Kwa wale ambao hamjapata likizo njooni tufarijiane.

Zekidon

JF-Expert Member
May 29, 2013
1,891
1,225
Kwa wale wenzangu na mimi ambao likizo imeota mbawa, mje hapa, hii ni thread maalum ya kufarijiana.

Inawezekana kabisa kua wewe hapo ndio umebaki mwenyewe hapo ofisini kwenu kulinda jengo, wenzako wako huko makwao wanakula bia na ndafu.

Inawezekana kabisa labda hukuona umuhimu wa kuchukua likizo na kuamua kubaki kwakua mambo hayakwenda vyema hivyo huna mpunga wa kwenda kufanya showoff huko kijijini kwenu kama kawaida yako.

Inawezekana kabisa kua utaratibu wa ofisi unakutaka ubaki kwa lazima kwakua mwaka uliopita wewe ndiye uliyekwenda likizo wenzako wakabaki.

Unaboreka kazi haziendi, una mawazo kila saaa.

Hapa ndipo mahali sahihi pa kutoa stress zako zote, na kuwa huru.

Karibuni wahanga wote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom