Kwa wale ambao wakiingia kwenye swimming pool wanatembea

Huwa najisikia vibaya sana ninapoenda hoteli yenye swimming pool naishia kutembea kwenye maji na kucheki wengine wakiogelea.. natamani kujifunza kuogelea maana naweza zama siku yoyote kwenye pantoni nikashinda kujitetea maana pia napandaga panton karibu kila wiki mara mbili na kuogelea sijui ebu tupeane uzoefu ni wapi naweza jifunza ogelea kwa dar.
Nitafute Pm ntakufundisha almost free na utajua
 
Ni kweli mkuu, ila je wapi pakujifunzia??

kama upo dsm na unataka kujifunza kuogelea kwenye swmming lisilo na watu wengi basi nenda ndege beach mbweni... hasa weekdays unaweza kujikuta kwenye swiming pool upo peke yako na mwalimu wako no interactions wala nini
 
Msema kweli ni mpenzi wa mungu, kiukweli mbwembwe za samaki siziwezi wazee wa kazi. Kila nikijitahidi msuli unakaza. Nahitaji masta wa ku swim anifundishe, akiwa mrembo itapendeza zaidi Khantwe
 
Duh! Kweli mazingira uliyokulia yanaathiri kila kitu! Mitoto niliyokuwa nayo mimi na mimi mwenyewe lazima tushangae kweli?! Hata swimming pool?! Binafsi wala sithubutu kuogelea swimming pool manake nina uhakika nitaleta misifa ya utotoni na kila mara nitaishia kujibamiza kichwa!

Ila bhana kuogelea kama hujajua wakati wa utotoni ambapo hufahamu vizuri nini maana ya hatari, ukubwani inakuwa taabu kidogo!
 
Msema kweli ni mpenzi wa mungu, kiukweli mbwembwe za samaki siziwezi wazee wa kazi. Kila nikijitahidi msuli unakaza. Nahitaji masta wa ku swim anifundishe, akiwa mrembo itapendeza zaidi Khantwe
Kuogelea ni rahisi sana kujifunza wakati upo mdogo kuliko wakati umeshafahamu maana ya kufa! Mi wakati nipo primary hadi secondary, uniwekee mkwanja wa kutosha Ferry upande wa Kigamboni halafu uniambie niufuate kutokea Ferry ya Magogoni; wallah ningeufikia!!

Lakini siku hizi wakati najua nini maana ya kifo, lazima iwe mtihani! Tena na hivyo misuli imeshakomaa, ndo kabisa!!
 
Nshajifunza bila mafanikio sijui nakosea wapi, nikilala kwenye maji sielei yani nazama kama jiwe, nikiinuka masikio yameingiwa maji naona kerooo
Hivi si ndo wewe yule ulisema kuna Youtube video, au?! Nilitaka kukuambia achana na hiyo mambo, huwezi kujifunza kuogelea kwa Youtube! Unaweza kutumia Youtube kama tayari unajua kuogelea lakini unataka uwe unaogelea as a professional!
 
Back
Top Bottom