Kwa wale introverts, anti social, na shy people maisha yako ya chuo yalikuwaje? Vipi mtaani kukoje?

KING 360

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,003
5,176
Natumai mko wazima na wale wenye changamoto nawapeni pole niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi kwanza sijijui kama ni introvert au anti social au nina vyote kwa pamoja nakumbuka maisha yangu ya chuo yalikuwa mtihani mkubwa sana vitu kama discussion presentation sikuwa napatana navyo kabisa sikuwai kushiriki discussion kazi yangu ilikuwa ni ku type assignment kitu kilichopelekea niwe na marafiki wachache

Baada ya kumaliza na kuwa na familia nilifanikiwa kupata mwanamke aliye tofauti na mimi yeye yuko social so vitu vinavyohusu changanyikeni kama misiba harusi nk mimi naonekana tu alafu natoweka hizo mambo anamaliza yeye hii ndio pona yangu.

Hii hali ilinifanya nisipange nyumba, yaani kitu cha kwanza kufanya kwenye maisha yangu ya baada ya masomo ni kujenga ili tu nikiwa natoka kazini najifungia nyumbani namshukuru sana baba yangu alinisapoti pakubwa sana nilikuwa nawaza sana mimi ni mtu wa aina gani ila nimezoea na wachache wanaonielewa ndio ninaoenda nao.

Tupe experience yako.
 
Tunatukanwa Sana, tunasemwa ni watu wa majivuno wasiopenda kushirikiana na wenzao lakini yote hayo si kweli. Tunasemwa ni watu wa kujiskia/wazito na mengineyo.

Shule ilibidi iwe sehemu ya kufundisha mambo muhimu kama haya katika maisha. Maisha yanayo siri kubwa muhimu yatafiti uyafahamu hapo ndio utaweza kuishi.

Half of what we have been fed are lies.
- Sérgi
 
Kama wewe ndo ulikuwa unatype assignment za makundi basi umewafelisha sana wenzako, post yako umetype hovyo sana, na hii ni yako sipati picha hizo assignments kutoka kwa lecturers zilikuwaje, hizi degree hizi yaani basi tu Mungu atusaidie.

Lakini nakutakia mwaka mpya wenye mafanikio, na usikubali mwaka 2020 upite ukiwa bado unatype hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POINT OF CORRECTION.

Watu wengi huwa wana-misuse neno anti-social.

Maana halisi au tafsiri halisi ya mtu ambaye ni anti social ni mtu ambaye hajali mambo ya watu wengine au hajari hisia za watu wengine yeye anafanya vitu vyote kwa manufaa yake.


Mfano wa hawa watu ni matapeli.

Watu wengi wanapenda kulitumia neno antisocial kama mtu ambaye hapendi kuongea au kuchangamana na watu kitu ambacho sio kweli.

Mtu anti social anaongea na watu vizuri tu as long as anafaidika kitu ni aina flani ya watu ambao wanaweza kuja wakawadamganya hata ndugu wa marehemu ili wapige rambirambi.
 
Mimi ni introvert na najivunia kuwa hivyo.

Being an introvert doesn't mean that you'll be antisocial or stressed.

Changamoto ambazo tunazipata sisi introvert ni kwenye mahusiano na watu.
Hatupendi kukaa na watu

-Hatupendi story za kipuuzi,kama udaku na kusema watu,tunataka story zenye facts.

-Hatuna marafiki.

-Kama tukitaka kwenda club tunaenda club tunaenda wenyewe na hatuchezi mziki tunasikiliza tu.

-Mtu akija kukutembelea unatamani aondoke,sio kwamba humpendi basi tu unakuwa hupo comfortable.

-Hupendi kupokea simu,simu ikiita unaiangalia , halafu unamtext muhusika

-Unapenda sana text kuliko calls

-Muda mwingi upo kichwani mwako
 
68 Reactions
Reply
Back
Top Bottom