Kwa wale introverts, anti social, na shy people maisha yako ya chuo yalikuwaje? Vipi mtaani kukoje?

Natumai mko wazima na wale wenye changamoto nawapeni pole niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi kwanza sijijui kama ni introvert au anti social au nina vyote kwa pamoja nakumbuka maisha yangu ya chuo yalikuwa mtihani mkubwa sana vitu kama discussion presentation sikuwa napatana navyo kabisa sikuwai kushiriki discussion kazi yangu ilikuwa ni ku type assignment kitu kilichopelekea niwe na marafiki wachache

Baada ya kumaliza na kuwa na familia nilifanikiwa kupata mwanamke aliye tofauti na mimi yeye yuko social so vitu vinavyohusu changanyikeni kama misiba harusi nk mimi naonekana tu alafu natoweka hizo mambo anamaliza yeye hii ndio pona yangu.

Hii hali ilinifanya nisipange nyumba, yaani kitu cha kwanza kufanya kwenye maisha yangu ya baada ya masomo ni kujenga ili tu nikiwa natoka kazini najifungia nyumbani namshukuru sana baba yangu alinisapoti pakubwa sana nilikuwa nawaza sana mimi ni mtu wa aina gani ila nimezoea na wachache wanaonielewa ndio ninaoenda nao.

Tupe experience yako.
Mkuu

Ninateseka Sana.. Nimejaribu Mara kadhaa imeshindikana... Hapa chuo kinachonitesa zaidi ni discussion na presentation.. Ila paper huwa nafanya vizuri Sana


Natamani kubadilika lkn nashindwa.. Nimejaribu Sana... Ndugu wa familia wengi wanasema Mm ni mpole na sijichanganyi.. Imefika mahali mpaka nimewekewa kikao

Majirani pia wanadai ninajiona na sishirikikiani nao kwakuwa nasoma chuo lkn Hali yetu ya kimaisha ni ya chini.. Roho inaniuma Sana

Thanks to my mom ambaye kila siku amenisupport kutokana na hali yangu


Nimeandika kwa uchungu Sana mkuu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu

Ninateseka Sana.. Nimejaribu Mara kadhaa imeshindikana... Hapa chuo kinachonitesa zaidi ni discussion na presentation.. Ila paper huwa nafanya vizuri Sana


Natamani kubadilika lkn nashindwa.. Nimejaribu Sana... Ndugu wa familia wengi wanasema Mm ni mpole na sijichanganyi.. Imefika mahali mpaka nimewekewa kikao

Majirani pia wanadai ninajiona na sishirikikiani nao kwakuwa nasoma chuo lkn Hali yetu ya kimaisha ni ya chini.. Roho inaniuma Sana

Thanks to my mom ambaye kila siku amenisupport kutokana na hali yangu


Nimeandika kwa uchungu Sana mkuu



Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana kijana wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni introvert konki. Wakati nilipokuwa chuoni nilisemwa nakusemwa mpaka basi, tena waliokuwa wanaongoza kunisema ni wanaume (waliona sina time nao). Na mpaka leo ninasemwa na hao hao wanachuo wenzangu. Baadhi ya vitu nilivyosemwa ni,
Nina dharau najikuta Mzungu
Najiona mzuri sana, uzuri haukai milele utaisha tu
Nina shida psychologically
Ninajishaua, nitakuja kupata shida etc
Kwasababu hii hata uniseme nini huniumizi wala sijali, nimekuwa sugu haswaa, ndio maana unaweza ukanitukana wewe na ukakasirika wewe mwenyewe.
Sawa mimi ni introvert lakini sipo shy hata kidogo. Nikisimama mbele ya watu ninaongea vizuri nakupangilia hoja zangu mpaka utafurahi. Ninachochukia tu ni kufanya social interactions na watu hasa hasa ambazo hazina maana. Nina kaa ndani muda mwingi na kutoka ni usiku ili nisionekane kiurahisi.
Napenda kuwa introvert kwasababu pamoja na disadvantages zote kuna advantages nyingi kama vile
Kutokuwa mnafiki
Na ninayoipenda binafsi kuliko zote ni deep thinking ambayo imeweza kunidevelop sana especially creatively.
Introverts, extroverts etc wote tuna umuhimu na tunahitajika katika maisha hapa duniani kwahiyo tuvumiliane tu.
Sorry mkuu hivi hua ww ni ke?
 
Mimi ni introvert na najivunia kuwa hivyo.

Being an introvert doesn't mean that you'll be antisocial or stressed.

Changamoto ambazo tunazipata sisi introvert ni kwenye mahusiano na watu.
Hatupendi kukaa na watu

-Hatupendi story za kipuuzi,kama udaku na kusema watu,tunataka story zenye facts.

-Hatuna marafiki.

-Kama tukitaka kwenda club tunaenda club tunaenda wenyewe na hatuchezi mziki tunasikiliza tu.

-Mtu akija kukutembelea unatamani aondoke,sio kwamba humpendi basi tu unakuwa hupo comfortable.

-Hupendi kupokea simu,simu ikiita unaiangalia , halafu unamtext muhusika

-Unapenda sana text kuliko calls

-Muda mwingi upo kichwani mwako
Kusema kwamba introverts hatuna marafiki si kweli. Marafiki tunao sema tunachagua sana wa kuwaita rafiki. Mengine umesema vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni introvert lakini kwenye ulazima naweza kujichanganya na kundi la watu. Kwenye discussion sipendi kuwepo ila ikinibidi basi nitahakikisha nashiriki kikamilifu sababu sipendi kukaa kivivu. Naweza sema wakati mwingine nakuwa kama extrovert.

Katika kutaka kujifahamu zaidi nilifanya personality test ya Myers & Briggs na nikaangukia kwenye INFJ-T. Kwa sehemu kubwa sifa zake ndizo ambazo ninazo. Napenda jinsi nilivyo ingawa kuna mambo ambayo yananiwia vigumu sana kuyafanya vinginevyo nijilazimishe.
Upo safi mkuu hiyo test huwa naiikubali. Mimi ni introvert ila hii test imenisaidia kubalance kidogo japo kuna mambo najua hayataweza kuchange.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi by nature ni introvert ila maisha yamenifanya nibadili baadhi ya tabia, zamani nilikua kila jambo nalifanya mwenyewe sitaki kampani na mtu ila now maisha yanataka kujichanganya na watu ili kupata chochote kitu sio kama zamani.
Tabia nilizonazo mpaka leo ni hizi
1. Sipendi kukaa kupiga stori na watu muda mrefu
2. Sipendi kusikiliza watu wakiongea mambo yasiyo na faida kwangu au hayamake sense.
3. Napenda muda mwingi kukaa peke angu huku nikisikiliza mziki, nikisoma vitabu na stories au kubuni vitu mbalimbali (DIY)
4. Mpaka umri wangu huu sina rafiki wa kudumu
5. Sipendi sana kuongea na simu muda mrefu au kuchat sana. Mtu anaweza akapiga simu kama sina mood ya kupokea basi naingalia tu.
6. Sipendi kuzoeleka na watu
7. Sipendi kuwanyenyekea watu au kunyenyekewa
8. Ni mbishi pia yaani msimamo wangu hadi ubadilike basi kuna jambo limetendeka
9. Kwenda outing napenda niende peke angu, napenda kutembea sehem zenye mandhari ya asili.
10. Sipendi kuishi maeneo yenye kelele, napenda kusikiliza muziki na kuangalia videos ambazo hazipendwi na wengi.
11. Starehe yangu kubwa ni kuendesha gari tena humo kwenye gari niwe peke angu nifungulie mziki sauti kubwa nifunge vioo then ndo nainjoi.
Je mimi bado ni introvert?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom