kwa wakatoliki:Kumcha mwenyezi mungu ni chanzo cha maarifa!

Status
Not open for further replies.
Ntolee uharisho wako hapa..lini na wapi umeskia padri wa kanisa katoliki kakamatwa "redihendedi" na madawa kama sio hao maaskofu wenu wa makanisa ya kisasa..acha kubwata kama umebanwa na NNYA..mtu mzima hovyo..too bad umeniharibia siku yangu..Mpssxxyy

Nisamehe bure sikujua kama uko kwenye siku "zako"....!

kwa hiyo muumini wa kawaida akiamua kufanya ibada kwa style hiyo ya kugala gala na kujinyennekeza kwa mungu ruksa au?
 
Hua wanafanya hivyo kwenye ibada ya upadrisho kwa wale mashemasi wanaoingia kwenye upadri na pia siku ya good friday japo co waumini wote..
 
Hapo wanakua wanamnyeneykea nani hasa mungu na huyo jamaa mbele mwenye kikofia chekundu?kama jibu ni mungu basi huo ni ucha mungu...!

Msikitini mkiinama kuelekea KIBRA halaf SHEIKH yuko mbele yenu, ina maana mnamsujudia SHEIKH? Mungu/Allah yuko `everywhere`and it doesn`t make sense kusema unamuabudu Padre/Sheikh (yeye ni kiongozi tu wa Swala/Misa).Upo hapo chief?
 
wapendwa,

hapo mashemasi wanapewa daraja takatifu la upadre! tukio lililo katika formalities za ibada za upadrisho na sio lazima iwe ndio "ucha Mungu". ucha Mungu uko moyoni mwa mtu na sio kwenye kanzu nyeupe na kulala kifudifudi kwenye zuria linalometameta mbele ya maaskofu! hiyo ni ishara ya unyenyekevu na inakuwa na maana zaidi kama unyenyekevu huo uko mioyoni mwao, na sio hapo mbele ya kamera pekee.

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!

Naona wakatoliki wanakukosesha raha kuliko hata Shetwani himself!

Hivi unyenyekevu unaouoenesha ki moyoni tu ni upi? Na wewe ni mortal being utaonaje mioyo ya watu?
Ndio maana wanasema hata uwe na imani ya kuhamisha milima kama huna upendo ni bure, na upendo hutafsiriwa kwa matendo.

Hao mashemasi, wameacha normal life (kuwa na familia zao wenyewe) wameamua kumtumikia Mungu, yet unataka uione mioyo yao, wewe ni nani? Si umuachie Mungu ndio mwenye jukumu la kuhukumu!
 
Hii thread inataka kuleta kukandia imani za watu ni bora busara ikapewa kipaombele
 
Kama umeandika kwa wema ubarikiwe, na kama umeandika kutafuta comment Mungu akusamehe maana hujui ufanyalo
 
Nimeupenda ucha mungu wa aina hii toka kwa waumini wa kikatoliki....ama hakika kumcha mungu ni chanzo cha maarifa...................

Kumbe sio wakatoliki peke yao bwana hata waanglikana nao wanayo hii style lol..nimeipenda sana hii,ni kielelezo cha utiifu wa kutukuka mbele ya madhabahu....

umenichekesha sana umetoa wapi hilo jibu?

Majibiu dizaini hii ndio dawa ya vijana wahuni walijazana humu jamvini siku hizi wakidhani huko waliko sasa na sisi hatukupitia,hebu fuatilia huko nyuma utajua kwanini nilimpa kauli ya kifedhuli kama hiyo ambayo sio kawaida yangu kwa wanaonijua sema kijana alitaka kuleta sanaa zake uchwara kwenye jumba la sanaa ndio nikaona nimrudi haraka kabla hajanivunjia heshma!
 
Katika Makanisa ya Catholic na Anglikana, sifahamu juu ya KKKT, kupewa madaraja matakatifu si jambo la mzahmzaha kama ilivyo kwa makanisa ya kisasa ambapo mtu analala na kuamka kesho kujitangazia kuwa yeye ni shemasi, askofu, mtume, au Nabii...

Kwenye makanisa ya RC na Anglicana, ni mchakato mrefu ambapo mtu ni lazima kwanza awe amesoma filosofia, teolojia na malezi kwa miaka ya kutosha, hukua akichunguzwa kwa ukaribu, na ndipo hatua ya mwisho, mbele ya waumini wote inakuja hatua ya kuapa kiapo kikuu cha kujitoa kwa kaz ya Mungu, ambapo kulala chini kwa namna hiyo ndiyo ishara kuu.

Wanaofunga ndoa wanavishana pete mbele ya kadamnasi, lakini hawa kwa vile ni waseja walioamua kumtumikia Mungu, wao ishara yao ni kulala chini, wala haina tafsiri za zingine!
Haya maelezo ya wasiojua ni kukimbiza upepo, na suala la imani kama alivyohoji Miss Judith, hilo ni baina ua muapaji na Mungu wa mbinguni!
Tusibeze vitu tusivyovielewa maana zake!
ASksanteni.
 
Tunashukuru kwa ufafanuzi lakini punguza hisia,nani kakwambia watu wanabeza imani ya mtu?lengo hapa ni kuelimishana wala si kubeza ama kukejeli na kujeruhi hisia za waumini wa imani fulani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom