Kwa wakazi wa Sengerema, saidieni Prisca Michael amepotea

kambagasa

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
2,261
1,785
Ni binti amepotea kwa kutelekezwa na shangazi yake machimboni (nahifadhi jina la eneo). Anaitwa Prisca Michael

Anatokea: Mchangani (visiwani) Sengerema. Amemfahamu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mchangani kwa jina la Mwalimu Irene.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mchangani: jina moja tu Simon. Ninachohitaji ili kufanikisha kumfikisha kwao ni namba za simu kituo cha polisi Sengerema ama mwenyeji yoyote wa Mchangani hasa namba ya simu ya mwenyekiti wa kijiji ama mkuu wa shule Mchangani.

Ninaye kwangu (kwenye familia yangu).

Nimemchukua leo.
f69575deb28569f107b6f2a2dc365b06.jpg
7edb737891d10df3674ed5c2ef9fa984.jpg
86fee22db46cb2860769e74e549b5e1b.jpg
32a7f0eb2f5424a95fb1f0d806d92342.jpg
 
Endelea kuishi nae tu mkuu maana tayari umeshauzihirishia umma kwamba mtoto yuko kwenye mikono salama.
 
Duh?fanya hima jamaa wasine fikiria umejitwaalia mke mwanafunzi.
 
Umesha pata contacts za mkuu wa shule??? Nikusaidie!!???
Nilimchukua ofisi ya kijiji nikiwa na mke wangu ndg Dagii. Ndugu yoga bado sijapata please nisaidie number ili leo nimsafirishe. Comment yako sikuiona jana huenda imefika nikiwa nimelala. Nasubiri kwa hamu.
 
Sasa kama alipotea kwa kutelekezwa unampeleka tena kwa huyo aliyemtelekeza, kwa nini usiende kumuhamisha shule ukae nae, Mungu atakubaliki
 
Alichukuliwa na shangazi yake kutoka kwao ambaye anaishi machimboni ndipo anavyodai akamtelekeza stand na kuondoka na nguo zake (hivyo unavyomuona ndo nguo aliyonayo hata viatu hana) . Kwa kifupi huenda alitoroshwa na mtu na kutelekezwa, nilimchukua ili tu awe salama kwani huku machimboni kuna watu wenye roho za kishetani usipime. Kukutoa kafara ama kubaka ili wafanikishe mazindiko yao hawaoni shida. Pamoja na ushauri wako lkn ni vizuri ndugu zake wakafahamu.
 
Kaka nakuomba Fanya haraka umpeleke kwao au nenda kwa mkuu Wa wilaya kamkabizi ndugu yangu,then kama utamtaka umchukue sehemu salama,Watanzania wepesi sana sisi wakulaumu na kusahau haraka ,
 
Sawa kabisa, nasubiri kuna mdau hapo juu ameahidi kunipatia namba za mwalimu mkuu wa shule Mchangani, lengo langu nimkatie tiketi apokelewe kwao katika mikono salama. Nikikosa nampeleka kituo cha polisi then atasafirishwa bure hadi Sengerema kituo cha polisi na wao watamfikisha huko Mchangani japo atapitia suluba na watu wenye mitazamo na mioyo tofauti.
 
Sawa ndugu maana likitokea lakutokea utasaga meno tuu
 
Back
Top Bottom