kitaalamu cement ya kenya ya 32.5R ni sawa na cement ya dangote ya 32.5N! HAKUNA TOFAUTI.

Acha kuwa na mawazo potofu ya kusema cement hii ni bora kuliko ingine. Si kweli.
Cement zote zinakaribiana ubora isipokua ubora hupungua ama hupanda kulingana na uchanganyaji wa fundi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Swali la nyomgeza kwako J. Ipo imani kwa mafundi kwamba cement fulani ni nzr kwa kufyatulia matofali na cement fulani ni nzr kwa kujengea. Je imani hii ni sahihi kitaaalamu au ni conspiracy tuu? Na kama ni kweli ujuavyo ww kwa soko letu la hapa ndani la cement, ungeshauri cement ipi itumike kwa kufyatualia matofali na ipi kujengea? Ahsante.

NB: Hii project inapangwa kufanywa Dar es Salaam.
 
Ungeka wazi kwamba ni cement gani wanasema ni nzuri na ipi si nzuri.

Cement yeyote inafaa provided haijakaa dukani zaidi ya mwezi mmoja tokea siku imetoka kiwandani.

Wa kuongezea tu kama unatumia mikono kutengeneza matofali tumia cement ya kampuni yeyote yenye namba 42.5N.
 
Ahsanten, naendelea kujifunza;

Kuhusu kuchanganya cement na mchanga kwa ujenzi wa nyumba ya kawaida ratio gani inatakiwa (karai ngapi za mchanga + mfuko mmoja wa cement) kwa viwango vyote hivyo vilivyotajwa hapo juu

42.5N na 32.5R

Sent from my cupboard using mug
 
Ungeka wazi kwamba ni cement gani wanasema ni nzuri na ipi si nzuri.

Cement yeyote inafaa provided haijakaa dukani zaidi ya mwezi mmoja tokea siku imetoka kiwandani.

Wa kuongezea tu kama unatumia mikono kutengeneza matofali tumia cement ya kampuni yeyote yenye namba 42.5N.

Ahsante mkuu. Sikutaja majina sababu sikumbuki zilikuwa ni cement zipi hizo ni muda kdg toka nimewasikia hao mafundi. Ahsante kwa ushauri wa hiyo no 42.5N endapo mikono itatumika kutengeneza matofali. Swali la nyongeza hapo ni what if mashine ndiyo itakayotumika? Na vp kwenye kujenga 42.5N ni sawa pia au kuna nyingine? Ninatanguliza shukrani za dhati.
 
Ahsanten, naendelea kujifunza;

Kuhusu kuchanganya cement na mchanga kwa ujenzi wa nyumba ya kawaida ratio gani inatakiwa (karai ngapi za mchanga + mfuko mmoja wa cement) kwa viwango vyote hivyo vilivyotajwa hapo juu

42.5N na 32.5R

Sent from my cupboard using mug
ndoo ndogo 18 kwa mfuko mmoja
 
Na kwenye joint ratio yake nayo pia itakuwa sawa na ya kwenye plasta au?

Sent from my cupboard using mug
 
Ahsante mkuu. Sikutaja majina sababu sikumbuki zilikuwa ni cement zipi hizo ni muda kdg toka nimewasikia hao mafundi. Ahsante kwa ushauri wa hiyo no 42.5N endapo mikono itatumika kutengeneza matofali. Swali la nyongeza hapo ni what if mashine ndiyo itakayotumika? Na vp kwenye kujenga 42.5N ni sawa pia au kuna nyingine? Ninatanguliza shukrani za dhati.
Kwa kifupi ni kwamba hizo N na R baada ya namba zinaonyesha uharaka wa cement ku gain strength na kuganda.

Mfano kama una kazi kubwa na unatumia mashine ku mix zege na unataka cement/zege iwahi ku ganda ili utoe formwork haraka basi unaenda na cement yenye R... mfano 42.5R ..hii R ina maanisha "rapid" au rapid strength gain!!

Sasa yenye N ni kinyume cha yenye R!!

Sasa kama unatumia mikono na mafundi wako hawana spidi basi ukitumia cement yenye R utajikuta zege imeanza kuganda wakati bado hawajamaliza kumwaga.

Ila kama una kazi ndogo ndogo unaweza tumia yeyote, iwe R au N lakini kama bei ziko sawa nenda na namba 42.5 yenye namba yeyote na sio 32.5!!

NB: Hakikisha unatumia cement ambayo haijakaa siku 30 dukani tokea siku imetoka kiwandani.. ukitaka kujua tarehe ya kutengenezwa angalia kwenye mfuko utaiona...
 
Nmekusoma vzr mkuu ubarikiwe sana.
 
Natarajia kupiga plaster muda wowote kuanzia sasa, wanamalizia Blundering baada ya hapo plaster inaendelea. Naomba kuelimishwa cement nyeupe inatumika wakati gani? Nakusudia plaster yangu ipigwe ile ya kuteleza kabisa na ikiwezekana wachanganye na chokaa. Naomba ushauri ndugu zangu asanteni
 
Back
Top Bottom