KWA WAJUZI WA SHERIA ZA KAZI/NYINGINEZO HII IMEKAAJE

naomba kazi

JF-Expert Member
Mar 5, 2019
253
213
Baada ya kuangaika sana kutafuta kazi pasipo mafanikio yeyote atimae nikaanza kusaka sehemu ya kujitolea japo nipate ela ya chai na nauli ila wapi

Atimae nikaamua kutafuta sehemu ya kujitolea bure kabisa pasipo kulipwa chochote

Nikapata kampuni moja xxxxxxx iliyopo dsm

Hii kampuni ikasema kuwa itanichukua ila ntatakiwa kujitolea kufanya kazi kwa mwezi mmoja bure pasipo malipo yeyote

after hapo ndio wataangalia waniajili au wasiniajili ila mshahara wao hauzidi laki 6

Baada ya interview na kufanikiwa kupita, wakata barua ya serikali za mtaa ninapotoka na picha zangu mbili, nikapeleka na Nikakubaliana nao kwa moyo mkunjufu kabisa.

Wakanipa mkataba wao wa page kama nyingi nyingi kidogo
(mkataba wa kufanya kazi kwa huo mwezi mmoja)

Katika mtaba hule kuna kipengele kinasema ivi ( ambapo ndio kiini cha uzi wangu)

1. Endapo utatokea kuacha kazi ndani ya huo mwezi mmoja, nitatakiwa kulipa faini ya sh milion 2

2. Endapo utatokea kuacha au kuachishwa kazi baada ya kuajiliwa hauruhusiwi kufanya kazi sehemu nyingine yeyote ile ndani ya jamuhuri ya muungano inayofanana na kazi katika kampuni ile.

3. Ni marufuku kutoa siri za mkataba ule sehemu nyingine yeyote ile

Kipengere namba 1 na 2 ndio ntaka kupewa ufafanuzi kulingana na hali hii

Mimi nimepata sehemu nyingine na nimeambiwa nikaanze jumatatu kazi...

Na hapo kwenye iyo kampuni bado mwezi sijamaliza, je kisheria imekaaje nikiacha naweza kufungwa, naweza kutengenezewa zengwe au

Naombeni mawazo yenu wakui

Asanteni

sent using bombadia
 
utalipa faini ya millioni 2, si ulisha saini na kurudisha (ikiwa na maana umekubaliana nao)
 
Back
Top Bottom