Kwa wajuzi wa sheria mtazamo wenu juu ya hili?

scientificall

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
454
314
Baada ya hakimu( mahakama ya mwanzo) kutuita mimi na mlalamikaji wangu kwa kesi ya wizi. Mlalamikaji alipewa mda wa kujieleza juu ya shida yake na akagusa yafuatayo ambayo kimsingi ni uongo.

Mshitaki alimueleza hakimu kuwa kesi ikiwa polisi, polisi walipoteza jalada lake na kumwambia aandike maelezo mengine.

Aidha mshitaki alisema baada ya kupewa mpelelezi wa kesi polisi(mpelelezi) alienda mpaka eneo husika ambapo kimsingi sehemu wizi ulipotendeka hakuna dalili zozote za kudhibitisha kuwa wzi ulitendeka.

Baada ya hapo mshitaki mbele ya hakimu akasema baada ya ukaguzi mpelelezi alimuomba kiasi cha pesa ili aweze kuifatilia kesi yake, mshitaki akakataa na kusema hataki kutoa rushwa na baadae akaenda kwa R.C.O kulalamika kisha R.C.O akanirudisha mahabusu mimi mtuhumiwa na mpelelezi wangu.

Nikiwa namsikiliza anaongea kwa kutetemeka mshitaki wangu kwasababu anatambua ni kesi ya kutengeneza.
Kimsingi mlalamikaji alitoa maelezo tofauti 100% na maelezo aliyoyatoa polisi.

Nilipo pewa mda wa kumuuliza maswali mshitaki wangu alijitahidi kuyajibu lakini mengine yalimtoa nock out.

Kwa maelezo hayo juu je kesi hii inaweza kuwa na % ngapi za mtuhumiwa kushindwa kesi na kufungwa bila kosa au mshitaki kushindwa kesi kwa maelezo aliyoyatoa mahakamani?

Je kuhusisha maswala ya kuombwa rushwa na kumsababishia mpelelezi wa kesi kuwekwa mahabusu kwa mda kama alivyoelezwa hakimu haina adhari kwa mlalamikaji kutokana na tafsiri ya hakimu?.

Ushauri na muono wa suala hili wana jamvi.
Maswala ya kuombwa rushwa yote ni ya uongo wa kutengeza.
 
Back
Top Bottom