Kwa wakubwa tujadili hizi kaulimbiu za serikali toka enzi za mwalimu

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Kwa wale wazee mnaweza kukumbuka enzi ambazo mzee ruksa aliingia madarakani, alikuja na fagio la chuma!

Hiyo ilikuwa just baada ya kupokea kijiti toka kwa Mwl. ambaye hata Mwl. wakati wa utawala wake bado alikuwa akisumbuliwa na wahujumu uchumi!

Je baada ya ufagio wa chuma taifa lilitakata?

Au walizaliwa wachafu wapya ndani ya jumba kuu na mfagiaji uchafu ukamrukia na kumtapakaa!

Raisi mpya alikuja kufagia uchafu aliouacha mwl. Lkn hadi anaondoka mjengoni, jumba lilikuwa chafu kuliko alivyolikuta!

Je, fagio la chuma lilikwama wapi?

Ni kweli hizi kampeni za zima moto huleta tija?

Nadhani issues za majipu, na fagio la chuma zinahitaji ulinganifu!

Wakongwe tunaomba mtupe experiences zenu juu ya sababu kuu za ufagio wa chuma, mafanikio na changamoto za ufagio!

Kisha sisi wa leo, tutapata picha angalau haya majipu yatatupeleka wapi!
 
Mzee Mwinyi hakuwa na elimu kubwa lakini alikuongoza nchi kwa hekima. Yapo mengi yalimshinda lakini huyu mzee alikuwa na subra. Hekima na subra uenda pamoja.

Ukiona rais hana subra basi waweza kusema kwamba hana hekima.
 
Kwa wale wazee mnaweza kukumbuka enzi ambazo mzee ruksa aliingia madarakani, alikuja na fagio la chuma!
Hiyo ilikuwa just baada ya kupokea kijiti toka kwa Mwl. ambaye hata mwl. wakati wa utawala wake bado alikuwa akisumbuliwa na wahujumu uchumi!
Je baada ya ufagio wa chuma taifa lilitakata?
Au walizaliwa wachafu wapya ndani ya jumba kuu na mfagiaji uchafu ukamrukia na kumtapakaa!
Raisi mpya alikuja kufagia uchafu aliouacha mwl. Lkn hadi anaondoka mjengoni, jumba lilikuwa chafu kuliko alivyolikuta!
Je, fagio la chuma lilikwama wapi?
Ni kweli hizi kampeni za zima moto huleta tija?
Nadhani issues za majipu, na fagio la chuma zinahitaji ulinganifu!
Wakongwe tunaomba mtupe experiences zenu juu ya sababu kuu za ufagio wa chuma, mafanikio na changamoto za ufagio!
Kisha sisi wa leo, tutapata picha angalau haya majipu yatatupeleka wapi!
Narrow as well as wrongly fabricated & illogically connected
 
Narrow as well as wrongly fabricated & illogically connected
Wasaidie kuonyesha wapi wamekosea kuunganisha mantiki na saidia kuweka sawa ili watu wapate faida. Otherwise, wewe ndio utakuwa wa hovyo zaidi na siyo huyo mleta uzi ambaye ameomba kujuzwa kuhusu hizo tawala mbili.

Kama hujui ni vema ukapita wima, umenifanya nimeandika, sikutaka kufanya hivyo.
 
Uelewa wako unatokana na kiwango cha elimu halisi iliyopo ndani yako, nielewe kuwa elimu halisi uliyonayo ndani yako! Umma wa nyerere na mwinyi huwezi kuufananisha na umma wa sasa, upinzani wa kipindi kile huwezi kuufananisha na upinzani wa leo!
 
Ahsante umenisaidia!
Naona jamaa amekurupuka wapi sijui!
 
Uelewa wako unatokana na kiwango cha elimu halisi iliyopo ndani yako, nielewe kuwa elimu halisi uliyonayo ndani yako! Umma wa nyerere na mwinyi huwezi kuufananisha na umma wa sasa, upinzani wa kipindi kile huwezi kuufananisha na upinzani wa leo!

Hii ni historia!

Haifundishwi popote, labda husomwa lkn hata maandiko pia huwa hayatoi picha yote in details labda basic information approximately to uhalisia!

Lakini humu JF kuna watu wameishi hiyo historia, watasema yaliyoandikwa na yasiyoandikwa, ni kama tunaoishi zama hizi za majipu, yapo written na unwritten majipu au process za utumbuaji!

Ninachoomba kufahamu kwa hii elimu ndogo niliyonayo ni juu ya process za ufagio na outcome!

Hakuna anayelinganisha nyakati za utawala, hapa ninaomba watu wasaidie kufanya tafakari za mikakati ya kupambana na ubadhirifu ktk taifa!
 
Umesahau Mr Clean (Ben) alianza na askari wa miavuli akamaliza akiwa fisadi kuliko wote
 
Fagio haliwezi kufagia lenyewe..fagio lilikosa mfagiaji...ila kwa sasa, majipu yamepata mtumbuaji
 
Narrow as well as wrongly fabricated & illogically connected

Kuwa narrow ndiko kulikoniongoza kuomba msaada wa "wakubwa" waliouishi mfumo wa ufagio!

Kwamba nimefabricate sidhani, labda kama unaweza kupoint ni eneo lipi hasa! Mzee ruksa alipotoka hali pia haikuwa shwari sana! Sijui kama idadi ya wabadhirifu aliowakuta toka kwa Mwl. na aliowaacha yeye wakati anatoka uwiano ulikuwaje?

So far sijui kama kweli ufagio na jipu vipo connected kiasi hicho au la! Ila baada ya kupata taarifa za waliouelewa vema ufagio wa chuma tutakuja elewa kama connection yake ipo logical or not!
 
Serikali ya sasa ndiyo itakuwa ya ovyo kuliko zote zilizowahi kutokea hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom