Kwa wale jobless wenzangu tusaidiane ni mbinu Gani unayotumia kujipatia kipato cha kuendesha maisha

Nakuunga mkono mkuu, alitakiwa aulize mnafanyaje ili muweze kuendesha maisha, ila ukishasema mnafanyaje kupata kipato wewe sio jobless tena, labda kama alikua anazungumzia kazi za kuajirilwa.
Kam umemuelewa alichomaanisha sas unahaja gani ya kutoa ufafanuzi badala ujibu kulingana na ulivomuelewa
 
Kam umemuelewa alichomaanisha sas unahaja gani ya kutoa ufafanuzi badala ujibu kulingana na ulivomuelewa
Ni lazima ujue kutumia lugha vizur mkuu, ukijifanya mjuaji unaweza ukajibu kitu ambacho mwenzio hakuwa anakusudia.
 
WaTanzania sisi Mungu katujalia ubinafsi ,ukimuuliza mtu au tajiri unapataje hela hataishia kukudanganya au jibu fupi utaambiwa ahahaaa ni misheni town tu.

Ss hiyo misheni town hautakaa ujue ni misheni town ipi maisha😂😂😂😂
 
Nakumbuka nilivyokuwa jobless nilikuwa nashinda getto tu washkaji wananiachia buku ya kula, sometimes no, nikaona hapa kama nawapa mzigo na maishs yalikuwa magumu kweli

Nikapata sehemu ya kujitolea kuhudumu bar bure, (kumenya viazi, kuosha glass, kufuta na kupanga vinywaji n.k) malipo yalikuwa ni msosi wa mchana na wa usiku, ilikuwa mwaka 2011
Nimeipenda courage yako.
 
Hebu tusaidiane ndugu zangu kwa wale jobless ni mbinu gani unayotumia kujipatia kipato cha kuendesha maisha

Hebu tupeane maujuzi ni mbinu unazotumia ambazo na sisi jobless tukizutumia tunaweza pata akiri na uwezo wa kujipatia kipato hata kama ni kidogo

Ukiwa jobless unadharauliwa hadi na watoto wadogo aisee, watu wanatupa ushauri anza biashara sa mtaji unapata wapi wakati ukiwa jobless hata buku ni kaz kupata, utaskia uza simu nan atannua simu yako ya kuunga unga na rubber band kioo kimepasuka balaa Mungu atukumbuke tuu
 
Amina
 
Nilikaa kitaa miaka 2 bila kazi. Application hazijibiwi. Ukipata interview lakini unakuta kwenye kuitwa kazini haumo. Kumbe mchawi ni kutafuta namba ya HR na kumpa pesa. Inshort 99% ya ajira siku hizi ni za kununua.
 
Hahahahahahahaha poleni
Uzeni sigara mitaa ya posta kkoo mjini mjini ideas zitakuja tu na utapata connection
 
Au fungueni account xvideos,n.k huenda vi dollar hukosi
Au rudini home mkapumzike kdg
 
Nilikaa kitaa miaka 2 bila kazi. Application hazijibiwi. Ukipata interview lakini unakuta kwenye kuitwa kazini haumo. Kumbe mchawi ni kutafuta namba ya HR na kumpa pesa. Inshort 99% ya ajira siku hizi ni za kununua.
kwa hiyo mkuu mambo yakatiki bila jasho
 
Kaka wengine ndipo tulipojifunza kuna kaz zinahitaji nguvu tuu ili kutoka, na ukipata hela kidogo kuwa mbunifu wa biashara, huku kaz ngumi hujaiacha. Mi niliingia machimboni baada ya kumakosa shule stil mpaka sasa huwa narudi mjini nasotea ajira ila nkiona znazingua naginhiwa tena chimbo, kuna wakat napata kias kikubwa nafungua biashara ila nikitetereka sichoki kujaribu. Mfano kaz hii imenizungusha mikoa 15 ya tz na nchi 3. Kiukweli ni ngumu ila urahis wake ni kwamba haiitaji elimu kubwa ili uifanye
 
Back
Top Bottom