Kwa waislamu; Je, ni sahihi muislamu kutangaza biashara ya kitimoto?

LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,312
6,638
Samahani ndugu zanguni,kuna swala linanitatiza kidogo hapa nataka nipate ilmu na ufahamu zaidi ,kuna rafiki yangu yeye ni muislamu,ana biashara zake huwa anazifanya,sasa leo katika status ya whatsapp kapost tangazo la biashara ya kitimoto,anatangaza soko la mshkaji wake kuwa anauza kitimoto nzuri na mazingira ni masafi,wateja wakaribie..nimeshtushwa na nikamuuliza kwanza kama anatumia kitimoto?na je alichokifanya ni sahihi kulingana na imani ya dini yake?
Majibu yake ni kwamba yeye hatumii hiyo bidhaa,lakini pia haoni tatizo kwa maana amesaidia kutangaza soko la his royal friend,je yupo sahihi kwa alichokifanya kutokana na misimamo mikali ya dini ya kiislamu?lengo langu nataka kujua na kujifunza kitu kipya kutokana na hili,naomba kuwasilisha.
 
Niliwahi kuishi kwenye moja ya Islamic Country, na kuna baadhi ya super market zilikua zinauza hiyo kitu kwa uwazi kabisa na wakiwa wamegawa compartment kwaajili ya huduma kitimoto tu.
Hata nami nilipata kidogo mstuko kuona moja ya nchi yenye sheria ngumu za kiislam na hata kuchinja wakosaji inaruhusu biashara hiyo kufanyika wallah....
 
Hayupo sahihi na inaonyesha haijui mafundisho ya dini full stop.
 
Huyo jamaa yako unayesema ni SHOGA
Mimi namjua

Sent using Jamii Forums mobile app
Nasikitika kukutaarifu kuwa huyu mtu sio mwanaume ni mtoto wa kike lakini kazaliwa katika uislamu na amesomea dini hadi kuna kipindi alipelekwa kusoma Sudan kwa miaka si chini ya mitatu,ndio maana kanichanganya...
 
Samahani ndugu zanguni,kuna swala linanitatiza kidogo hapa nataka nipate ilmu na ufahamu zaidi ,kuna rafiki yangu yeye ni muislamu,ana biashara zake huwa anazifanya,sasa leo katika status ya whatsapp kapost tangazo la biashara ya kitimoto,anatangazo soko la mshkaji wake kuwa anauza kitimoto nzuri na mazingira ni masafi,wateja wakaribie..nimeshtushwa na nikamuuliza kwanza kama anatumia kitimoto?na je alichokifanya ni sahihi kulingana na imani ya dini yake? majibu yake ni kwamba yeye haoni tatizo kwa maana amesaidia kutangaza soko la his royal friend,je yupo sahihi kwa alichokifanya kutokana na misimamo mikali ya dini ya kiislamu?lengo langu nataka kujua na kujifunza kitu kipya kutokana na hili,naomba kuwasilisha..
Nguruwe ni haramu ktk uislamu,
Hivyo muislamu yeyote atakayefuga,kutangaza biashara ya nguruwe,kuuza dhambi zake ni sawa na aliyekula nyama ya nguruwe
 
Nasikitika kukutaarifu kuwa huyu mtu sio mwanaume ni mtoto wa kike lakini kazaliwa katika uislamu na amesomea dini hadi kuna kipindi alipelekwa kusoma Sudan kwa miaka si chini ya mitatu,ndio maana kanichanganya...
Nilisoma na kijana "muislam asiyejitambua" alikua na elimu ya dini kunizidi ila alikua anaonja kitimoto

Kuna raia wao wamezaliwa tu na mtindio wa ubongo automatically

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikitika kukutaarifu kuwa huyu mtu sio mwanaume ni mtoto wa kike lakini kazaliwa katika uislamu na amesomea dini hadi kuna kipindi alipelekwa kusoma Sudan kwa miaka si chini ya mitatu,ndio maana kanichanganya...
Hayuko sahihi.

Yuko ndugu yangu mmoja ye husemaga wazi kua akifika kwenye eneo la tukio na jamaa zake walaji hua anakulaga zile ndizi na rosti la mb oha mboga tu, nyama anawaachia wenzake. Huu ni uhuni uliopitiliza, hakuna kitu kama hicho. Ni sawa na useme eti uchukue za kununua halafu sababu unapiga na ndomu au sababu hujakojoa basi hujazini
 
Samahani ndugu zanguni,kuna swala linanitatiza kidogo hapa nataka nipate ilmu na ufahamu zaidi ,kuna rafiki yangu yeye ni muislamu,ana biashara zake huwa anazifanya,sasa leo katika status ya whatsapp kapost tangazo la biashara ya kitimoto,anatangazo soko la mshkaji wake kuwa anauza kitimoto nzuri na mazingira ni masafi,wateja wakaribie..nimeshtushwa na nikamuuliza kwanza kama anatumia kitimoto?na je alichokifanya ni sahihi kulingana na imani ya dini yake? majibu yake ni kwamba yeye haoni tatizo kwa maana amesaidia kutangaza soko la his royal friend,je yupo sahihi kwa alichokifanya kutokana na misimamo mikali ya dini ya kiislamu?lengo langu nataka kujua na kujifunza kitu kipya kutokana na hili,naomba kuwasilisha..
Hata kwenye ukristo wa kweli kitimoto ni haramu.Lakini watu wanakula na pia wanatangaza kwa ulafi wao

Huku Biblia imekataza kabisa na kusema:-

WALAWI 11:1-8

1 BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.
3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.
4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
7 NA NGURUWE, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu
8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu

Unaona !!
Watu hao watatupa tena maandiko mengine yafuatayo yanayokataza kwa uzito mkubwa kula nyama ya nguruwe:-
ISAYA 65:3-4:-" Watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabibu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali; waketio juu ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; WALAO NYAMA YA NGURUWE, na mchuzi wa vitu viinichukizavyo u katika vyombo vyao".
ISAYA 66:16-17:-" Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi. Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; WAKILA NYAMA YA NGURUWE, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema BWANA".

Asije mtu akadanganya kuwa hiyo ilikuwa agano la kale ,sijui ni la wayahudi. Yesu alisema:

"Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.(Mt. 5:17-18).
Waebrania 13:8
''Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele''

Hawezi leo akataze kiti moto alafu kesho aseme ruksa. Huo ni ukigeugeu ambao Mungu alisema yeye hanao.

Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
 
Back
Top Bottom